Huko Anfield, mashabiki wa Liverpool walimwita Robbie Fowler kuwa ni mungu wao. Kuna baadhi ya wachambuzi wanaamini pengine hiyo ndiyo laana inayoifanya timu hiyo hadi sasa kushindwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England licha ya kukaribia kufanya hivyo zaidi ya mara mbili.
Msimu huu wanaonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa, lakini kama watashindwa basi itabidi waende kutubu kutokana na kumwona Fowler kama mungu wao. Kilichowafanya Kop pengine kumfanya Fowler awe wanavyofikiria wao ni ule uwezo wake wa kufunga mabao, ambapo rekodi zinaonyesha kwamba staa huyo amefunga hat-trick tisa kwenye Ligi Kuu England. Hat-trick yake ya mwisho Fowler alifunga Boxing Day, 2001.
Rudi Nyumbani Kumenoga.