Kawaida ni kua you can not choose mwenzio aishi maisha gani.... But ukweli unabaki ulooweka hapa ni kweli kabisa kua haipendeza... na thou waweza ona kama wanamsimanga mgeni wao... IMO hio inatoa picha the type of people they are... Hicho kibao says Loads kuhusu Watu wenyewe... mahala wanaishi... attitude towards watu wa nje... Na lack of busara ya kuweza tafakari kua hapo wageni ni aina nyingi na wengine hawastahili kabisa waone huo ujumbe.... as much as they mean it...
Tena ww ndo umelengwa maana umeanza kuongea na mshkaji wako mambo ya kibao badala ya kuongea ishu iliyokupeleka ndo umbea huo wenyewe unaokusudiwa kwenye kibao.
Wao wenye nyumba ndo wanajua kwann wamekiweka kutokana na maswahibu yanayowakuta, we yanakuhusu nn maisha ya wa2-MIND UR BUSSINESS!
AT least kwa hapa TZ, hususani ukanda wa pwani, wanawake ni watu wanaopenda sana mipasho na maongezi ya mafumbo!!! Bila shaka ni wahitimu wazuri wa baadhi ya tanzu za fasihi simulizi. Last week, nilimtembelea rafiki yangu mmoja ambae mwenzangu ameoa (mie bado hivyo natoa offer kwa mwana-jf single wa kike apendae kuwa na mume!). Ile kuingia tu sebuleni, nikakutana na kibao kilichoandikwa "UKIJA UJE NA YAKO, UMBEYA NYUMBANI KWAKO!" Kwa bahati shemeji yangu (mke wa mshikaji) alikuwa hayupo kwa muda huo hivyo tukapata nafasi ya kutosha kujadili masuala ya kimaisha. Baada ya mimi kuona kibao hicho, nikamuuliza mshikaji kwanini ameweka hicho kibao. Akajibu, aliyeweka si yeye bali ni mke wake! Nikamuuliza kawalenga akina nani; akajibu "sijui yeye mwenyewe!" Baada ya majadiliano ya hapa na pale, nikamshauri akiondoe kibao hicho kv anafanya embrassement kwa wageni wake! Jamaa akadai kv alikuwa ni mke wake basi asingeweza kukiondoa yeye kv mke wake na yeye ana haki na hiyo nyumba! kimsingi, nilishindwa kabisa kumshawishi kukiondoa kibao hicho! Na kama ningekuwa nina mazoea ya kwenda kwenda pale nyumbani au kukutana na huyu rafiki yangu basi bila shaka ningejisikia vibaya sana kuhusu ujumbe ule! Sasa swali ninalojiuliza na kuwauliza wadau, je; ni muhimu kuwa na vibao vyenye ujumbe wa aina hii kwenye nyumba zetu?! Hivi hatuoni tunaanza kumsuta mtu ambae hata kuongea hajaongea tayari unamkaribisha kwa masimamngo?! Wengine unakuta wanaweka vibao vyenye ujumbe aina hii kwenye sehemu zao za biashara kama vile "HAPA CASH TU, KUKOPA HUKO HUKO!" HIVI ni busara kuwasemanga watu ambao hata mdomo hawajafungua?!
NAWASILISHA!!!
Kawaida ni kua you can not choose mwenzio aishi maisha gani.... But ukweli unabaki ulooweka hapa ni kweli kabisa kua haipendeza... na thou waweza ona kama wanamsimanga mgeni wao... IMO hio inatoa picha the type of people they are... Hicho kibao says Loads kuhusu Watu wenyewe... mahala wanaishi... attitude towards watu wa nje... Na lack of busara ya kuweza tafakari kua hapo wageni ni aina nyingi na wengine hawastahili kabisa waone huo ujumbe.... as much as they mean it...
Mstaarabu hawezi kuweka maneno hayo lkn na mstaarabu hawezi kwenda nyumbani kwa mtu akataka kumpangia cha kufanya vile vile
!Ushapata pm ngapi hadi sasa, maana kiaina uliwakilisha search.
Heheh mm nilienda nyumba moja ina kibao kizuuuri kimeandikwa ' All because two people fell in love' nilikitamani haswa...
Ndo maana yake kisukari, na ndio maana ninaamini nina wajibu wa kumshauri kile ninachohisi na kuamini ni right hata kama sitakuwa right!ni kweli hayo ndio maisha yao,lakini kwa maneno yaliyowekwa kama hayafai.mfano ningeenda kwa sister wangu,na kuona huo ujumbe,nisingekaa kimya,ningemuuliza tu na kumuelewesha.bila shaka urafiki wenu umeshibana,ndio maana umeyauliza.kwa jibu ulilipewa,siku nyengine usiyaulize tena.maana ndoa zina formular nyingi,mengine wewe utayaona kinyume,lakini kwa wao ni sawa tu
Unajua humu tunapeana ushauri na ujumbe nilopata kupitia hii thread ni kuwa tuwe makini na vibao tunavyoweka majumbani kwetu. Unaweza kuta huyo mwanamke kawawekea mawifi na wakwe zake; lakini hata marafiki wanaweza wasitie mguu hapo nyumbani kwenu kama ni watu wa vibao vya mafumbo.
Hata maneno tunayoongea kwenye mazungumzo yanaweza kufukuza wageni; kuna familia zinageuka kuwa ni gumzo na watu wanapeana tahadhari ya ku stay away from them kwa sababu ya midomo michafu na ya kejeli ya mmoja au wanandoa wote. Binadamu wa kawaida hawezi kufurahia kutengwa; kama tunapenda kuwa na ndugu na marafiki tuwe makini na mabango na maneno tunayozungumza.
Sikumwambia akitoe hicho kibao, bali nilimshauri akitoe!!! Bila shaka hapo utaona kuna tofauti kubwa kati ya kumwambia afanye kile ninachokiamini na kumshauri afanye kile ninachoamini kipo sahihi! Akiwa kama mshikaji wangu, nina haki na wajibu wa kumshauri ingawaje sina haki wala wajibu wa kumwambia/au kumpangia afanye jambo lolote! By the way, jaribuni kumwelewa mtu, huyo niliyemzungumzia ni my friend, na sio mtu mtu tu, kama ulivyomwita (ingawaje wapo watakaouliza kwani yeye sio mtu)!!! Ni mtu ambae sichelei kumwambia kitu chchote hata kama hawezi kukubaliana na mimi; na huo ndivyo urafiki ulivyo!
u're right AshaDii, na ndio maana sikukiondoa kile kibao kv wame-opt kuishi hivyo!!! Nilichofanya ni kumshauri kama rafiki on how could other pple perceive on such paintings! I still believe, it ain't right at all at least basing on my thinking ability!
Kwavile ninahisi kwamba wewe ni mwanamke, basi i've no comment!