Mume bora ni yupi?

Mume bora ni yupi?

bibliatimes

Member
Joined
May 13, 2025
Posts
7
Reaction score
9
Leo nataka niwasaidie wadada kwenye mahusiano.

Na ukinielewa leo hauwezi ukaingia kwenye hizi kesi ambazo zimetesa wanawake wengi, wadada wengi sana. Unaingia kwenye mahusiano na mwanaume anakupa mimba anakuacha. Nataka niwaambie wanaume wanaofanya hivi wanakosea sana na ni uovu mbele za Mungu. Na Wako wengi sana. Hizi taarifa napokea karibu kila siku. Haya malalamiko napokea karibu kila siku. Sasa nataka nikufundishe wewe dada utajuaje huyu mwanaume kwamba ni muhuni? Njia rahisi ya kujua kwamba huyu mwanaume ni muhuni ni very easy. Mwanaume akishakutafuta kaomba namba kafanya chochote pengine ukawa umempa ile namba. Okay. Baada ya hapo kuwa makini. Kinachofuata ni nini?

Kama kipaumbele chake itakuwa ni mapenzi, haitaji kuelewa zaidi kuhusu familia yako na nini. Hata kama atataka kuelewa familia yako, lakini siku ambayo atakuambia nahitaji kulala na wewe, kuwa makini sana. Yes. Kuwa makini.

Ngoja nikuambie mwanadamu yeyote nisikilize mpaka mwisho dadangu sawa eh mwanadamu yoyote hawezi akaja kwenye maisha yako kama hajaletwa na aidha Mungu au shetan maana yake, huyo mwanaume ambaye umekutana naye hujakutana naye bahati mbaya ni aidha Mungu amemleta au shetani. Sasa mwanaume aliyeletwa na shetani utamjuaje?


Na aliyeletwa na Mungu utamjuaje? Ni very easy. Mwanaume yeyote ambaye atakuja akademandi kuanguka kwenye dhambi na wewe ili adhibitishe unampenda au ili aone unampenda. Huo sio udhibitisho wa kimungu. Huo ni udhibitisho wa shetani.

Maana yake kile kitu kinadhibitisha kwamba huyu mtu hajaletwa na Mungu. Mi nakuambia haijalishi. ngoja nikuambie kama kaletwa na Mungu hataondoka hata kama utamwambia hicho kitu siwezi kufanya hawezi kuondoka na wala hawezi akaacha kujibu messej kuna wengine ukishawaambia tu hivyo anaacha kuwa anajibu meseji anaanza kukupotezea mim nakuambia huyu ana mwingine alikuwa alikutamani sio kwamba alikupenda alikutamani alikuwa na miemk hisia tu umenielewa kakuona tu hivi kwa nje kakupenda enda kakutamani sio upendo wa kimungu sijui umenielewa mpaka hapo hiki kitu ninachokuambia kitakusaidia kwa sababu gani kama kaletwa na Mungu, Mungu atahakikisha anabaki. eh Mungu hataruhusu aondoke. Haijalishi umemkatalia hilo jambo. Wengi wanataka uanguke nao uzini nao. Mfanye mapenzi na wadada wengi ndio hapa wamekufa. Wewe mwenyewe mdada anakuja jamaa badala ya kuwa very serious uko busy na wewe unamwangalia mwonekano ushadat. Akili yote imeyeyuka na wengine ni mawakala anakuja na vitu huna Yesu kuomba hautaki kufunga mara ya mwisho hujui ni lini neno la Mungu hausomi
akija zile nguvu za giza zinakuvuta umpende wengine wamejichanganya wakaona magari wakaona hapa ni penyewe alafu baada ya muda wakapotea wakaingia shimoni na wengine hadi vizazi vyao vimetolewa sadaka kwenye kwenye madhabahu za giza kuzimu kwa sababu ya kuingia kwenye mahusiano ya watu wasio sahihi.


Mtu yeyote atakayekuja akatanguliza ngono maana we au wewe baada ya kumkataa akawa mkali akawa hana muda na wewe. Alikuwa anajifanya kukusaidia saidia alafu baada ya hapo hakusaidii.

