Dada uliyepata na mkasa huu pole sana, naamini wapo wengi wenye mikasa kama hiii ndani ya ndoa.
Ushauri, naomba tutoe ushauri endelevu kwa wanandoa iwe kwa mwanamke au mwanaume, kwani minyanyaso ipo pande zote.
Ushauri wangu kwa huyu dada, kwanza akaonane na vyama vinavyotetea haki, kama Tamwa, Tawla nk wao watamshauri namna ya kufanya kisheria, kuhusu ndoa yake na haki zake zote ndani ya hiyo ndoa.
Pili awasiliane na waliowafungisha ndoa endapo imefungwa kidini. Wazazi wa kiroho wana nafasi na wanaweza kuwashauri wanandoa hawa juu ya mstakabali wa ndoa yao.
Naona hakuna haja ya kushirikisha wazazi, kwani hawatakuwa na la kufanya, wazazi wa mwanaume hawataamini kinachosemwa na mwanamke na wazazi wa mwanamke, watakirihika na damu kuchemka kiasi cha kutaka talaka itolewe papo papo waondoke na binti yao kwani mzazi yeyote hawezi kuvumilia huo uibilisi.
Ninapenda wana JF tusaidiie kutoa njia ya kuzuia mambo yasiyokubalika kama haya, hawa wanaotendewa haya ni dada zetu, watoto wetu, shangazi zetu nk.
Natoa wito katika JF, tufikirie namna ya kuanzisha thread endelevu kushauri kuhusu masuala ya ndoa na haki za wanandoa.
Ni dhahiri huyu dada hajui haki zake na ana hofu ya kuogopa kueleweka vibaya na jamii endapo akitoka katika ndoa yake, kwani watu wanapenda kujua umetoka katika ndoa kwa sababu ipi? Sasa tunaelewa sababu ni nyingi, nyingine ni udhalilishaji, unyama wanaofanyia akina dada kama huu!!!
Akina dada hawana haja ya kukaa katika ndoa, ambayo tayari mwenzi ameshavunja misingi ya ndoa.
Katika uelewa wangu mdogo wa sheria, nakumbuka kusoma mahali fulani, kile kitendo cha mwanandoa ( mwanaume ) kudai tendo la ndoa kwa njia ya kinyume cha maumbile na kumwingilia kinyume na maumbile, ni kwamba mwanaume amevunja ndoa tayari.
Kuepuka majanga kama ya huyu dada, wanandoa tunahitaji kumuendea ( MUNGU) yeye aliyeanzisha taasisi ya ndoa, na kuomba kupata msaada wake wa jinsi ya kupata mwenza sahihi wa ndoa.
Watu wengi na hasa wadada wanaingia katika ndoa kwa sababu potofu, kama utajili au nguvu za kiuchumi za mwenzi wa ndoa na bila kuweka vipimio sahihi katika msingi halisi wa ndoa. Angalia kama unayefunga ndoa naye ana hofu ya kweli ya Mungu! Kwani anayempenda na kumwogopa Mungu, atampenda kiumbe wa Mungu ambaye ndiye mke au mume wako.
Mungu awabariki wana ndoa na watu wanaofikiria kuingia kwenye ndoa, ndoa ni raha kabisa kwani yupo anayefanana na wewe, tusivunjwe moyo wa mafisadi wachache wa ndoa, ambao wao ni ufisadi kila eneo.