Mungu kama Mfanyabiashara au Mwekezaji Mahiri

Mungu kama Mfanyabiashara au Mwekezaji Mahiri

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,777
Reaction score
6,907
Siku chache zilizopita nilikuwa nasikiliza mafundisho ya Mwalimu Christopher Mwakasege akagusia jambo moja lilinisisimua sana. Alipolisema kwa mara ya kwanza nadhani wengi walishtuka ila alipokuja kutoa mifano na kuchambua lilikuwa moja ya jambo kubwa nililowahi kujifunza kwenye Biblia. Utaona kabisa liliwagusa wengi.

Kiufupi alisema, Mungu ni mwekezaji au mfanyabiashara mzuri au makini asiyependa hasara. Katika uchambuzi wake akasema akiwekeza kwa mtu kwa kumpa kitu fulani ndani yake mfano kipaji, ujasiri nk. atahakikisha amekifuatilia hadi amerudisha 'hela yake' na faida juu (hayo ya mwisho ni maneno yangu mwenyewe ila maana ndiyo hiyo hiyo). Hapendi kuona 'hela' yake inatumika visivyo.

Akatolea mifano ya Jonah aliyejaribu kukimbia wito wake hadi akamezwa na samaki. Akatolea pia mfano wa Sauli aliyekuwa anawatesa wafuasi wa Yesu hadi alipotokewa na Yesu.

Nimetafakari haya mafundisho na mimi nimepata vitu vya kuongeza nikimfikiria Mungu kama mfanyabiashara na mwekezaji na nini naweza kujifunza kutoka kwake:

1. Mungu huwa anawekeza kwa vijana wadogo kabla hawajakomaa na kuwa na mawazo mgando.

Hapa namaanisha wale ambao bado hawajawa tayari. Anawapa yeye mwenyewe uzoefu anaoona utawasaidia kwenye kazi anayowaandaa kufanya. Mfano mmoja ni kwa Daudi. Samuel alipokwenda kwa nyumba ya Yese, aliwakataa kaka zake wooote akaenda kumchukua dogo ambaye hata nyumbani hakuwepo.

Mfano mwingine ni kwa Yusufu aliyepewa ndoto iliyowakasirisha kaka zake.

Kuna msemo unasema 'hauwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya'.

Nikiliongelea hili suala katika sura ya jamii zetu, wasomi wengi wanapoenda kuomba kazi wanaenda na fikra ya kwamba tayari wanajua kila kitu na wanakuwa na kiburi fulani hivi. Wanataka mishahara mikubwa wakati hawana hata uzoefu.

Mungu akiwa kama mwekezaji makini anatambua hilo tatizo lipo, badala yake anaenda kuchukua yule aliyedharaulika ndiyo anamuinua. Anajua huyo mtu atakuwa mnyenyekevu na msikivu.

Isaya 53 inazungumzia kwa kina aina ya watu ambao Mungu anapenda kuwainua ili yeye atukuzwe. Neno lina nguvu sana hili. Na wewe unapotafuta watu, angalia wale watakaothamini nafasi unazowapa. Ukiwainua hao watakukumbuka daima. Ni rahisi sana kutambua watu wenye kiburi, dharau na jeuri ambao hawatathamini nafasi unazowapa au ambao mbele ya safari watakugeuka.

2. Mungu anaanza na mtaji mdogo halafu anaukuza taratibu.

Hili linajielezea. Mungu anakuwa very specific nini anataka kutoka kwako vingine anakuletea yeye mwenyewe. Inaonyesha Mungu anaamini sana katika uzoefu lakini anataka uzoefu uupate kabla ya kazi. Hataki kukulipa wakati bado unajifunza! Kina Yusufu na Daudi ni mifano mizuri.

Mfano mwingine ni Musa. Musa alipodhani hana zana za kutosha kufanya kazi, Mungu hakwenda 'kukopa benki kumuongezea mtaji', alimuuliza ana nini? Musa alivyosema ana mti tu, Mungu akautumia mti huo huo kumaliza kazi. Katika Isaya 52:3, Mungu anasema watu wake waliuzwa bure na watakombolewa bila fedha. Mungu hatumii hela yake ovyo ovyo kabisa.

Utaona tena na tena jinsi gani Mungu hapendi kutumia gharama na watu wengi zaidi ya inavyobidi. Mungu ni afadhali awe na Komando mmoja aliyefundwa akafundika kuliko kuwa na watu wengi ambao wengine hawako fit kwa kazi. Unakumbuka alivyomwambia Joshua apunguze watu wake? Ukiwaangalia kina Yusufu, Daudi, Joshua, Musa, Samson na Yesu kama makomando wa kijeshi hautakuwa unakosea. Wengi wana limit Biblia kama kitabu cha mambo ya kiroho tu, lakini kimesheheni mafundisho na mbinu za kijeshi, za biashara, za maisha na mahusiano, nk.

Kwa kumalizia point hii, kuna watu wanasema biashara ni vita na ni vita kweli. Hakikisha hauna wafanyakazi wengi zaidi ya unaowahitaji.

3. Mungu anajua kutoa motisha kwa 'wafanyakazi wake'.

Mifano ipo mingi. Kuanzia Musa aliyemuuliza atafanyake kazi anayomtuma wakati yeye ana kigugumizi, Yeremia aliyesema atawezaje wakati yeye ni mtoto hadi Yesu aliyeomba kikombe kimuepuke hadi Mungu akawatuma Elia na Musa kumpa motisha. Inaonyesha Mungu akishawekeza kwako, akiona unasitasita hakutumbui, anakupa motisha kwamba unaweza, songa mbele.

Pale anapoona kweli huyu mfanyakazi wangu amefanya kila awezalo ila amekwama, anaingia mwenyewe mzigoni. Na ili kuonyesha bado anathamini mchango wako, bado atakuhusisha. Mfano wa hili ni Musa tena na mapigo yaliyowapata Wamisri.

4. Mungu akikupa kazi hatakuacha uifanye yote mwenyewe. Atakusaidia kuikamilisha.

Ili kuhakikisha kazi inaenda kwa ufanisi na uwekezaji wake unaenda sawa, Mungu atakupa kazi ya msingi uifanye wewe ila makorokocho mengine anakurahisishia kwa kuyafanya yeye mwenyewe ili ufocus kwenye jambo la msingi.

Hapa nitatolea mfano wa Nuhu. Mungu alipompa Nuhu kazi ya kujenga safina alimpa maelekezo ya wanyama na ndege na idadi yao wa kuingia nao. Lakini ukisoma kwa makini utagundua alichofanya Nuhu ni kujenga tu safina na kuwaingiza wanyama na ndege ndani pamoja na familia yake kama Mungu alivyoagiza ila hakuhitaji kwenda kuwatafuta hao wanyama na ndege. Mungu aliwaleta hao wanyama na ndege kwa Nuhu. Embu fikiria ingemchukua muda gani kama ingebidi aende kuwatafuta yeye mwenyewe. Kuna somo muhimu sana hapa. Bado natafakari hili neno na naandaa maandiko mengine.

5. Mungu anaweka lengo la faida. Likitimia anatumia sehemu ya faida kuanzisha biashara zingine nyingi, ile ya mwanzo inabaki kama biashara mama.

Kwa watu wanaojua mambo ya biashara kuna kitu wanaita Parent Company na Subsidiaries. Biashara mama ikishajijengea jina unatumia ile sifa iliyojijengea kufungua biashara zingine.

Mfano mzuri ni wa Yesu. Baada ya Yesu kumaliza kazi yake, amebaki kama 'kampuni mama' iliyomsaidia Mungu kusambaza Neno lake dunia nzima.

Hii concept nchi zilizoendelea wanaitumia sana ingawa kwa huku kwetu bado haijaingia sana. Mfano wa kampuni za namna hiyo ni Acacia vs. Barrick Gold. Kuna njia nyingine inatumika sana inayofanana na hii inaitwa Franchising ndiyo haya makampuni kama KFC na McDonald's na Pizza Hut, kutoa mifano michache.

