Mume aomba talaka baada ya kushindwa shughuli za kitandani

Mume aomba talaka baada ya kushindwa shughuli za kitandani

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,423
MUME ADAI TALAKA BAADA YA KUSHINDWA "MAJUKUMU"

Bwana mmoja jijini Mumbai nchini India, amepewa talaka yake, baada ya kulalamika kuwa hawezi kukata "kiu kubwa" aliyokuwa nayo mke wake ya kufanya tendo la ndoa.

kwa mujibu wa tovuti ya Metro - Mwanaume huyo akiwa amechoka, alifika katika mahakama inayoshughulikia masuala ya kifamilia mwezi Januari, akidai kuwa mke wake amekuwa akimnyanyasa kwa kutaka kufanya tendo la ndoa, tangu walipofunga ndoa mwaka 2012, na kuwa amekuwa akitumia 'mabavu na udikteta' wakati akitaka jambo lake.

Na hakuishia hapo: bwana huyo ameiambia mahakama kuwa mke wake pia alithubutu hata kumpa dawa za kuongeza nguvu, na kutishia 'kutembea' na wanaume wengine kama atashindwa kukata kiu yake kubwa.

Mume huyo akiwa taabani- ambaye amesema amesumbuliwa na maradhi ya kidole tumbo 'appendicitis' kutokana na kutopumzika, alipewa talaka aliyokuwa akidai.

"Kwa kuwa mshtakiwa (mke) hakutokea mahakamani, ushahidi wa mshtaki (mume) haujapingwa.

Na hivyo mahakama hii haina budi, ila kukubali ushahidi uliowasilisha" amesema Jaji Laxmi Rao.
 
Masikini mwanamme wawatu kaona bora ajivue isiwe tabu,na huyo mwanamke nae sijui kachanganya na nchi nyengine
manake wahindi hua wavumilivu sana kwenye ndoa zao huyu mbona mbabe anaitaka kupita maelezo..........
 
Swadaktaaaa

"pori limeshakushinda, uwaachie wenzio"

ni kipande cha wimbo wa taarab cha Elizabeth Sigira, mwimbaji wa zamani wa JKT Taarab
 
makubwa, sipati picha ingekuwa bongo
 
Kudaaadeki.... nikipata mwanamke wa hivyo mbona.mambo yatasonga
 
Hii ni kawaida kabisa

Unaweza kudhani hakuna wanawake ambao wanahitaji ngono kwa kiasi cha kutisha lakini wapo,tatizo ni wao kuwa wazi tu,inapopatikana mahali au wakati anakuwa wazi watu wanashangaa lakini ingekuwa nao wanaweza kuwa wazi kama wanaume ingekuwa ni kawaida tu na idadi ya wanaume ambao wanahitaji ngono kwa kasi ya ajabu ingekuwa sawa na ya wanawake

Malezi na jinsia yamewafanya wanawake waonekane kama wasiohitaji sana jambo hili wakati ukweli unaweza kuwa kinyume sana!
 
Yaani wakati Waname wengine wanalalamika kuwa Wake wananyima unyumba kumbe kuna wengfine wanakimbia Unyumba.

Kudadadekiiii!!!!!!!!!!!!!!!

Huyu mwanamke angekuja kwangu ningekesha hadi angekimbia yeye.
 
Back
Top Bottom