Muigizaji wa maisha ya mzanzibari Freddie Mercury ashinda Oscar

Hukusema achilia mbali kuandika.Halafu ulivyoandika mimi nikaku-quote na kuandika "Kakosea,mrekebishe"!

Nimemuuliza kwanza ili nijue kama anafahamu au la , pengine alikusudia kuandika kitu chengine, Lakini wewe umechupia au ni msemaji wake?
 
Kitu muhimu cha kukumbuka ni kuwa Freddie Mercury alizaliwa Zanzibar lakini hakuwa mzanzibari ndo maana wazanzibari wasingeweza kumclaim

Wazazi wa Freddie walihamia kutoka India ili babake kuja kuendelea na kazi yake ya ukeshia katika serikali ya ukoloni wa muingereza Zanzibar na wakapewa uraia wa Uingereza sababu waliishi katika serikali ya Uingereza japo ilikuwa ni Zanzibar, hivyo Freddie alipozaliwa mwaka 1946 alizaliwa kama raia wa Uingereza mwenye asili ya Uhindi aliezaliwa Zanzibar na ni hivyo kuwa alikuwa considered kama Muingereza tangu kuzaliwa kwake. Hata Freddie mwenyewe alikuwa akijichukulia kama Muingereza,alikuwa obsessed na westerners na alipenda sana kusikiliza miziki ya westerns kama vile Rock music na ndipo alipoamua kujibadili jina lake kutoka Faroukh Bulsara na kuwa Freddie Mercury na ndipo alipokuwa inspired kuwa anaandika nyimbo

Freddie pia hajaishi sana Zanzibar, ameishi miaka nane ya mwanzo na baada ya hapo akiwa na miaka minane alipelekwa kusoma boarding school nchini India, amesoma boarding takliban miaka nane na aliporudi Zanzibar hakukaa sana kwani mapinduzi ya Zanzibar yalitokea na ndipo yeye na familia yake walikimbia kwenda Uingereza

Hakuwa mzanzibari vipi na mapinduzi ya Zanzibar yametokea yeye akiwa kama raia kamili wa Zanzibar? na alikimbilia ingereza kama wakimbizi wengine waliokimbia?
 
Rami Malek aliua Ile scene ya
Freddie Mercury alipopiga tamasha la live aid pale Wembley stadium,daaa ukicompare unaona kama reality ya Ile show miaka Ile,
Jamaa alistahili Hiyo Tuzo maana aliua Sana Kwenye
Bohemian rhapsody!
 
ukiangalia hio movie vizuri, Freddy ushoga kauanzia huko huko Uengereza, kuna jamaa alimuingiza. lakini mwanzoni Freddy alikua yuko sawa na demu alikua naye, baadae ndio akawa Shoga. kwa hio wakati anaondoka Zanzibar aliondoka na marinda yake.
 
Nakumbuka kabisa siku Zeyana Seif aliyekuwa mtangazaji wa BBC Swahili alipotangaza kifo cha Freddy Mercury. Siku moja kabla ya kifo chake ndiyo alijitangaza rasmi kuwa ana HIV ijapokuwa kulikuwa na maneno ya chini kwa chini mengi wakisema alikuwa muathirika. Na members wa group lake nadhani walimalizika kwa ugonjwa huo.

Enzi zile bado ilikuwa ni kitisho.
 
Back
Top Bottom