Mume/Mke kumuibia mwenzake kwenye ATM

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
8,950
2,000
Wanajamvi,

Kuna haka katabia nimekutana nako mara nyingi kwenye mazingira yangu ya kazi ambapo mtu anakuja akiwa mkali sana kwamba haoni pesa zake kwenye akaunti zimepungua,ukimuhoji kama anashare na mtu password anakuja juu kwamba hakuna mtu alishampa password na lazima arejeshewe pesa zake vinginevyo anamwita mwanasheria wake.

Kiungwana tunamshauri akaulize vizuri kama nyumbani kuna mtu anaijua password yake na kachukua pesa kwenye ATM lakini mtu anarudi kesho yake / au anagoma kwamba hakuna mtu anaijua.Hatua ya mwisho ni kumuonesha picha za mtu aloingia na kadi yake na kuchkua pesa.

Hapo ndio panakua patamu.., unamuuliza vipi hii sura unaifahamu? Mtu anakua mpole kwanza halafu utaskia ngoja nipige simu... halafu anasema ukweli huyu ni mme/mke wangu.. hapo kesi yetu inakua imeisha.

Sasa hii inakuwaje jamani mtu anamuibia mwenzake na anakataa kabisa kwamba si yeye hadi akioneshwa picha ndio anakubali?

Majanga haya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom