Nyakipambo
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 435
- 141
Mullah Mohammad Omar
Taliban. Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kuwa kiongozi wa Kundi la Taliban, Mullah Mohammad Omar anaweza kugombea katika uchaguzi ujao wa rais uliopangwa kufanyika nchini humo mwezi Aprili, mwakani.
Rais Karzai alisema kuwa kiongozi huyo wa Kundi la Taliban anaweza kuwa mgombea wa kiti cha urais na kuwapa fursa raia wa nchi hiyo kumpigia kura ya ndiyo au hapana.
Alisema kuwa katiba ya Afghanistan ina uhalali kwa raia wote wa nchi hiyo na kwamba Kundi la Taliban pia linapasa kunufaika na katiba hiyo.
Rais Hamid Karzai aliyasema hayo siku chache baada ya kurejea kutoka safari ya kiserikali ya siku mbili huko Qatar ambako alijadiliana na viongozi wa nchi hiyo kuhusu uwezekano wa kufungua ofisi ya Taliban nchini humo kwa ajili ya mazungumzo ya kusaka amani.
Mullah Omar alikuwa mafichoni tangu Marekani iishambulie kijeshi Afghanistan mwaka 2001. Hii ni katika hali ambayo mwezi Januari mwaka jana vyombo vya habari vya Pakistan viliripoti kuwa Polisi wa Upelelezi wa Marekani (FBI) waliliondoa jina la kiongozi huyo wa Taliban katika orodha ya magaidi wanaosakwa kwa udi na uvumba na nchi hiyo.
Washington ililiondoa jina la Mullah Omar katika orodha hiyo licha ya kulituhumu Kundi la Taliban na kiongozi wa zamani wa Al Qaeda Osama bin Laden kuwa ndiyo waliohusika na mashambulio ya Septemba 11, nchini Marekani.
Mullah huenda akagombea urais - Kitaifa - mwananchi.co.tz