Mungu angekwambia leo hii niombe utakacho, ungeomba nini?

obseva

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
573
646
Nimetafakari na nikatamani kukumbusha na wewe hasa wakati huu ambao maisha ni magumu kwa watu wengi na tunapita kwenye upepo unaohitaji matumizi makubwa ya akili na ufahamu. Kwa Kiasi kikubwa watu wamekuwa busy sana na inawezekana hata wanachokipata hakilingani sana na nguvu wanazo wekeza hivyo kujikuta ni wahanga wa kuwaza sana lakini matokeo ya mawazo yao hayaleti tija ya kutosha.

Kwa jinsi hiyo ni vigumu sana watu kuwa na utulivu wa kusikiliza sauti za watu wengine kwa makini, akiwa nyumbani, kanisani , kwenye mikutanao na nk, kwani mawazo yamechukuliwa na hali za kimaisha zinazoendelea mtaani. Jambo hili limeongeza ugumu wa kuelewa na kupata maarifa mapya kwa kuwa Imani huja kwa kusikia “Basi imani, chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwaneno la Kristo”( warumi 10.17)

Kwa kawaida mambo yanapokuwa magumu, unahitaji kusikia mawazo mapya ili uweze kusonga mbele, kwa maana nyingine mawazo uliyonayo katika wakati huu hayawezi kukuvusha kwenye mkwamo huu, lazima upate mbinu na njia mpya kuvuka kwa Sababu kila wakati kwa MUNGU unasababu zake za kuja, njia zake za kuishi na namna ya kupita ndani ya wakati huo. (Muhubiri 3.1 10) “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. 2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung'oa yaliyopandwa; 3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga; 4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza; 5 Wakati wa kutupa mawe, na wakati wa kukusanya mawe; Wakati wa kukumbatia, na wakati wa kutokumbatia; 6 Wakati wa kutafuta, na wakati wa kupoteza; Wakati wa kuweka, na wakati wa kutupa; 7 Wakati wa kurarua, na wakati wa kushona; Wakati wa kunyamaza, na wakati wa kunena; 8 Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani. 9 Je! Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo? 10 Nimeiona taabu ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.

Kwa mfano kama ni wakati wa Mungu wa kubomoa halafu wewe unajenga, bilashaka unafanya kazi ya kuchosha akili ambayo hakika ni ubatili mtupu kwa Sababu unachojenga kitabomolewa soon, fikiria ni wakati wa MUNGU Kupanda wewe unataka kuvuna, itakuwa ngumu sana kuweza kutokeza na ndiyo maana utajikuta unaangukia pua.

Ndiyo maana kwenye kawaida tu ya dunia, watu watakwambia huu ni wakati wa kufanya jambo Fulani na sio jambo lile, wachumi watakwambia huu ni wakati wa kununua hisa au ni wakati wa kuuza hisa, mambo haya ni mambo ya rohoni na yanahitaji utulivu Fulani kuweza kujua na kusikia mambo ya majira na nyakati. Mfano kwenye wakati huu Tanzania inaoupitia umejiuliza ni wakati wa namna gani na unatakiwa kufanya nini?, je umewaza MUNGU anatengeneza future ya aina gani kwa taifa na unatakiwa ukae wapi?. Ni jambo muhimu kujiuliza kwa unayefahamu mambo ya majira na nyakati, kwa Sababu bila kujua unaweza ukawa unapingana na nature (MUNGU) na ukajikuta unaharibikiwa kabisa na usisimame tena.

Luka 19:42 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Neno hili ni la msingi sana kila mabadiliko yana matokea yake, wapo watakaofaidika nayo, nawapo watakao umia, maranyingi malengo ya mambadiliko hufichwa ili wapumbavu waangamia, wenye utulivu wa moyo na hekima ndiyo huona na kuushinda mwelekeo wa upepo wa mambadiliko hayo.

2Nyakati 1:7-10 “Usiku huo Mungu akamtokea Sulemani na kumwambia: “Omba! Nikupe nini?” 8 Ndipo Sulemani akamwambia Mungu: “Wewe Ndiye uliyemwonyesha Daudi baba yangu fadhili kubwa zenye upendo na kunifanya niwe mfalme mahali pake. 9 Sasa, Ee Yehova Mungu, acha ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, kwa maana wewe mwenyewe umenifanya kuwa mfalme+ juu ya watu wengi sana kama chembe za mavumbi ya dunia. 10 Sasa unipe hekima na ujuzi+ ili nitoke mbele ya watu hawa na ili niingie ndani, kwa maana ni nani anayeweza kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?”

Ukisoma story hii juu kidogo, unakutana na Selemani unapewa ufalme hajui sana mambo ya uongozi na umewekwa katikati ya watu wenye akili na utajiri kuliko kuliko yeye.Hivyo kwake ni majira mapya ya maisha na anajaribu kutafuta nmna ya kumpendeza MUNGU ili aweze kuvuka, anaamua kutoa sadaka imusaidie kuvuka.

Baada ya sadaka MUNGU anamwelewa kuwa huyu jamaa mazingira ni magumu na anahitaji msaada, hii sadaka aliyotoa sio bure, na anaamua kumuuliza sadaka nimeiona omba lolote, Majibu ya Selemani yanatuonyesha alijua mazingira ya kazi yake, aliyaona mabadiliko yaliyokuwa mbele yake na pia alijua anahitaji nini iliaweze kupita hapo na ndiyo ulipoulizwa omba, aliomba kitu ambacho wengi wasingeomba. Yawezekana pia wewe katika kipindi hiki unahitaji zaidi hekima kuliko fedha, au nyumba kuliko gari, au mtaji kuliko nyumba, au elimu zaidi kuliko vyote na nadhalika na kadhalika kadili ya uhitaji wa mtu.

Swali kwako unajua mabadiliko unayopitia ndani ta nchii hii kwa wakati huu, unaoutulivu wa kusikiliza sauti ya MUNGU kama ungehitaji msaada wake?, akikujia leo hii usiku unahisi utamsikia kweli na huo ubussy wako? na kama ukabahatika kumsikia akakuuliza omba, utaomba nini sambamba na majibu ya mabadiliko unayoyaona maishani mwako? Lengo la swali ni utafakari usikivu wako na mahusiano yako na watu pamoja na MUNGU
 
Nmejaribu kuwaza majibu ya Hili swal Kat ya sie wa tandale kwa Tumbo na mbez beach
 
hahahaaa umenichekesha sana ndugu, mshindi anapimwa ndani ya mashindano, utashindaje kukiwa kweupe bila vikwazoo
JAMBO LOLOTE mkuu. Suleiman angeomba hili mapema hadi leo mambo yangekuwa safi, tatizo yeye akaomba hekima, akaishia kuwa na wanawake 1000
 
afungulie VIROBA aisee
Kwa mawazo yako unafikiri kweli MUNGU anaweza kufanya hivyo?, sawa akikufungulia kisha kesho ukanywa vikakupoteza unafaidakaje? na maisha yako ya baadaye?
 
Yaani kama mtu alikuwa ana uwezo wa kufungua ubongo wa mtu aliye concentrate na kusali ingekuwa ni kituko cha kufa mtu watu wengine huwa wanaomba maujinga matupu
 
Back
Top Bottom