Mpondoshilla
Member
- Jul 4, 2022
- 36
- 132
Haimake Sense hata kidogoo! Maisha ya mwanadamu kila kinachotokea kina sababu na Mungu anajua sio kesho yako tu hata maisha yako yote hapa duniani mwanzo mpaka mwisho.Ina make sense.
Sasa kwanini aruhusu mi nizaliwe si angepotezea tu nisiwepo?Lengo ni hitimisho la maisha yako ya umilele, Mungu hana hasara hata ukipotea,maana ana viumbe wengine mamilioni kwenye sayari zingine wasio na dhambi, anakupa muongozo kwa faida yako Ili uishi vyema hapa duniani na kesho ahera.
Sasa kwanini huwa tunamuomba ili abadili maamuzi?Nionavyo binadamu uwa tunatenda na kupita mule mule kulikokwisha pangwa na kujulikana kwa muumba wetu milele na milele huko nyuma.
Haijalishi hayo tunayotenda ni mema au mabaya na tunayopitia ni mepesi au magumu maana yalishapangwa na kubwa zaidi kujulikana na Mungu mwenyewe na hivyo binadamu kutenda au kupitia njia tofauti na hiyo ni ngumu. Tukikataa hili basi tuwe tayari kusema Mungu hana uwezo wa kujua kila kitu.
Na hili la Mungu kutojua kila kitu sitaliamini milele.
ulimuona akisema?Anasema Allaah (Ta'aalaa):
وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ
Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghayb; hakuna azijuaye ila Yeye tu [Al-An’aam 6:59]
Na Anasema (Jalla Jalaaluhu):
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ
Sema: “Hakuna aliyoko katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. [An-Naml 27: 65]
Unaweza kulithibitisha?Mungu wetu anaijua leo kesho yako milele daima
Unachosema ni kwamba binadamu hana uchaguzi, hayupo huru zaidi ya kufuata kilichopangwa jambo ambalo si kweli.Nionavyo binadamu uwa tunatenda na kupita mule mule kulikokwisha pangwa na kujulikana kwa muumba wetu milele na milele huko nyuma.
Haijalishi hayo tunayotenda ni mema au mabaya na tunayopitia ni mepesi au magumu maana yalishapangwa na kubwa zaidi kujulikana na Mungu mwenyewe na hivyo binadamu kutenda au kupitia njia tofauti na hiyo ni ngumu. Tukikataa hili basi tuwe tayari kusema Mungu hana uwezo wa kujua kila kitu.
Na hili la Mungu kutojua kila kitu sitaliamini milele.
hoja dhaifu sana. Kesho ya Kila mtu huwa imepangwa na Mungu mwenyew tena Mungu humwazia mema kila mtu ila dhambi ndio hublock baraka bora za kesho ya mtu na kwakua ibilisi yuko against na mema Mungu anayowatakia watu wake. hutumia mlango wa dhambi kama kichocheo cha kublock baraka hizo kwakushawishi wanadamu kujiingiza huko. hakuna baya au zuri linalo mpata mtu kwa mpango wa mungu lile lisilo bora kwa huyo mtu. elewa sio kila jambo baya linalomtokea mtu Mungu anataka limpateNi ukweli ulio wazi ila ni ngumu kukubalika hasa kwa watu waliokaririshwa imani,
Iko hivi Mungu angekuwa anaijua kesho yako kusingekuwepo na kitu kinachoitwa dhambi, kwa sababu, mfano mtu amechinjwa hapo hakuna dhambi maana tayari mungu alishapanga utachinjwa au huo uovu unaoufanya sasa ungekuwa sio dhambi maana mungu alishapanga.
Njia unayoipitia ndiyo hatima ya maisha yako.
Kuna watu wanamtumikia Mungu mpaka wanazeeka na pia wapo wanamtumikia shetani mpaka wanazeeka.
Pia wapo walikuwa wanamtumikia Mungu ila hawajauona hata ujana
Maisha ni kama simu tu utachagua uitumieje vile unaitumia ndiyo inakupa majibu unayoyataka wewe
Kumbe kila kitu kimeshapangwa..🤣🤣Haimake Sense hata kidogoo...!! Maisha ya mwanadamu kila kinachotokea kina sababu na Mungu anajua sio kesho yako tu hata maisha yako yote hapa duniani mwanzo mpaka mwisho...
Yani hata usipoenda jua ndivyo ilivyopangwaaa 😀 😀 usidhani kwamba ukienda sijui kuna mpango utaubadilisha hapana ndo maana unaweza toka kanisani na still ukagongwa na gari ukafa... haubadilishi kitu ila hivyo ndivyo ilivyoandikwa juu ya maisha yako zaidi ukienda Kanisani unatengeneza maisha yako baada ya kifo.Kumbe kila kitu kimeshapangwa..🤣🤣
Basi haina haja ya kuhangaikia sijui kwenda church maana matokeo ni yale yale mwisho wa siku