Mume wangu hataki kunipa chakula cha ndoa

Kaa nae chini hongea nae maana maisha ya sasa hatari, unaweza kukuta anadaiwa hajarejesha hata mikopo wewe kaa nae chini hongea nae, sio bure anamatatizo na wala usimfikirie vibaya.
 
Labda humpeti peti kama zamani, labda roho inamuuma kuona mapenzi yamehamia kwa mtoto. Mjali yeye, pendeza kwa ajili yake. jipambe, chumba kinukie, mpikie chakula kizuri, kula nae...punguza mahaba kwa mtoto, mpe muda mumeo. yeye alikuwepo kabla ya mtoto na atakuwepo siku zote hata pale mtoto atapokuwa hayupo...( kumbuka atakua. ataenda shule, ataanza kazi) ila hubby atakuwepo siku zote.....Pia usisahau Sala.
 

nenda naye taratibu, inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, usimbake. iko siku utajifunza kitu dhidi ya uchovu wake
 
Kama uko dar ni pm. Tusaidiane, si wajua msaada kwenye tuta
 
Bi mdogo;
Kuna mambo mawili matatu naweza kukusaidia kutokana na maelezo yako.
Moja;
Hivi, biashara yenu imechanua zaidi? Je, Hapo anapofanyia hiyo biashara kuna mazingira yanayo mfanya atumie akili na nguvu nyingi za mwili? Hayo humchosha mtu saana na anapokuja nyumbani anajikuta bado anawaza ya shughuli.
Pili;
Una mtoto mchanga, kumbuka ana hitaji saana usafi. Ni jambo ambalo ni jipya kwako. Una usafi? Mtoto awe msafi, weye uwe msafi, kitanda kiwe kisafi?? Utashangaa, chumba kinajaa nepi chafu au pampas zilizotumila au hata ambazo hazijatumika zinazagaa kila kona ya nyumba.
Mumeo, hili ni jipya kwake.
Tatu;
Sijui weye ni kabila gani, lakini kuna makabila wanapenda kuwatunza wake zao kwenye kipindi hiki cha uzazi. Unaweza ulibugia uji zaidi ukanenepeana, harufu ile ya maziwa yanayovuja etc. Je, upo sawa hapo? Chunga hayo na ujiweke fit. Usijiachie ukajikuta umechepuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…