6. Utafiti - Kupitia utafiti wa Mungu, dunia tunayoijua leo ikaumbwa.

Ukisoma Biblia katika kitabu cha Mwanzo mstari wa kwanza kabisa, kinaonyesha Mungu tayari alishaziumba mbingu na nchi. Unaweza kusema alipoona ukiwa, utupu na giza vimetanda akaona kuna maboresho yanaweza kufanyika na ndiyo kazi aliyoifanya kwa siku sita.

Ukiangalia kila baada ya siku moja, neno linaishia na 'Mungu akaona ya kuwa ni vyema'. Mimi kwa maoni yangu naona kama kwa lugha ya kibiashara, Mungu alikuwa anaenda akiboresha kupitia rafiti. Ndiyo maana hata alipomfanya Adam baadae akaona siyo vyema awe peke yake, ndiyo akampatia Hawa. Baada ya siku sita kuisha akaangalia alipofikia akaona 'bidhaa iko vizuri na iko tayari kuingia sokoni'.

Katika biashara, makampuni mengi duniani, hasa makubwa yanawekeza sana kwenye tafiti. Haya makampuni yana vitengo vya R&D (Research and Development) na wanavipa hela nyingi sana. Hata nchi mbalimbali, mfano Israel ambao ni moja ya nchi zinazoongoza kwa uvumbuzi wa teknologia mpya inajua sana umuhimu wa tafiti. Kupitia tafiti ndiyo bidhaa mpya zinagunduliwa au zile za zamani zinaboreshwa.

Lakini hili halihitaji kuwa tu kwa makampuni makubwa kama Apple au Google. Hata wewe katika biashara yako ndogo usiache kufanya utafiti. Je kuna jambo moja zaidi unaweza kulifanya kuleta wateja wapya? Halafu jaribu hilo jambo uangalie. Ukiona wameongezeka au wale wa zamani wanalipa zaidi, sema ni vyema, iweke kwenye biashara halafu nenda kwenye utafiti unayofuata. Ni hadi hapo utakapoona una 'perfect product' ndiyo upumzike.

7. Fungu la kumi na kubakisha faida iliyobaki kwenye biashara.

Kuna tatizo linatusumbua wengi wafanyabiashara ndogondogo au wale wanaoanza. Nalo ni kujua kiasi gani ule na kiasi gani kibaki kwenye biashara. Wengi hatujiwekei mshahara maalumu, muda wowote unatoa unachotaka, wewe si ndiyo bosi bwana!

Mungu anajua hilo ni kosa kubwa. Aliwaambia Waisrael fungu la kumi ni lake. Yeye wala hataki zaidi wala hataki kuwa anakuja na kujichukulia kama vile chuma ulete! Anajua akitaka zaidi au akichukua bila mpangilio ingawa vyote ni vyake utaumia na biashara itakufa na kesho utashindwa kupeleka hilo fungu la kumi.

Niliwahi kumsikia mfanyabiashara mmoja mkubwa anaitwa Steve Masiyiwa, anayemiliki Kwese TV akisema, hata kama biashara yako ni ndogo, jiwekee mshahara na uwe na nidhamu ya fedha ya biashara. Hata kisheria, biashara ni 'nafsi' inayojitegemea.

8. Mungu anaona ushindani wa shetani ni mzuri kwa ajili ya utukufu wake

Wote tunajua Mungu hashindwi kitu na angetaka angemuangamiza shetani toka zamani. Lakini ameamua kumuacha ili tuweze kumjua yeye na ukuu wake.

Katika biadhara ni hivyo hivyo. Hautakiwi kuogopa wala kuchukia wapinzani wako. Ukicheza karata zako vizuri ukaonyesha umahiri wako watu watakuja kwako tu. Ndiyo maana wenye uelewa wanaenda kufungua biashara sehemu ambapo wengine wanafanya biashara hizo hizo. Hii kitu zamani na mimi nilikuwa sielewi na nilikuwa naona si jambo zuri ila baada ya kufunuliwa nimeona ni vizuri kwa biashara yako. Wanachokosea au kusahau wengi ni kutokwenda hatua moja zaidi kutofautisha biashara yako ili watu wakija eneo lile waone utofauti. Hilo wengi hawafanyi.

Upinzani unachangamsha soko. Ndiyo maana ukileta kitu kipya kabisa ambacho watu hawajawahi kukitumia, unaweza kupata tabu sana kufanya biashara hata kama hiyo bidhaa au huduma ni wazo zuri na ina manufaa makubwa kwa jamii. Utatumia nguvu nyingi kuelimisha wakati kama ungekuwa na upinzani ni kama mnagawana gharama.

Hii concept ya ushindani inatumika sana na nchi zilizoendelea. Ndiyo maana 'monopoly' ni kinyume cha sheria kwenye nchi nyingi. Na ndiyo maana concept ya 'contrast' inatumia sana kwenye muziki, filamu, photography na hata siasa.

Miaka fulani iliyopita kuna dada alikuwa anaendesha magazine moja hapa Dar es Salaam (jina limehifadhiwa). Kuna siku tulikaa tunaongea nikamshauri aanzishe lingine au mengine ili kuchangamsha soko kwa sababu mambo ya magazine hayakuwa na soko sana Bongo na nadhani mpaka sasa hivi ni hivyo hivyo. Hakunisikiliza. Sijui lile gazeti liko wapi siku hizi!

Simba siyo Simba bila Yanga! Chanya siyo chanya bila hasi. Wachina wana kitu wanaita yin na yang. Unahitaji wapinzani wako ili ufanikishe malengo yako!

9. Mungu anatumia rasilimali za wapinzani wake kufundisha wafanyakazi wake.

Hii kitu ndiyo utajua Mungu kweli ni level nyingine kabisa. Mungu ana mtindo wa kutumia rasilimali za wapinzani wake kupanua soko lake. Cha kuchekesha wapinzani wake hawajashtuka mpaka leo lakini Mungu amefanya hivi tena tena na tena na mpaka leo bado anatumia mbinu hii. Kweli Mungu ni 'savvy investor'.

Hii ina faida kubwa tatu.

Kwanza, inamuwezesha Mungu kutotumia rasilimali zake mwenyewe. Mungu ndiyo tafsiri hasa ya mfanyabiashara makini. Wapinzani wake watawekeza kweli kuchukua kile kilicho cha Mungu lakini mwishoni Mungu anarudisha kile kilicho chake tena kikiwa na uzoefu na uelewa zaidi, kwa maana nyingine kikiwa bora zaidi na tena anakirudisha bure.

Mfano mzuri ni Ayubu. Shetani eti anaenda kwa Mungu na waziwazi anamwambia Mungu amuachie mmoja wa wafanyakazi wake akamtumikie yeye. Hivi shetani anamuonaje Mungu? Mungu akijua nini anaenda kufaidika anamuachia Ayubu achukuliwe. Utaona wakati Ayubu anapitia kipindi kigumu alikuwa hajapitia mambo kama yale kwa hiyo kupitia yale amemuelewa si tu Mungu, bosi wake wa zamani lakini kamuelewa pia shetani, bosi wake mpya. Embu waza ni uzoefu kiasi gani Ayubu alioupata Mungu alipomrudia. Ndiyo maana alienda kupata mali na utajiri zaidi ya aliokuwa nao mwanzo.

Mfano mwingine ni Yesu. Ni rasilimali kiasi gani zilitumika kumsulubu na kumtesa Yesu. Mwisho wa siku Yesu aliweza kumuelewa Mungu Baba yake lakini pia alimuelewa vizuri zaidi adui wa Mungu kwa sababu shetani huyo kwa ujinga wake aliruhusu adui yake apate access ya mafile ya siri sana ya biashara yake ambayo ni KIFO. Embu waza wewe mshindani wako anakupa access ya siri zake zote, mbinu zake, nk. Ndiyo maana baada ya hapo jina la Yesu linashinda kila siku mbele ya shetani.

Pili, kwenye biashara kuna kitu wanaita 'Competitive Intelligence'. Hii ni kufanya utafiti wa kuhusu wapinzani wako, wanafanya nini, mbinu zao za biashara ni zipi, nk. Embu angalia Mungu alivyomtumia Sauli. Siku nyingi Sauli alitumika kuwaua wafuasi wa Yesu. Mungu ni Master Competitive Intelligence Analyst.

