Mungu akitaka kukupa hakuandikii barua anakupa tu, wakati unapokufikia

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
805
810
BISSIROU DIOMAYE FAYE-RAIS KIJANA WA SENEGAL:
Ni mtu aliyevunja rekodi,kwa kugombea nafasi ya juu sana kwa mara yake ya kwanza, na akashinda kwa kishindo.Pia ni mtu ambaye wakati anagombea urais hakujua kabisa nahakujiandaa kugombea nafasi hiyo!Yaani Faye hajaota ndoto ya kuwa rais,lakini kawa rais!

Kabla hajashinda uchaguzi wa urais nchini Senegal siku ya jumapili ya tarehe 24/03/2024,ambayo ni siku 10 tu tangia aachiwe kutoka gerezani,Bwana Faye alijaribu tu kugombea nafasi ya Umeya katika mji wao mdogo wa Ndiaganiao.Alipoteza uchaguzi huo kwa mgombea wa chama tawala,mwaka 2022.

Wasenegali wachache sana wanajua safari ya huyu bwana mkubwa. Ana umri wa miaka 44 tu,alikuwa mkuu wa idara ya wakusanya kodi katika mji wa Dakar,ambaye alichoshwa na mfumo mbovu wa serikali,akaamua kuongoza vuguvugu la vijana wengi sana kupinga serikali yake.Ni mtu ambaye atakapoapishwa atakuwa ndiye rais mwenye umri mdogo zaidi kwa sasa barani Afrika. Alishinda uchaguzi kwa asilimia 54!Ushindi wa nguvu ya upepo wa kisulisuli.

Marafiki,jamaa na ndugu zake wa karibu huko kijijini kwao Ndiaganiao wanasema Faye ni mtu anayependa sana kujifunza mambo mapya,anapenda sana kusoma na kusikiliza muziki.Ni mtu mwaminifu,mdadisi na mwenye imani kali za kiislamu.Ni mtu anayeelewa sana matatizo ya nchini kwake na wananchi wake,sanasana mahitaji ya vijana.

Faye amekulia katika mazingira ambayo watu hupigania haki zao na za watu wengine,hii ilianzia kwa babu wake,ambaye alifungwa na Wafaransa kwa kupigania haki ya wanakijiji.Babu alikuwa chifu wa kabila lake,na alishiriki kwenye vita vya pili vya dunia.Kisha baba yake naye akawa chifu kwao.Yaani uongozi umemfata badala ya yeye kufata uongozi!

Lakini Faye amepata nafasi hii baada ya kuteseka nakusota jela.Alifungua jela kutokana na kupigania haki za rafiki na mshirika wake wa kisiasa.Alifungua mwezi April mwaka 2023,kwa kosa la kupinga serikali kutokana na posti zake kwenye mtandao wa facebook kuonekana ni hatari sana na ni tishio kwa amani ya nchi hiyo.Alipinga vikali hatua za serikali za kumfunga mshirika wake anayeitwa Ousmane Sonko,mwanasiasa maarufu sana wa upinzani nchini humo.Faye alisimama kidete kumtetea Sonko kwa namna ya kipekee.

Hatimaye uchaguzi ukatangazwa,lakini Sonko akakatazwa,au kupigwa marufuku kugombea uraisi baada ya kupatikana na kosa la kusingiziwa la kubaka,ambayo hata hivyo ilipunguzwa ikawa kosa la kushiriki ngono na mtoto….(mdogo).Kufuatia katazo hilo,Sonko alimtaja kama mgombea badala yake,kitu kilichompa sifa na umaarufu wa haraka sana Bw Faye nchini humo.Yaani alipata zali la kimentali(vijana wanasema)!

Wakati anamtangaza Faye kuwa mgombea kwa niaba yake,Faye alikuwa gerezani,kwenye gereza ndogo ambapo alikuwa amekaa miezi 10.Bw Faye alianza kampeni zake humo gerezani,kabla hajaachiwa.Wakati huo Sonko naye alikuwa ndani amefungwa!

Faye na mshirika wake Bw Sonko waliachiwa wiki mbili zilizopita,siku 10 tu kabla ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo,wakaanza kampeni za nguvu.Rais wa nchi kipindi hicho Bw Macky Sall alijaribu kuairisha uchaguzi huo bila mafanikio.Sonko amekuwa maarufu sana kwenye nchi mbalimbali za Afrika Magharibi,lakini watu wachache sana wanamjua au Bw Faye.Siku ya uchaguzi ulipofika,wengi,na sanasana vijana walisema na kutangaza waziwazi kwamba wanampigia kura Bw Sonko….yaani Faye.Ukweli ni kwamba Faye amedandia bahati na nyota yake Bwana Sonko.Kura alizopewa ni kura za Sonko.

Bw Faye anajulikana kama mtu asiyeongea sana,lakini wakati anatoka gerezani ndipo alipogundua kwamba yeye na Sonko wanapendwa sana na wasenegali.Aliongea maneno machache lakini yenye mashiko sana!

Kwa njia nyingi,Bw Faye ni mwanasiasa kijana anayefahamika sana sana kwenye Facebook,mara nyingi anaonekana akiwa na ‘earphone’ masikioni akisikiliza sana mziki.Ni mtu asiyependa kuvaa suti za nchi za mgaharibi,na badala yake anapenda mavazi ya kiafrika,na sanasana kanzu.Lakini ni mtu mwenye ushawishi sana kwa vijana wa Dakar.

Hadi wakati muda wake unaanza kumezwa na siasa,alikuwa mpenda soka,alikuwa mchezaji maarufu wa timu ya wakusanya kodi wa mjini Dakar.Faye pia ni shabiki maarufu wa timu ya Real Madrid wa Uispania.

Bassirou Diomaye Faye (inatamkwa BASS-ih-ru jo-Mai Fie)alikulia kwenye familia kubwa.Anapenda sana kusoma,na mwandishi wake anayempenda sana ni Dale Carnegie,mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho “Jinsi ya kupata marafiki na kushawishi watu”.Baba yake, Samba Ndiagne Faye anamtaja mwanae kama kijana ambaye uelewa wake umezidi umri wake wa miaka 44.

Bw Faye anawake wawili,kitu ambacho hafichi na anajivunia.Amepata watoto wanne na mke wake wa kwanza,alioa mke wa pili mapema mwaka 2023.Mke mdogo huyo anafanya kazi na kuishi nchini Ufaransa.Wawili hao walikutana mara moja tu baada ya harusi na kabla hajakamatwa na kufungwa jela.Walikutana tena kwa mara ya pili kwenye kipindi cha kampeni…

Faye na Sonko wanania ya kuleta mageuzi ya kisiasa,ikiwemo kuachana kabisa na nchi ya Ufaransa,na kutaka kubadilisha sarafu yao kutoka kwenye umiliki wa nchi ya Ufaransa.Wameonekana kama wanasiasa wanaoleta mageuzi na hewa mpya katika siasa za Senegali.

Kabla ya uchaguzi,Bw Faye alitaja mali zake zote,kitu ambacho ni kipya katika nchi hiyo.Anayo nyumba mjini Dakar na kiwanja kimoja tu.

Kwa sasa imekuwa jukumu la wasenegali kufanya utafiti kuhusu rais wao, kumjua vizuri kwa sababu hawamjui vizuri kihivyo.Faye ametokea katika familia masikini,familia ya kilimo na ufugaji mdogo…..Wasenegali wanaamini nchi hiyo inahitaji mtu kama Faye kwa sasa.Tusubiri tuone kitakachojiri nchini humo,lakini ukweli ni kwamba Afrika inabadilika kwa kasi sana.

Na ukweli mwingine ni kwamba haujui kesho yako.Mtegemee Mungu anayejua kesho yako!

#LifeCanChange
 
Mkuu mchawi wa kusini, Asante kwa Makala nzuri juu ya Rais Mteule wa Senegal.
Kupatikana kwake naamini kunatokana na mifumo ya haki ya upatikanaji viongozi nchini mwao....

Baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na Kati kwavile hatuna Mifumo ya haki ya Uchaguzi ndo maana alo shinda hatangazwi bali aloshindwa na hii iko siku linaweza ziingiza nchi zetu kwenye sintofahamu kubwa.
Acha tusubirie iko siku tutaona.

