Ukwaju, we usitake kukataa, mazingira ya Tanzania yanajulikana kabisa, ukienda mikoa ya Singida na Dodoma vijijini hauwezi kukosa hali kama hii, tena bora hawa inakokotwa na ng'ombe. kuna sehemu nyingine kina mama wajawazito wanakokotwa mpaka na mkokoteni wa tairi moja, tukikubali ukweli kwamba tumesahau kuwekeza baadhi ya sekta maalumu nadhani tutasonga mbele.
Unaongelea suala la mwenyeji kumkarimu mgeni, nimekushangaa sana, sijui unaishi karne gani. kwa taarifa yako Canada ni nchi ya kibepari na hawana utamaduni wa kukarimiana, wao kwa wao hawajikarimu itakuwa mgeni!! na hii sio kwa hao Canada tu bali ngozi nyeupe kiufupi hawajui kitu kinachoitwa ukarimu au utu, kama ilikuwepo hiyo ni miaka 500 iliyopita. wao katika kujenga urafiki na mahusiano kwa ujumla wanachoangalia zaidi ni pesa, ama ni jinsi gani wanaweza kunufaika na huo uhusiano. na wakishanufaika tu basi na urafiki unakomea hapo wanakwenda kuanza kujenga uhusiano mwingine.
Barrick Gold wale ni wacanada, hivyo ni lazima wampe treatment ya kutosha huyu ****** ili kulinda maslahi yao yaliyopo Tanzania, naye ****** huenda akavimbiwa kichwa kwa kudhani kwamba anapata special treatment!
Kumbe ukweli ni kwamba hawa jamaa huwa wana strategy kali sana, kwanza wanamsoma mtu wanayedeal naye, wakishagundua tu udhaifu wake , Kwisha kazi! na kama unavyojua huyu ndugu yetu ana udhaifu wa aina kedekede , ikiwamo udhaifu wa kupenda kuuza sura. hebu angalia hapo chini:
Hapa analainishwa!
sasa hebu niambie, kikwete anachezea timu gani mpaka apewe jezi?
Hapa kalainika
View attachment 67240
kama picha zinavyojieleza hapo juu, ukiangali hapo anaposaini utaona kwamba nyuma yake kuna wanasheria, upande wa kushoto na kulia kuna njemba hizo zimevaa badge za vyeo vya kijeshi, inaonekana hao wote hapo ni top officials , hivyo moja kwa moja naamini hapo kuna jambo kubwa sana linafanyika , iwe kati ya kuongeza msamaha wa kodi kwa makampuni ya kigeni yanayochimba madini, ama JK ndio hivyo tena anasaini mkataba mpya wa madini. utashangaa utakaposikia kwamba wamepewa kuchimba madini kwa miaka 200 na msamaha wa kodi juu, lolote linawezekana kwani Tanzania karibu kila kona kuna madini na yanachimbwa kwa kasi, tukija kuamka tutakuta kweupe.