Mume ni mtamu asikwambie mtu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,792
Habari za jioni wakuu,

Basi kule kibaruani nilitokea kupata swahiba ni mkaka umri wetu ni karibia sawa, kaka huyu ameoa na amebahatika kupata watoto wanne na mke wake. Kaka huyu tunaongea mengi, nikipata hata mitihani kibaruani nitampigia simu tunaongea ananifariji basi siku inapita. Kaka yangu huyu wa hiari alinitambulisha kwa mkewe, ikiwa siku kukiwa na ki sherehe nitakwenda birthday za watoto na vitu kama vile.

Ilitokea wakati flani walikuwa na mtafaruku mkubwa sana na mke wake, kwakweli yule kaka yakimzonga alinipigia simu na tukafarijiana, ule mtafarufu ulikuwa mkubwa kiasi cha wazazi wa pande zote mbili kuitwa, basi kwenye kikao wakaambiwa kila mtu aweke manyanga yake mezani yachambuliwe, lisiachwe jani la tatizo, kikao kimekuja kufagia, kwani kikiisha famila zote zinataka kuona wanalea watoto wao.

Mke wa swahiba si aseme kwenye kikao, kuna mwanamke anaitwa Sky Éclat, kila siku wanaongea kwenye simu, muulizeni uhusiano wao. Swahiba anakuja kunisimulia kesho yake kazini ananiambia lilimfika hata mwenyewe hakulitegemea.

Jamani mume mtamu, nimekoma kuwa na uswahiba na waume za watu.
 
Urafiki wenu kama una mipaka "no jigijigi" sioni shida la muhimu kwa sasa punguzeni ukaribu.

Lakini shoga swali

1; wewe umeolewa?
2; una mchumba?

If no 1 and 2 yes achana na huyu swahiba ingawa inauma kwa rafiki ulomzoea.
 
Back
Top Bottom