famicho
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 2,191
- 2,852
Habarini wapendwa wana JF,
Naandika uzi huu nikiwa na STRESS NYINGI SANA.
Katika pitapita zangu za kujitaftia ridhiki, nilikutana na huyu mdada ambaye baadae tuka-fall in malavidavi. Katika kutambulishana aliniambia kwamba hana mume, hivyo nisiwe na wasiwasi wowote.
Baada ya kucheki afya na kujiridhisha, ndipo mchezo ukaanza rasmi, mwezi mmoja baadae aliniambia anajisikia utofauti mwilini mwake, tuliamua kwenda hospitali kupima na aligundulika ana ujauzito(furaha ilitawala). Na mpaka naandika uzi huu ujauzito una miezi 2.
Kizaa zaa,
Juzi amenipigia simu na kunieleza kuwa mumewe(nilishangaa sana, ila aliniambia alinificha kwani mumewe alikuwa nje ya nchi na kwa muda mrefu) amerudi na amefurahi kumkuta yeye(mkewe) akiwa mjamzito kwa maana katika ndoa yao wana miaka 13 na hawajawahi bahatika kupata mtoto wala ujauzito kutungwa, hivyo jamaa amekubali kuhudumia tena bila kinyongo kwani kitanda hakizai haramu.
Katika maongezi akanieleza kwamba mumewe anataka anione ili anipongeze na kunishukuru kwa kufuta aibu, na ameenda mbali zaidi kwa kusema "nisiwe na wasiwasi"(haya maneno nashindwa kuyaelewa anamaanisha nini)
Lengo la kuuleta uzi huu hapa, ni kuomba ushauri wa je, niende kuonana na huyo mumewe au nisiende!?
NAWASILISHA KWENU WANAJF KWA USHAURI.
Mbarikiwe!!