Mume wangu kantongoza

Du! hii ni kali, yaani hata sauti ya mumeo ulishindwa kuigundua na kujua kuwa anakutega!!! lazima wewe utakuwa kicheche. Mwombe samahani yaishe...maisha yaendelee. kwa kuwa zimeshapita siku kadhaa lolote utakalosema itakuwa unatwanga maji kwenye kinu tu, jamaa alishakupata. Wewe omba msamaa tu. Vinginevyo mgeuzie kibao mwambie "Mume wangu niliposikia sauti kama ya mume wangu kwenye simu wakati namba siijui nikatakanijue kama kweli ulikuwa ulikuwa serious (una-date na mwanamke mwingine) au ulikuwa unanitega tu. Sasa niambie ukweli lipi sahihi kati ya hayo mawili?". Akijibu nilikuwa natakakujua kama kweli mwaminifu au unagawa kwa wengine, mwambie "sidanganyiki". Akisema nimekugundua kuwa wewe sio mwaminifu, mwambie "mimi ndio nimegundua kuwa wewe sio mwaminifu. Kama ni mwaminifu kwanini uwe na simu ambayo mimi mkeo siijui?". Hapo ndio inakuwa ule mchezo wa "mwaga mboga mimi nimwage ugali" na kama mumeo hana busara na ndoa pengine ndio itaishia hapo
 
Eeh! We kaka/dada ukicheche wangu ni upi hapo jamani? Mie nlitamani tu kumjua huyo anaenitongoza kwa kudai kuwa mie ni mpenz wake. Na mind you huyu mtu alionekana kunifahamu vizuri. Sasa sijui kwa nini umenihukumu hivyo
ukicheche wako ni pale ulipopanga kwenda kuonana na huyo jamaa bila kumshirikisha huyo mumeo. kama kweli ulikuwa una haja tu ya kuonana na huyo anayekusumbua si ungemwambia mumeo? na je ungekuta siyo mumeo ungefanyaje? swali litakuwa rahisi kama hujampenda, lakini je ungempenda?
Let me tell you, kama kweli hukuwa na mpenzi wakati mumeo hayupo nchini usingepanga kuonana na mtu ambaye eti anajidai ni mpenzi wako na anajua kuwa mumeo karudi ndo hutaki kuonana naye. hii inaonyesha dhahiri kuwa ulikuwa na huyo mpenzi, ambacho hukuwa na uhakika tu ni hiyo namba yake ya simu.
 
Mwambie mumeo aache umamiloo. Mkumbushe kuwa mtu mmoja hawezi kulinda bahari.
 
Wewe mwanamke ni miongoni mwa mambumbumbu wa chache kuwahi kutokea
 
Wewe maharage ya njano...umekamatika unajaribu kubadilisha stori..mume wako alipoenda nje wewe ulikuwa unadanga.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…