Multiple choice questions - ktk mtihani wa maths std seven 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Multiple choice questions - ktk mtihani wa maths std seven 2011

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Campana, Jun 1, 2011.

 1. C

  Campana JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wapendwa wadau wa Elimu JF,

  Inasemekana kuwa serikali kupitia Wwizara yake ya Elimu, imeamua kuwa mtihani wa Hisabati darasa la saba mwaka huu utakuwa na maswali yote ya kuchagua (multiple-choice questions). Haiingii akilini uamuzi huu umefanywa kwa manufaa yapi, sababu katika hali ya kawaida sio rahisi kupata sifuri kwa mwanafunzi yeyote katika mitihani ya namna hii.

  Inasemekana shule zimeshataarifiwa, na mimi kama mzazi na mdau wa elimu, nimetembelea shule wanaposoma watoto wangu nikahakikishiwa jambo hili na nikaonyeshwa juhudi za waalimu kuwaanda watoto kwa mitihani hiyo itakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

  Inawezekana uamuzi huu una malengo yafuatayo:
  Moja, kulidanganya taifa kuwa kiwango cha ujuzi wa Hisabati kinakua, mara matokeo yatakapotangazwa,
  Mbili, kubana matumizi ya serikali inayofilisika kwa kupunguza muda wa usahihishaji wa mihihani hiyo,
  Tatu, kutumia wasahihishaji wasio wataalam wa Hisabati, hiyo kama kuwasaidia kwa viposho waweze kujikimu


  Vilevile kuna hatari kuwa wanafunzi wengi wasio na uwezo wa kusoma na kuandika watafaulu mitihani hiyo na kuingia sekondari.

  Ndugu, kama inawezekana kuzuia upuuzi huu usio na manufaa, tushauriane na tuweze kuuzuia maana ni hatari kwa mustakabali wa taifa linalochipuka.

  Nawasilisha

  [/LIST]
   
 2. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hawa watu wanaiharibu sana elimu, multiple choices ktk maths inamadhara makubwa sana mfano pale mwanafunzi anapofanya maswali 4 hlf amepata majibu ambayo hayapo kwenye choices basi anakuwa frustrated na kupoteza muda mwingi kurudia swali kutafuta jibu litalofanana. Mimi nimefanya hayo nikiwa chuo lkn kunakuwa na marks 3 za solution na 2 jibu nijuavyo shule ya msingi huwa hakuna marks za solution, kwa shule ya msingi ni mbaya sana na pia inawadumaza wanafunzi vichwa maana mwingine atasema nikiingia tu nachagua c swali la kwanza hadi la mwisho
   
 3. J

  Jerry k Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa mada. Wanajenga kizazi kisichoweza kufikiri kwa kina,kizazi kinachojengwa ni chenye uwezo mkubwa wa ku-guess.Hatari sana na inasikitisha.Ni matokeo ya kuwa na viongozi dhaifu wa kufikiri.
   
 4. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,988
  Likes Received: 20,391
  Trophy Points: 280
  Hii itakuwa ni hatari kubwa kwa usatwi wa vijana wa taifa letu, ninachukia sana elimu kusiasishwa, hapa tunaweza kupata watoto wasio na uwezo wa hisabati lakini kwa kuwa tu wanauwezo wa kufumba macho na kulengesha kalamu kwenye jibu basi kashafaulu, sic
   
 5. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Taifa linazidi kuangamia kwa utaratibu huu. Kijana aachwe aonyeshe njia na kuandika jibu ambalo yeye anaamini kuwa ni sahihi.

  Pia naomba mtambue kuwa zaidi ya asimilia 60 ya watoto wetu walioko KIDATO CHA KWANZA kwa sasa wameingia kidato cha kwanza wakiwa wamefeli somo la HISABATI KATIKA MTIHANI WAO WA KUMALIZA DARASA LA SABA MWAKA JANA (2010).
   
Loading...