RGforever
JF-Expert Member
- Apr 3, 2011
- 6,878
- 5,431
Mwanaume mmoja alienda kwa kinyozi kunyoa nywele zake pamoja na ndevu. Baada ya kinyozi kuanza kumnyoa wakaanza maongezi mbalimbali kuhusu utumbuaji majipu, mshahara wa rais, na issue nzima za siasa michezo na burudani.
Walipoanza kuzungumzia suala la Mungu tu, konyozi alikuja juu na kesema kwamba yeye haamini kama Mungu yupo. "Kwanini unasema hivyo? - Mteja alimuuliza kinyozi wake.
Kinyozi akamwambia "Unatakiwa uende mitaani huko uchunguze vizuri ndipo utaamini hakuna Mungu, niambie kama Mungu yupo kungekuwa na wagonjwa na wenye tabu kama hivi? Kungekuwa na watoto wa mitaani? Kama Mungu angekuwepo kusingekuwa na mahangaiko wala maumivu.
Sitaki kuamini Mungu anaependa waja wake aruhusu wapate mabaya kama hayo.Kinyozi akamaliza.
Mteja wa kinyozi akafikiria kidogo lakini hakumjibu chochote kwa kuwa hakutaka kuanzisha mabishano.
Kinyozi akamaliza kumnyoa yule mteja, akalipa na kuondoka. Yule mteja baada ya kuondoka tu nje akakutana na mwanaume aliyekuwa mchafu, nywele ndefu zilizo chafu pamoja na ndevu zilizovurugika. Alionekana mchafu haswa na asiyejitunza hata kidogo.
Hapo hapo yule mteja akarudi tena kwa kinyozi na kuingia ndani, akamwambia kinyozi "Unajua nini? Vinyozi hawapo duniani" Kinyozi akashangaa na akamjibu "Kwanini unasema hivyo? Mimi hapa ni kinyozi na nimekunyoa mimi mwenyewe si muda mrefu, utasemaje vinyozi hawapo Duniani?"
"Hapana" yule mteja aliendelea kudai. "Vinyozi hawapo Duniani kama kweli wangekuwepo Duniani kusingekuwa na watu wenye nywele ndefu na chafu, ndevu nyingi ma zilizovurugika kama yule mtu aliesimama pale nje"
Kinyozi akatizama nje akamwona yule mtu mchafu, akamgeukia yule mteja na kumwambia "Vinyozi tupo, kinachotokea kwa mtu kama yule haji kwetu kutuomba kunyoa."
"Sawa sawa"- hiyo ndio pointi ya msingi. Mteja alimjibu kinyozi.
Mungu pia yupo sana, ila kinachotokea ni kwamba watu hawaendi na kumtafuta yeye, mteja akaendelea kumwambia yule kinyozi;
"Watu wamekuwa busy sana na mambo yao binafsi, anasa za ulimwengu zimewalewesha mno, wamesahau hata kumtafuta Mungu wao. Utaachaje kusema Mungu hayupo?
Nikwambie tu ndugu yangu Kinyozi, wakati ndio huu. Sisi je tutapataje kupona tusipoujali wokovu mkuu namna hii?"
MUNGU YUPO NDUGU KINYOZI.
"Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Alikuja kwake , wala walio wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.- Yohana Mt. 1:10-12.
TO GOD BE THE GLORY.
Nawatakieni Jumapili njema.
I CARE
Share.
Tweve Hezron