Mungu anapofanya kitu kwako... Mi nimepata, kweli kupata ni Majaaliwa

Joined
Nov 2, 2023
Posts
88
Reaction score
264
Mungu anapofanya kitu kwako. NAwe wakumbuke wengine pia. Usiwe mbinafsi. Ukifanikiwa kupata usiwadharau waliokosa na kuamini kuwa wao ni wazembe.

Kupata ni Majariwa. Unamwona ng'ombe pamoja na ukubwa wake? Hana ndevu. Ila mbuzi anazo. Utashangaa kweli kupata ni majariwa ndugu yangu. Lakini na mkosaji wa leo usibweteke. Kesho ipo. Unamwona fundi selemara na msumeno wake akikata mbao?

Anasema kama si leo, kesho. Anapeleka mbele msumeno na kurudisha. Mwisho mbao inakatika. Hivyo wapendwa msichoke kusaidia wengine. Mimi leo nmepqta natakiwa kushare na wasiopata. Na msiopata endeleeni kupambana na kumshukuru Mungu. Huo uhai aliokupa ni kitu muhimu sana. Usisahau kuwa hauna ubia nao wala dhamana.

Kama si leo, Kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…