Tayari fahamu kabisa huyu kuna shida mahali. Yeyote ambaye kaletwa na Mungu hatatanguliza uovu kwa sababu Mungu na dhambi ni maadui. Umenielewa? Eh maana yake nini? Matokeo ya wadada wengi Roho Mtakatifu ndio ananiambia sasa hivi. Matokeo ya wadada wengi ambao wana watoto na hawajaolewa. Ni matokeo ya kutoelewa hii siri. kutomjua Mungu ni Mungu wa aina gani. Mungu hawezi kutumia uovu kukuingiza kwenye mahusiano. Eti kwamba kama unanipenda tulale kwanza. Mungu hawezi kuprove. Huyo ni sauti ya shetani inazungumza pale.

Mungu hawezi kusema hivo tayari. Lazima ujue kaingiliwa tayari na shetani. Yaani very hii dunia ukishajua sauti ya Mungu ni hii na ya shetani ni hii. Huwezi ukasumbuka. Watu wengi wanaishi maisha fulani ambayo ni ya majuto. Majira yao yameliwa kwa sababu walishindwa kutofautisha sauti ya Mungu na ya shetani. Na utaijuaje? Lazima uwe na neno la Mungu. Lazima uwe na Roho Mtakatifu.


Apart from kusikia sauti ya Roho Mtakatifu. Neno la Mungu basi soma ulielewe tu litafsiri. Kwa sababu kuna namna unaweza ukadesn ukapambanua huyu mtu ni sahihi au sio sahihi kwa ufahamu wa rohoni. Yaani ufahamu ulion nao tu kwenye neno la Mungu. Kwenye maarifa kama haya unayofundishwa. Wadada wengi wamejikuta kwenye wanaume ambao ni mawakala wa kuzimu. Wanaume ambao wameletwa na shetani kwenye maisha yao. Na wengine ni kwamba kabisa walikuwa hawataki.

Lakini jamaa alivyokuja tu ana gari ana funguo ya BMW nini rench wakaingia tamaa zao. Unapigwa mimba watoto watatu unaachwa alafu unakuja kusikia baadaye ana mke na ana watoto sita. Baada ya mtu unasikia ana mke tena mwingine mimi naongea true story wala sitengenezi. True story kabisa. Na kama unajipenda dadangu naongea na wanawake leo hii kitu utaiweka. Kitu cha kwanza ukitaka kuishi kwenye kusudi la Mungu ni kukaa mbali na dhambi. Wewe mwenyewe lazima uichukie dhambi ili akija anataka dhambi usifanye naye dhambi. Kama wewe mwenyewe umeikumbatia dhambi ukishamuona utaangalia mwonekano wake tu na wewe hisia zinainuka unaanguka dhambini baadaye unabeba mimba mnachati vizuri sana.


Siku utamwambia tu na mimba ndio siku hiyo anakuwa mkali. kaitoe kaitoe kaitoe kaitoe mwanaume yeyote anayekuambia kaitoe kaitoe hayuko tayari na wewe sasa cha ajabu unaenda kutoa alafu unarudi unaendelea naye hiyo dhambi sawa Mungu atakusamehe lakini unarudi vipi kwa mtu ambaye alitamka sauti yaani ndani yake ilitoka sauti ya shetani unarudi kufanya nini unataka kufa akumalizie mwanaume amekuambia toa mimba kama hakuwa tayari kuwa na mahusiano na wewe kwa nini alilala na wewe Si tumeelewana mpaka hapo? Kama hakuwa sawa kwa nini si angetulia?

I'm telling you mim nawaambia wadada wengi hiki kitu mkikielewa kitawasaidia. Sasa hivi kuna wasingo mama kibao mtaani. Kila mwanamke ana mtoto na baba mtu hamjui yuko wapi. Wamejaa mtaani. Wamejaa kwa sababu gani? Wamekosa maarifa ya kiroho

Hatuwezi tukawalaumu lakini lazima tuwafundishe ili wajifunze. Hata wewe unayenisikia fundisha mtoto wako. Fundisha watu wajue ili kuna mwingine uko hapo unatafuta mwanaume wa kukuoa. Kuwa makini. Hii ndio kriteria namba moja. Kriteria namba moja ni hii. Eh mtu yeyote asiye na hofu ya Mungu sio mume. Menielewa? Eh. Ngoja nikuambie

kwenye Ukristo lazima ujue bwana harusi ni Yesu mwenyewe. Anakuja baba, anakuja mama. In short ni hivi baba ambaye hayuko mwaminifu kwa bwana harusi wake ambaye ni Yesu Kristo hawezi kuwa mwaminifu kwa mke wake. Anaanza Yesu kule juu ambaye ni mume wa wote huku chini.


Huyu Yesu ni kichwa cha kanisa. Alafu anakuja mwanaume kichwa cha familia. anakuja mama na watoto huyu mwanaume kama ameshindwa kumtii Yesu kama bwana kama bwana harusi wake umenielewa eh usitegemee yuko tayari kuwa na [Muziki] mwanamke. Umenielewa?


Kwa sababu ili wewe mwanamke aishi na wewe vizuri lazima awe mtii kwa Kristo ili huyu Kristo akisema hivi afanye hivi. Kama hana wa kumsikiliza, hana wa kumuogopa, anaishi tu duniani humu anazurula. hana hofu ya Mungu. Hamuogopi Mungu anafanya tu mambo anavyojisikia. Huyo jamaa atakupa mimba na atakuacha. Lakini kama ana hofu ya Mungu Mungu atamkumbusha. Roho Mtakatifu atamwambia kwa nini unamjaza mimba mtoto wa watu unamwacha? No way out. Kuna wengine mnaenda kwenye hizo dini. Jamaa hawamwamini hata Yesu kama yupo.

Wanakuambia ni mwizi alafu na wewe unaenda kuungana naye. Nimempenda. Nimempenda.

I'm telling you we ambaye bado hujapitia hayo auo ambao wameshapitia wamepitia of course wanaweza wakarejea Mungu akarudisha majira waliopoteza lakini wewe ambaye sasa hivi ndio upo kwenye mahusiano na hao watu hao hao watu wenye ndevu nyingi mi nakuambia those guys are worshipping other gods I'm very sure ninakuambia ninachokuambia endelea kama hautapata hata nguvu ya kutoka. Mwambie Mungu nisaidie nitoke m mi nafanya huduma nina roho mtakatifu ndani yangu ananifundisha nikikuambia kitu elewa sio mambo ya kuwatenga wala nini lakini elewa tu those people are not people unaowafikiria walivyo.

Haijalishi ni mzuri kiasi gani ana tabia nzuri, anakupenda, anafanya hivi, anafanya hivi, mwisho wa siku utakuja kulia. Eh utakuja ulie. So I'm telling you nimeamua kusema hiki kitu wadada wanisikilize vizuri.

Ukinisikiliza hapa vizuri utashauri hata mtoto wako, utashauri hata jirani yako, mdogo wako, utamshauri dada yako ambaye yuko busy anawaza kuolewa, kuolewa, kuolewa na anajiuliza nitajuaje mume saa hii? Nitajuaje mume saa hii? Of course roho mtakatifu anatakiwa akusaidie.

Lakini kuna neno la Mungu ambalo moja kwa moja linadefine. Bibilia imeweka wazi. Kwenye Isaya 59:1-2 tunaona Mungu hasikiaji yaani whenever kuna dhambi ni ukuta mbele za Mungu. Kama kuna dhambi kuna ukuta mbele za Mungu. Maana yake nini? Mungu hata siku moja hawezi akaleta mtu kwako yule mtu atumie kigezo cha dhambi eti kwamba kuonyesha wewe unampenda. Haiwezekani.

Haiwezekani. Haipo. Haipo. Mungu ni mtakatifu. Mtakatifu. Mtakatifu. kasome Isaya Isaya sita nadhani ile m najaribu kuwafundisha hawa dada zangu waelewe kwa sababu mimi inaniuma sana karibu kila siku kila siku haiwezi ikapita siku sijapokea taarifa zao lakini wengi ukifuatilia ni kwa sababu hawakuwa na neno ndani yao walitanguliza mihemko

IMG-20250514-WA0008.jpg
 
Numelogy speaks it all. Not necessarily mtu mmoja akawa compatible na kila mtu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom