Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Mume wa Malkia Elizabeth, Phillip ameamua kupumzika na kuacha majukumu yake ya kiufalme.
Kwa mujibu wa jumba la kifalme ya Buckingham, uamuzi huo ulichukuliwa na Mfalme Phillip mwenyewe na unaungwa mkono na malkia Elizabeth kulingana na msemaji wa kasri hilo.
Philip ambaye anatarajia kufikisha umri wa miaka 96 mwezi ujao, atafanya kazi za kifalme kati ya sasa hadi mwezi Agosti lakini hatakubali mwaliko wowote.
Malkia Elizabeth ataendelea na majukumu yake yote ya kifalme katika kasri hiyo limesema.
Mwanamfalme huyo alifanya kazi siku 110 mwaka 2016 na hivyo basi kumfanya kuwa mwanachama wa tano wa familia hiyo ya kifalme aliyekuwa na kazi nyingi.
''Ni kiongozi ,rais na mwanachama wa zaidi ya mashirika 780 na ataendelea kuhusishwa na mashirika hayo lakini hatochukua majukumu yenye kazi nyingi kwa kuhudhuria hafla zao'', alisema Msemaji wa jumba la Buckingham.
Katika taarifa msemaji huyo amesema kuwa ufalme huo utaendelea