Much respect Mkuu KIGAGULA a.k.a mchawi wa kusini
 
Na Tanzania itakuwa hivi muda si mrefu. Mark my words! Tunataka Rais kijana, tunataka Rais anayesimamia haki na ambaye amechaguliwa kihalali. Hatutaki rais aliyeingia madarakani kwa wizi wa kura. Wizi wa kura ndio unawafanya watendaji wanakuwa mafisadi. Sababu wanakuwa wamesaidia kuiba kura na hivyo kiongozi anakuwa hana moral authority ya kukemea mafisadi. Sababu kiongozi anakuwa amechafuka
 
Ila Macky Sally alizingua sana alitaka kugeuza Senegal Mali yake hata picha yake ilianza kuchukiza imejaa tamaa na kibri
 
BISSIROU DIOMAYE FAYE-RAIS KIJANA WA SENEGAL:
Ni mtu aliyevunja rekodi,kwa kugombea nafasi ya juu sana kwa mara yake ya kwanza, na akashinda kwa kishindo.Pia ni mtu ambaye wakati anagombea urais hakujua kabisa nahakujiandaa kugombea nafasi hiyo!Yaani Faye hajaota ndoto ya kuwa rais,lakini kawa rais!
Ingekuwa kukomaa sana ndio kuwa Rais basi
-Magufuli asingekuwa Rais(japo alitaka kulazimisha awamu ya 2)
-Lowasa angekuwa Rais
-Dr.Slaa angekuwa Rais
-Samia asingekuwa Rais
-Felix Thisekedi asingekuwa Rais na Fayulu na Tajiri wa TP mazembe wangekuwa Marais
-Raila Odinga angekuwa Rais
-Abiy Ahmed asingekuwa Rais
-DB Faye asingekuwa Rais na Sonko angekuwa Rais

Kiufupi mifano ni Mingi sana.Utaoata unachostahili japo Kwa staili tofauti.

Rais pekee aliyekomaa na akabahatika kupata ni Hichilema wa Zambia.
 
Ingekuwa kukomaa sana ndio kuwa Rais basi
-Magufuli asingekuwa Rais(japo alitaka kulazimisha awamu ya 2)
-Lowasa angekuwa Rais
-Dr.Slaa angekuwa Rais
-Samia asingekuwa Rais
-Felix Thisekedi asingekuwa Rais na Fayulu na Tajiri wa TP mazembe wangekuwa Marais
-Raila Odinga angekuwa Rais
-Abiy Ahmed asingekuwa Rais
-DB Faye asingekuwa Rais na Sonko angekuwa Rais

Kiufupi mifano ni Mingi sana.Utaoata unachostahili japo Kwa staili tofauti.

Rais pekee aliyekomaa na akabahatika kupata ni Hichilema wa Zambia.
Wengi wanaiba kura kuwadhulumu wanaostahili. Tukatae hilo
 
Mungu hatoi kitu broh,biashara yake na yko iliishia alivyokupa akili,kila kitu ni juhudi yako,ingekuwa anatoa,angempa nuhu safina ya bure
 
Na Tanzania itakuwa hivi muda si mrefu. Mark my words! Tunataka Rais kijana, tunataka Rais anayesimamia haki na ambaye amechaguliwa kihalali. Hatutaki rais aliyeingia madarakani kwa wizi wa kura. Wizi wa kura ndio unawafanya watendaji wanakuwa mafisadi. Sababu wanakuwa wamesaidia kuiba kura na hivyo kiongozi anakuwa hana moral authority ya kukemea mafisadi. Sababu kiongozi anakuwa amechafuka
KANISA/ mwanamke ndiye atakayetuletea Rais wa kulivusha Taifa letu 2025 na kuendelea,

Tusubiri.
 
BISSIROU DIOMAYE FAYE-RAIS KIJANA WA SENEGAL:
Ni mtu aliyevunja rekodi,kwa kugombea nafasi ya juu sana kwa mara yake ya kwanza, na akashinda kwa kishindo.Pia ni mtu ambaye wakati anagombea urais hakujua kabisa nahakujiandaa kugombea nafasi hiyo!Yaani Faye hajaota ndoto ya kuwa rais,lakini kawa rais!
Ahsante sana kwa uchambuzi mzuri.
 
Back
Top Bottom