Muleba, Kagera: Watu 4 wamekufa leo baada ya hiace waliyokuwa wakisafiria kugongana na lori na kuungua moto

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,930
Habari zilizotufikia kutoka Muleba zinasema kuna ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo ikihusisha Gari dogo la abiria (Hiace) iliyokuwa ikitokea Muleba kuelekea mji mdogo wa Katoro wilayani Chato lililogongana na Gari kubwa la mafuta (Semi) nje kidogo ya mji wa Muleba katikakati ya Kyamiolwa na Kasharunga.

Watu 4 wamekufa leo baada ya hiace kuungua katika Kijiji cha Kashenyi wilayani Muleba, Kamanda Augustino Ollomi athibitisha

Kamanda Augustino amesema mwendo kasi wa dereva wa gari dogo la abiria ni chanzo cha ajali hiyo.

Ingawa Kamanda Olomi hakuwataja waliokufa, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango amesema miongoni mwao ni dereva wa gari dogo, kondakta na abiria watatu.

Amesema watu hao walishindwa kujiokoa kutokana na mlango wa gari kubanwa hivyo kushindwa kufunguka.


bukoba 1.jpg


bukoba 2.jpg


bukoba 3.jpg


bukoba 4.jpg
 
Watu 4 wamekufa leo baada ya hiace kuungua katika Kijiji cha Kashenyi wilayani Muleba, Kamanda Augustino Ollomi athibitisha.

More to follow
 
RIP wote mliopoteza maisha ktk ajali hiyo na nawaombea majeruhi uponyaji wa haraka in the name of Jesus.......
 
Back
Top Bottom