Mume Kikojozi

Wa Nyumbani

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
438
65
Siku moja tu baada ya harusi yao, mke akagundua kuwa mume wake ni kikojozi. Akamvumilia mpaka wakamaliza wiki moja. Siku moja mke akamwambia.
"Mume wangu, majirani wanaona kila siku tunaanika godoro nje na hatuna mtoto anayelikojolea. Unajua wanajiuliza sana?"
"Ni kweli" alijibu mume kwa unyonge.
"Nashauri twende kwa mganga wa kienyeji, namfahamu mtaalamu mzuri wa magonjwa mengi, utaacha kukojoa" akasema mke.

Wakakubaliana na kwenda kwa mganga. Huko mganga akawaambia hakuna tabu, ameshajua chanzo cha tatizo hilo.
"Hilo ni jinamizi, ukilala lilakuja na kukutisha, ndio unakojoa kitandani. Sasa nunua kisu kipya, weka mchagoni wakati unapolala, ukiliona jinamizi tu, lichome kisu , na tatizo lako litaishia hapo!"
Wakarudi nyumbani wakiwa na kisu kipya walichonunua dukani. Usiku ulipofika, wakiwa wamelala, mara mume akaliona jinamizi linamsogelea, akachukua kisu na kulifuata, likaanza kukimbia, maana lilijua akilichoma tu jamaa ataacha kukojoa. Jamaa akalikimbiza jinamizi, likatoka chumbani, likaenda sebuleni, likapitia jikoni jamaa analo tu. Kisha baada ya kuona hatari, likatoka nje na kuingia kwenye shimo la choo. Kuona hivyo, jamaa akashindwa kulichoma kisu. Kwa hasira akaweka mawe juu ya choo ili lisitoke tena halafu akanya juu ya mawe hayo. Alipomaliza tu kunya, AKAAMKA TOKA USINGIZINI! akakuta kumbe amekunya kitandani!. Mke kuona hivyo, akasema sasa balaa, jamaa kaacha kukojoa sasa ameanza kunya kitandani!! ha ha haaa!
 
Hahahaha duh Balaa kubwa sasa sijui ataomba talaka au watarudi tena kwa mganga!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom