Mwanaume wa kiislam mwenye umri kuanzia miaka 30 na kuendelea, anaejua dini na maana ya Uislam, mwenye kufuata misingi ya dini ya kiislam anahitajika hapa, nina miaka 28 ila sina mume kwani sijapata kila anaenifata hana sifa tajwa hapo juu .
mpz ukishapata yule second best naomba unipe mana natafuta vigezo sawa sawa
Kwani shehe wako amesema hakutaki. Mwambie huyo atakufaa zaidi. Au nenda pale msikiti wa Kwamtoro baada ya swala ya ijumaa, halafu sema watafuta mume. Hapo utapata hata zaidi ya mia.
Mpigie simu Mrisho Ng**sa
Ni wachache sana wanaume waislam mwenye kufuata misingi ya dini haswa kukaa mpaka miaka 30 hawajaoa, kwani kuoa mapema ni sunnaa..mtu mwenye miaka zaid ya 30 then hajaoa kuna uwezekano anazini, sasa kama anazini(kufanya mapenz bila ndoa) hapo kuna misingi ya dini dada yangu..hvo bado utakuwa na kazi ngumu kumpata huyo mwanaume labda uwe mke mwenza. Punguza vigezo watu wakamate fursa.
As'salaam Alayk.. Weka cv yako ili muoaji amjue anayekutana nae..
Hawezi kuweka cv yake hadharani especially kama ni dada wa kiislamu mwenye maadaili. kama kuna alie interested amfuate pm wakapeane cv huko
Ukifika huko pm atakuambia huna sifa vile vile bora aweke cv yake hadharani nae tumpime maadili