Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Pole sana shost, samahani lakini kwani huyo mumeo dini gani na huyo mwanamke kazaa nae tuu au kamuoa? isitoshe usitoke kwenye ndoa yako ukampisha yeye banana nae mpaka kieleweke,najua kama sio rahisi unahisi kama kuchanganyikiwa lakini jikaze wewe mwanamke na usikubali mwanamke mwenzio akakuzidi kete,kama mume mumeo wewe na unajua nini anapenda zaidi analadha gani na wapi mtamu funga mbeleko umrudishe mumeo nyumbani mlee watoto wenu na kumbuka hakuna ndoa
isiyo kua na misukosuko inshallah mwenyezi mungu atakupa moyo wa subra na ushindi.
pole sana shosti,umegunduaje kakwambia au?
Ila anaweza kuwa amebambikiwa pia........msisitize akafanye DNA test
Mh,endeleeni kuchangia kwanza,maana na miye nina soo langu kidogo linafanana na hili,labda naweza nikapata majibu kwenye hii thread ila nikikosa ntaiachia ili mnipe mawazo,pole sana mama.
Kazi kweli! Kama unadhani unahitaji mtoto wa 3 na wewe mchakachulie. Formula ni kuwa mna open marriage, na wewe uta-apologise tu yeshe. (Tahadhari, uwe tayari kuachwa. Kama ni tegemezi sana chakachua kwa siri)
Inauma, huyo si mwaminifu kaa mzungumze hayo matatizo kama bado ana mahusiano na mama wa huyo mtoto ama sivyo, usiondoke kwa kuwa una watoto wadogo. Ikiwa ataamua kukuletea huyo mtoto umlee, sikushauri hata kidogo.
kumbuka kuwa yawezekana unamtimizia yote mumeo,halafu bado kaenda nje,niamini maneno yangu,mwanaume kwenda nje si kwamba umridhishi,ni hulka tu!ila wewe usimnunie hata kidogo ongeze mapenzi zaidi na zaidi,pia muombe sana mungu wako,atakusimamia.
hii ni defence nzur sana kwa huyu jamaa-jamaa alikuwa anajaribu kama anaweza kufyatua watoto wa kiume, naona wee umeletea wana wa kike tu. Ila sijui bhana.