Chukua muda kujifunza mbinu wanazotumia wapinzani wako. Hata ukiweza, penyeza mtoto wa mjomba afanye kazi huko ndani kwa muda ikiwezekana apande vyeo kabisa. Akija kutoka huko, mshindano wako atapigwa na butwaa na hataweza kukushika tena. Nchi nyingi zinapopambana na ugaidi na madawa ya kulevya wanatumia mbinu hizi sana. Kuna hata vyama vya siasa wanatumia hii mbinu sana! Hayo tuyaache, nimeona tu nigusie jinsi gani mbinu hii ni pana na yenye ufanisi mkubwa.

Tatu, mfanyakazi wako akifanya kazi kwa mpinzani wako anakuwa na nafasi ya kuiona biashara yako kutokea nje kwa hiyo ataielewa zaidi pale atakaporudi kwako. Wakati Ayubu anapata mapigo yale ya shetani aliweza kumtafakari Mungu na kumjua zaidi kuliko mwanzo. Yale majadiliano na mabishano aliyokuwa anafanya na ndugu zake yalimjenga sana kiuelewa na kumjua Mungu kuliko hapo kabla.

Nadhani kitabu cha Ayubu kuna mafunzo fulani wengi hawajayaelewa. Napanga siku kukichambua kwa uelewa wangu.

10. Mungu anachukia wafanyakazi wakaidi au wakorofi. Hao hana msalia mtume nao!

Mungu ana uvumilivu sana na ni mwenye huruma. Nimeongelea hapo juu jinsi anavyotoa motisha kwa wafanyakazi wake wanaositasita na wasiojiamini. Ila linapokuja kwa mfanyakazi ambaye kwa makusudi anaenda kinyume cha maagizo yake kama vile kutaka kushindana naye, aisee namuonea huruma mtu huyo!

Ukisoma Isaya 45:9, Mungu anasema 'Ole wake ashindanaye na Muumba wake! kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! udongo umwambie yeye aufinyangaye, Unafanya nini...' Adam alipomkosea Mungu na tena kwa ujeuri kabisa anabishana naye badala ya kuomba msamaha, Mungu alimpa adhabu kali sana. Sidhani kama katika Biblia kuna sehemu nyingine Mungu amempa mfanyakazi wake adhabu kama aliyopewa Adam. Yaani ukitaka kujua ni jinsi gani Mungu alikuwa na hasira na Adam, alimfukuza Adam kabla hata hajatafuta mfanyakazi mwingine wa kufanya kazi aliyoiacha, aliona ni bora bustani ifungwe tu na alileta mlinzi kuhakikisha Adam hakanyagi tena!

Kwenye biashara jaribu kuwa na huruma na staha na wafanyakazi wako mfano. Ila ukiwa na mfanyakazi mkaidi anayedharau au kukebehi maagizo yako, huyo fyekea mbali na usimchekee wala kumuonea aibu. Kama mfanyakazi ameonyesha bila shaka ni mtiifu kwako na ameshafanya kazi yako kwa muda mrefu bila matatizo, ikitokea mmetofautiana kwa jambo fulani, huyo msikilize, anaweza kuwa na jambo jema la kukwambia. Unaona jinsi Mungu alivyoshauriana na Musa pale Mungu alipotaka kuwamaliza wana wa Israel aanze upya. Mungu alimuheshimu sana Musa. Hata wakati wa Sodoma na Gomora, Mungu alishauriana na Abraham ingawa kwa hili la Sodoma Mungu hakuukubali ushauri wa Abraham. Lakini Abraham alitoa ushauri kwa heshima bila kebehi wala dharau.

Chukua ulichojifunza halafu weka katika biashara zako utaona matokeo.
 
Kwann ww upo?!
Mm nipo ili niishi. Nathibitika kuwa nipo kwa sababu unaweza kuniona na kusikia sauti yangu ukiachilia mbali matendo ambayo nayafanya mfano kuandika huu ujumbe. Viashiria gani vitatufanya sasa tuamini Mungu yupo??
 
Hili ni moja ya majawabu yakinifu sana

Asante Mkuu
ili uelewe ishu hizi unapaswa uyaangalie maisha yako tokea ulipojitambua mpaka sasa hivi na kule uendako. Ndio utaelewa ile kauli iliyosema "NIKO AMBAYE NIKO"
 
1. Mungu huwa anawekeza kwa vijana wadogo kabla hawajakomaa na kuwa na mawazo mgando.

Hapa namaanisha wale ambao bado hawajawa tayari. Anawapa yeye mwenyewe uzoefu anaoona utawasaidia kwenye kazi anayowaandaa kufanya. Mfano mmoja ni kwa Daudi. Samuel alipokwenda kwa nyumba ya Yese, aliwakataa kaka zake wooote akaenda kumchukua dogo ambaye hata nyumbani hakuwepo.

Mfano mwingine ni kwa Yusufu aliyepewa ndoto iliyowakasirisha kaka zake.

Kuna msemo unasema 'hauwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya'.
Mkuu acha kabisa kukariri vitu wewe, huwezi kumwelewa MUNGU hata siku moja na akili zake na mawazo yake hayachunguziki. Ukisema eti, MUNGU huwa anawekeza kwa vijana wadogo mimi nakataa, fahamu kwamba MUNGU aliwekeza kwa MUSA akiwa mzee kabisa wa miaka 80! MUNGU alimchagua Ibrahimu akiwa mzee kabisa wa miaka 99 na NUHU alikuwa na zaidi ya miaka 500 pale alipoanza kuongea na MUNGU.
 
Hili ni moja ya majawabu yakinifu sana

Asante Mkuu

Mkuu wanaopinga uwepo wa Mungu si kwamba tuu wanakufuru bali pia wanathibitisha kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana. Wao hutegemea akili ya nyama wasijue kuna zaidi ya ubongo. Ubongo huweza kuliwa na wadudu lakini akili ya rohoni kamwe haiathiriki
 
Mkuu acha kabisa kukariri vitu wewe, huwezi kumwelewa MUNGU hata siku moja na akili zake na mawazo yake hayachunguziki. Ukisema eti, MUNGU huwa anawekeza kwa vijana wadogo mimi nakataa, fahamu kwamba MUNGU aliwekeza kwa MUSA akiwa mzee kabisa wa miaka 80! MUNGU alimchagua Ibrahimu akiwa mzee kabisa wa miaka 99 na NUHU alikuwa na zaidi ya miaka 500 pale alipoanza kuongea na MUNGU.

Mkuu yeye kamuelezea kwa uelewa wake na si kosa. Ni kama kanisani kila mmoja hutoa sadaka kwa kadiri alivyojaliwa ndivyo hata katika uelewa na utoaji maoni. Yeye uelewa wake umeishia hapo. Biblia inasema "Usihukumu usije ukahukumiwa" Japo hujahukumu. Hivyo mtu akisema ajuavyo si kosa, kosa linabaki kwa mwenye uelewa kujifanya yeye ni bora kuliko mwingine. Kosa hilo hufanywa na waumini wengi wa dini
 
Neno la Mungu halina mipaka (is infinite). Mifano niliyotoa ni dhahiri ina ukweli lakini pia mifano uliyoitoa ni dhahiri na ina ukweli lakini yakiwa na mafundisho yake tofauti bila kukinzana na yale ya mwanzo. Ndiyo maana pia neno hilo hilo ukilisoma katika nyakati tofauti unapata maana tofauti ingawa maana hizo huwa hazikinzani. Maana ya Neno inakujia kwa wakati mahsusi upate ujumbe unaostahili kwa wakati huo.

Siyo kosa kuchunguza matendo ya Mungu. Bila kufanya hivyo utapataje mafundisho? Kwani mahubiri ya walimu na wachungaji ni nini zaidi ya tafakuri ya matendo ya Mungu?

Kuongezea, Mungu aliwajua Musa na Abraham kabla wao hawajajua wito wao ni nini. Ndiyo maana Mwalimu Mwakasege alitolea mfano wa Sauli. Mungu alimwambia Yeremia alimjua kabla hata hajaanza kuwa kiumbe tumboni mwa mama yake!
 
Siku chache zilizopita nilikuwa nasikiliza mafundisho ya Mwalimu Christopher Mwakasege akagusia jambo moja lilinisisimua sana. Alipolisema kwa mara ya kwanza nadhani wengi walishtuka ila alipokuja kutoa mifano na kuchambua lilikuwa moja ya jambo kubwa nililowahi kujifunza kwenye Biblia. Utaona kabisa liliwagusa wengi.

Kifupi alisema Mungu ni mwekezaji au mfanyabiashara mzuri au makini asiyependa hasara. Katika uchambuzi wake akasema akiwekeza kwa mtu kwa kumpa kitu fulani ndani yake mfano kipaji, ujasiri nk. atahakikisha amekifuatilia hadi amerudisha 'hela yake' na faida juu (hayo ya mwisho ni maneno yangu mwenyewe ila maana ndiyo hiyo hiyo). Hapendi kuona 'hela' yake inatumika visivyo.

Akatolea mifano ya Jonah aliyejaribu kukimbia wito wake hadi akamezwa na samaki. Akatolea pia mfano wa Sauli aliyekuwa anawatesa wafuasi wa Yesu hadi alipotokewa na Yesu.

Nimetafakari haya mafundisho na mimi nimepata vitu vya kuongeza nikimfikiria Mungu kama mfanyabiashara na mwekezaji na nini naweza kujifunza kutoka kwake:

1. Mungu huwa anawekeza kwa vijana wadogo kabla hawajakomaa na kuwa na mawazo mgando.

Hapa namaanisha wale ambao bado hawajawa tayari. Anawapa yeye mwenyewe uzoefu anaoona utawasaidia kwenye kazi anayowaandaa kufanya. Mfano mmoja ni kwa Daudi. Samuel alipokwenda kwa nyumba ya Yese, aliwakataa kaka zake wooote akaenda kumchukua dogo ambaye hata nyumbani hakuwepo.

Mfano mwingine ni kwa Yusufu aliyepewa ndoto iliyowakasirisha kaka zake.

Kuna msemo unasema 'hauwezi kumfundisha mbwa mzee mbinu mpya'.

Nikiliongelea hili suala katika sura ya jamii zetu, wasomi wengi wanapoenda kuomba kazi wanaenda na fikra ya kwamba tayari wanajua kila kitu na wanakuwa na kiburi fulani hivi. Wanataka mishahara mikubwa wakati hawana hata uzoefu.

Mungu akiwa kama mwekezaji makini anatambua hilo tatizo lipo, badala yake anaenda kuchukua yule aliyedharaulika ndiyo anamuinua. Anajua huyo mtu atakuwa mnyenyekevu na msikivu.

Kuna sura mmoja ya Biblia nzuri sana inaoongelea hiko kitu nikiikumbuka nitaiweka.

2. Mungu anaanza na mtaji mdogo halafu anaukuza taratibu.

Hili linajielezea. Mungu anakuwa very specific nini anataka kutoka kwako vingine anakuletea yeye mwenyewe. Inaonyesha Mungu anaamini sana katika uzoefu lakini anataka uzoefu uupate kabla ya kazi. Hataki kukulipa wakati bado unajifunza! Kina Yusufu na Daudi ni mifano mizuri.

Mfano mwingine ni Musa. Musa alipodhani hana zana za kutosha kufanya kazi, Mungu hakwenda 'kukopa benki kumuongezea mtaji', alimuuliza ana nini? Musa alivyosema ana mti tu, Mungu akautumia mti huo huo kumaliza kazi.

3. Mungu anajua kutoa motisha kwa 'wafanyakazi wake'.

Mifano ipo mingi. Kuanzia Musa aliyemuuliza atafanyake kazi anayomtuma wakati yeye ana kigugumizi, Yeremia aliyesema atawezaje wakati yeye ni mtoto hadi Yesu aliyeomba kikombe kimuepuke hadi Mungu akawatuma Elia na Musa kumpa motisha. Inaonyesha Mungu akishawekeza kwako, akiona unasitasita hakutumbui, anakupa motisha kwamba unaweza, songa mbele.

Pale anapoona kweli huyu mfanyakazi wangu amefanya kila awezalo ila amekwama, anaingia mwenyewe mzigoni. Na ili kuonyesha bado anathamini mchango wako, bado atakuhusisha. Mfano wa hili ni Musa tena na mapigo yaliyowapata Wamisri.

4. Mungu akikupa kazi hatakuacha uifanye yote mwenyewe. Atakusaidia kuikamilisha.

Ili kuhakikisha kazi inaenda kwa ufanisi na uwekezaji wake unaenda sawa, Mungu atakupa kazi ya msingi uifanye wewe ila makorokocho mengine anakurahisishia kwa kuyafanya yeye mwenyewe ili ufocus kwenye jambo la msingi.

Hapa nitatolea mfano wa Nuhu. Mungu alipompa Nuhu kazi ya kujenga safina alimpa maelekezo ya wanyama na ndege na idadi yao wa kuingia nao. Lakini ukisoma kwa makini utagundua alichofanya Nuhu ni kujenga tu safina na kuwaingiza wanyama na ndege ndani pamoja na familia yake kama Mungu alivyoagiza ila hakuhitaji kwenda kuwatafuta hao wanyama na ndege. Mungu aliwaleta hao wanyama na ndege kwa Nuhu. Embu fikiria ingemchukua muda gani kama ingebidi aende kuwatafuta yeye mwenyewe. Kuna somo muhimu sana hapa. Bado natafakari hili neno na naandaa maandiko mengine.

5. Mungu anaweka lengo la faida. Likitimia anatumia sehemu ya faida kuanzisha biashara zingine nyingi, ile ya mwanzo inabaki kama biashara mama.

Kwa watu wanaojua mambo ya biashara kuna kitu wanaita Parent Company na Subsidiaries. Biashara mama ikishajijengea jina unatumia ile sifa iliyojijengea kufungua biashara zingine.

Mfano mzuri ni wa Yesu. Baada ya Yesu kumaliza kazi yake, amebaki kama 'kampuni mama' iliyomsaidia Mungu kusambaza Neno lake dunia nzima.

Hii concept nchi zilizoendelea wanaitumia sana ingawa kwa huku kwetu bado haijaingia sana. Mfano wa kampuni za namna hiyo ni Acacia vs. Barrick Gold. Kuna njia nyingine inatumika sana inayofanana na hii inaitwa Franchising ndiyo haya makampuni kama KFC na McDonald nadhani hata Pizza Hut.

Chukua ulichojifunza halafu weka katika biashara zako utaona matokeo.

ITAENDELEA....
Hakuna kitu kinaitwa mungu kimewahi kuwepo. Ni hadithi zilizotungwa na wajanja
 
Hakuna kitu kinaitwa mungu kimewahi kuwepo. Ni hadithi zilizotungwa na wajanja

Msituharibie uzi usije ukafungwa kwa sababu zenu. Kama hauamini si ukae kimya upite tu? Mbona hauendi kanisani na kupiga kelele zenu hizo?
 
Mkuu yeye kamuelezea kwa uelewa wake na si kosa. Ni kama kanisani kila mmoja hutoa sadaka kwa kadiri alivyojaliwa ndivyo hata katika uelewa na utoaji maoni. Yeye uelewa wake umeishia hapo. Biblia inasema "Usihukumu usije ukahukumiwa" Japo hujahukumu. Hivyo mtu akisema ajuavyo si kosa, kosa linabaki kwa mwenye uelewa kujifanya yeye ni bora kuliko mwingine. Kosa hilo hufanywa na waumini wengi wa dini
Nimekusoma mkuu, lakini mimi ninachopinga ni maelezo yake kuwa eti MUNGU huwa anawekeza kwa vijana wadogo tu. Hapo ndipo ninapopingana naye. Ukweli ni kwamba MUNGU anaweza kuwekeza kwa mtu yeyote yule kama apendavyo YEYE, iwe ni mtoto mdogo au mzee.
 
Back
Top Bottom