Munishi amgonga Rais Kikwete na CCM

Munishi amgonga Rais Kikwete na CCM

THE COMMISSIONER

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2012
Posts
267
Reaction score
111
Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Deogratias Munishi amemnanga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ameidhooifisha hadhi ya ikulu kiasi kwamba hata vichaa wangependa kuwa marais wa nchi

Pia Munishi ameuambia umati wa watu wa kata ya Majohe Jimbo la Ukonga kuwa Tanzania imegeuzwa kuwa nchi ombaomba chini ya utawala wa CCM na tabia hiyo imeshamiri chini ya Kikwete ukiacha ukweli kuwa Tanzania inaweza kuwa moja ya nchi za kutoa misaada kwa mataifa mengine kama rasilimali zilizopo zingepata uongozi bora wa kuzipangia matumizi makini.

Munishi aliwaeleza wanachi wa majohe kuwa utawala wa Kikwete unatia fora kwa kufanikiwa kutenga bajeti ya bilioni 50 za kuzurura mataifa ya Ulaya na Marekani kuomba omba wakati wanafunzi wa shule za msingi jimbo la ukonga wanakaa chini, shule za sekondari za ukonga hazina maabara wala maktaba na kwamba ziko ndani ya jiji la Dar es salaam

Alieleza kwa mapana kuwa kwa nchi ya Dhaabu, alamasi, makaa ya Mawe, Uranium, Misitu , bandari ya Dar es salaam na n.k wanafunzi wanakaa chini hawana madawati, maktaba na maabara.

Kuhusu Katiba Mpya, Munishi ameonyesha kumsikitikia Rais Kikwete kwa kuendelea kuona kuna upenyo wa serikali mbili kupitishwa kwenye katiba mpya akidai kuwa kama ikipita hiyo itakua ni katiba ya CCM na washirika wake na si katiba ya Watanzania ambao kupitia tume ya Warioba wamependekeza serikali tatu na kumtaka Rais Kikwete aliyeutaarifu umma kuwa anasubiri kuona maamuzi ya Bunge la Katiba kama yatakuwa ni ya serikali mbili ama tatu kuondokana na mawazo uwewzekano wa serikali mbili kwani haupo na wananchi hawajaufikiria

Pamoja na mambo mengine amehitimisha kwa kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura mwezi Septemba ili kupata kibali cha kufanya mabadiliko kwa kupiga kura za kuiondosha CCM madarakani mwakani.

Munishi pia amewapokea baadhi ya wanachama kutoka CCM ambao wamaeamua kujiunga na CHADEMA baada ya mkutano wa hadhara.

Chini ni sehemu ya picha zilizofanikiwa kupatikana na mwandishi wa habari hii
Majoe 1.jpg majoe.jpg Majoe 2.jpg
 
yaani huyo kamanda aliyekaa demu kamzingua kweli, yuko busy kusomesha.
 
yaani huyo kamanda aliyekaa demu kamzingua kweli, yuko busy kusomesha.

Hahaha hahaha hahaha huyo kamanda mwenye gwanda ya khaki demu kamchanganya akili anasomesha mbaya hahaha hahaha
 
Back
Top Bottom