Mungu ni mwema kila wakati

Mungu ni mwema kila wakati

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,195
Asante baba leo ni siku nyingine,Nashukuru kwa pumzi na nguvu ulizonipa leo,naomba pia nifungulie na ridhiki yangu ili ata kile kidogo nitakachopata kinisaidie mimi pamoja na jamaa zangu.

Kuna ambao walitamani kuiona leo lakini kwa Neema zako wamerejea kwako wape pumziko la milele,
Kuna ambao Walitamani kuamka na Afya Njema lakini Maradhi ya mwili yamekuwa kisababishi wape uponyaji wako.

Mimi ni binadamu kuna muda nakosea naomba unisamehe nipe Rehema zako ili nilitangaze jina lako na kusema wewe ndio mkuu siku zote.

Vitu vyote vitapita lakini ukuu wako hautapita kamwe .

Nawatakia ijumaa njema yenye baraka.

Ameni.

Mungu ni mwema kila wakati.
 
Heeee kumbe mnadini zenu!!!!
Mnavoletaga uzi wa utumbo nazaniaga hamumjui mungu kumbe makusudi tu
Mkuu sometime we need to Refresh our mind na ndio maana tukapewa chaguo.
 
kumbe ziro mda mwungine unakuwaga mzima ?
nimeshangaa sana kumbe kuigiza unaweza
Aaha aaha mkuu Mungu ana maksudi yake hakuna siku anaekosea kwenye uumbaji wake always God is perfect.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom