Mume amuua mkewe kisa futari!

Mume amuua mkewe kisa futari!

Status
Not open for further replies.

Maneno izaak

Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
21
Reaction score
1
Mapenz yanaua! Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Dotto.anahusishwa na mauwaji ya mkewe anaye itwa Zainabu Bakari kwa kumchoma kisu na kusabisha kifo chake! Et kisa kukataa kurudiana naye ili awe anampikia futari katka mfungo huu wa mwez mtukufu wa ramadhan.
 
Dunia imeharibika mno leo kwenye habari kuna watoto wawili wameuwawa na wazazi wao wakufikia, ni mauaji mawili tofauti mmoja kauliwa na mama wa mambo mwingine kauliwa na baba wa mambo Yani huko tuendako cjui.....!!!!!
 
Kweli haya majanga, starehe ale na vimada wengine,miezi yote hiyo kakaa na hao wengine lakini futari aje apike aliyeachana nae.Huyo Dotto angekuwa amemuua Dada'angu ningegeuka Rashid Matumla
 
Kila siku ni mauaji mauaji tu!!!! tena wanaouliwa zaidi ni watoto, wanawake na wazee, sijui serikali inaliona hilo kama ndio ina mkakati gani ya kuzuia hivyo vifo vya makusudi. kwa mfano kuna habari gazeti la mwananchi leo mtoto kauliwa na kaka yake kwa kukatwakatwa mapanga hadi kutenganisha kichwa na kiwiliwili nimesikitika na nimeumia sana mtoto hana hatia yoyote kukatishwa maisha kirahisi rahisi tu!!!!! vyombo husika tumechoka na hayo mauaji chukueni hatua za haraka imagine ndio mwanao anauliwa utajiikiaje
 
Dotto, dotto, dotto, dottoooo, why!!?!! Kisa futar?!?! Si mke wa kulwa angekua anakupa futar?! Ona sasa umelikoroga! Segerea hiyooo inakuita!
 
Kweli haya majanga, starehe ale na vimada wengine,miezi yote hiyo kakaa na hao wengine lakini futari aje apike aliyeachana nae.Huyo Dotto angekuwa amemuua Dada'angu ningegeuka Rashid Matumla

Hizi ndoa za mafungu na danadana ndio shida yake. Mtu mmoja anakuwa na table ya vipindi vya kuolewa na kuachika as if ni footballer
 
Si angetafuta mwingine naye aoe zile ndoa za Shabaan-Ramadhan (Kuoana mwezi shabaan kuachana baada ya Ramadhan)
 
Kwani wakati anamuacha hakujua kama kuna wakati FUTARI?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom