Mungu mbona umetuacha hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu mbona umetuacha hivi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mmakonde, Dec 24, 2010.

 1. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mungu wetu wa Mapendo,mbona unaiacha nchi yetu inakwenda mrama?
  Ni nchi yenye amani tangu uhuru toka kwa Waingereza!Jirani zetu wamepigana,wameuana lakini UCHUMI wao na maendeleo ya wananchi wao bado yanatuzidi.Mfani ni kirani zetu wa RWANDA.

  Mwalimu Nyerere alitupa Mkapa na kutuhakikishia kuwa ni mtu safi.Na sisi tukasema ni chaguo lako!Tulifikiri mzee wa Ruksa alikuwa amepotoka kidogo,hakujua rule of law na heshima ya IKULU.Waarabu na Wahindi wakawa ndio kwao pale.Mkewe wa Mzee Ruksa wa Kiarabu ndio akawa mtu wa deal.Tuliokuwa Dar miaka ile tuliona mara ya kwanza First Lady anajihusisha na biashara,hata tetesi lile jumba la kumetameta opposite na Maktaba ni lake.
  Oh my God
  Akaja Mmakonde mwenzangu,chaguo lako!!!Yeye na familia yake wakaanza kuuza kila kitu cha serikali.Akafungua kampuni akiwa IKULU.Akanunua kiwanda cha Kiwira kutumia benki zetu.Ufisadi ndio ukaanza rasmi kila ngazi ya serikali.Akanunua fake RADAR.BOT Twin Tower!Meremeta.Presidential JET.Migodi mikataba fake.Tenda mbovu za vifaa vya jeshi,IPTL aka Dowans now etc etc.
  Muda wake ukaisha,hakuna mtu wa kumgusa mpaka leo.

  Akaja JK,tukafiri yeye ana nidhamu ya kijeshi kueza kuinusuru nchi.Ni tofauti kabisa.Ameitumia ndege ya Rais vizuri ku globe trotting .Ni aibu kwa nchi maskini kama Tanzania kuwa na life style hii.Kesi zote alizoacha Mkapa ,hazijafika mbali .Lowassa,Rostam,Karamagi,Mkono,Vijisenti & gangs bado wanafurahia matunda ya ufisadi na kuwa mabilionea wa kwa kuiibia serikali ya Tanzania.Mbaya zaidi Wanasheria wetu ndio wanashirikiana na viongozi wetu kuiibia nchi.REX attorneys,IMMA advocates na MKONO advocates wamechukua billioni nyingi eti kutetea clients wao.

  Mungu wetu tumekukosea nini?Umewapa uwezo watu wachache kuifilisi nchi na resources zake bila kujali maisha ya millions ya Watanzania ambao,wanalalia ngozi vijijini,hawana maji na umeme,hawana madaktari wazuri!!!

  Mungu wetu ,uchaguzi umepita,tumeona kwa mara ya kwanza jinsi gani ,elites wa chama tawala na UWT kuwanyima wananchi haki zao.May be Mungu wetu una mpango na nchi yetu,tuambia wazi tufanye nini,ili cake ya nchi ,iliwe na wananchi wote.

  Tunauaga mwaka huu wa 2009,miaka 49 tangu tupate uhuru.Mungu wetu tunakuomba utume mwanga,tutakapofika 50,tuwe tumepuvuka ,uwaadhibu mafisadi wote ambao wanaiibia nchi yetu kila siku through tenda za serikali,kodi,madini etc.

  Kama tumekukosea tangu UHURU,tunakuomba utusamehe.Tupe nguvu tukabiliana na mafisadi bila ya kumwaga damu.

  Bila shaka utazisikia sara zetu zitimie 2011!
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Aamin Aamin Aaamin!!!
   
 3. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Chukua hatua,dhamani ya nchi yako Mungu ameiweka mikononi mwako. Kama ukiendelea kulalamika bila kuchukua hatua madhubuti hakuna kitakachofanyika. Kama wapigania uhuru wangeacha wakoloni waendelee kututawala, tungekuwa mikononi mwa Waingereza mpaka leo. Great people of Tanzania can make a change if they want.
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mungu hajatuacha, sisi ndio tumemuacha.Tunacho ona sasa Tanzania, ni ghadhabu ya Mungu juu yetu baada ya sisi kumwacha.Tumemkumbatia shetani badala ya kumpinga, kama Mungu alivyo tuagiza(Yakobo4:17-18).Kwa ufafanuzi zaidi if you are interested, go to Romans1:18,21-31, utaona ukweli juu ya fate yetu,inatisha sana.Frankly speaking, I don't see any hope for Tanzania, mpaka tugeuze njia zetu.
   
 5. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mungu anasaidia wale wanaojisaidia. Na wala siyo wale wanaimba huo wimbo wa amani na utulivu wakati wototo wao wanazidi kupukutika kwa utapi wa mlo na maradhi yanayotibika. Kama siyo unafiki uliwahi kuona wapi mtu mwenye njaa miongoni mwa wanaokula na kusaza akawa na amani.
   
 6. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mungu katupa akili na utashi. Hajatuacha kamwe. Tumeshindwa kuwawajibisha wanaotunyanyasa kwa woga wetu wenyewe.
   
 7. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mungu wetu,wakati tunasheherkea Xmas na mwisho wa mwaka tuepushe na GREED has viongozi wetu.
  Wabunge wetu wawakilishe mawazo ya wananchi na kusikiliza matatizo.

  Mungu wetu viongozi wa dini uliotupa Tanzania hawafai kabisa,wameshindwa kutupa morality kabisa.Hao hao wanaotoa sadaka misikitini na makanisani ni mafisadi wakubwa.Viongozi wa dini wameshindwa kuwakemea viongozi maana wote niu status quo.Watoto wao watafunga ndoa makanisani/misitini kwa mbwembwe ,bila viongozi wa dini kusema kuwa hii ni kashfa kwa nchi maskini kama Tanzania.
  Send off/reception zitafanyika Diamond Jubilee bila ya aibu!

  Mungu wetu umetupa GREED ya hali juu.Tuko obsessed na magari ya kifahari.Hatujali mazingira tunayoishi.Mbunge na V8 au afisa wa serikali anaona amefika kwako na yuko mbinguni.
  Mpaka leo nikaangalia picha ya supermodel Naomi Campbell akitembelea hospitali ya Temeke,na WAJA WAZITO wakilala sakafuni,machozi yananitoka.
  Kumbuka temeke iko jijini ,je huko vijijini itakuwaje.Si ajabu Mkuu wa hospitali hiyo anatembelea V8 shangingi.Angalia misafara ya viongozi wetu na magari ya kifahari ,wakati hospitali hazina dawa.
  Mungu greed yetu inavuka hata ya nyani.

  Mungu wetu ulitupa nchi nzuri ,maziwa ya Nyasa,Nyanza ,Tanganyika,Bahari ya Hindi etc.Ukatupa dhahabu,almasi,coal etc bila kusahau katani,pamba,chai,mkonge,karanga ,wali etc.Umetunyima ELIMU ya kujua zuri na baya,elimu ya kujua maendeleo ni nini.
  Mungu wetu viongozi wet u wengi wanafikiri kuiba serikali ni maendeleo,kujenga ghorofa Masaki/Mbezi ni maendeleo,kuwa na Phd fake ni maendeleo ,kuendesha 4WD jijini Dar Es Salaam ni maendeleo.Hivyo kila mtu hata wa chini lengo lake ni hilo.Nchi za wenzetu ,4wd kuwa jijini sio fashionable,otherwise utakuwa taxed.Sio siri 4WD zina emissions kubwa,mbaya zaidi wasomi wetu wa MUHAS ,hawajawahi kufanya study how increase ya 4wd jijini Dar na magonjwa ya pumu kama arthma etc

  Mungu wet mbona umetupa greed ya kusahau kuwa maendeleo sio hayo tu.
  Nimepata wasaa wa kutembelea western europe na kuona maendeleo haya:
  1.Kila mtu ana access ya Medical doctor-sio medical assistant wa darasa la saba/form 4
  2.Kila mtu ana access ya Dentist-sio dental assistant
  3.Kila mtu ana choo cha ndani cha kuvuta,hakuna kujisaidia ovyo
  4.Kila mtu ana uwezo wa kula chakula hata kama hauna uwezo
  5.Kila nyumba ina UMEME na mengineo mengi

  Baada ya miaka 49 ya UHURU,Mugu wangu bado tunaface mgao wa UMEME!

  Mungu wangu umetunyima ELIMU ya haki.
  Mungu wetu labda umewapendelea watu wa aina fulani.Wanapozungumzia global warming sisi tunacheka cheka na kuhudhuria mikutano ya kimataifa tu.
  MVUA hazinyeshi,mabwawa hayajai maji,so hatuna UMEME kwenye HEP kama Mtera.Najiuliza nchi gani za kuendelea zinategemea HEP katika umeme wao?hakuna.Wazungu wakati wanajenga Mtera walijua hili,sasa tumeachwa mataa!Mungu wetu kwa nini haukutupa mwamko huu?
  Ndio maana tuna TANESCO/IPTL/Dowans etc

  Lakini tuna JUA zuri tu ambalo linaweza kuwasha umeme nchi yeti milele.Mungu wetu tupe uwezo na akili hasa kwa waandisi wetu wajue jinsi gani ya kutuletea SOLAR ENERGY milele.Mungu unatuadhibu na MGAO wa UMEME baada ya miaka 49 ya UHURU.Hatustahili hili.

  Mungu wetu 2011 uwe mwaka wetu!Tupe akili na uwezo
   
Loading...