Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' abadilishiwa adhabu, sasa kutumikia kifungo cha nje



Msanii nyota wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu Lulu, amepunguziwa muda wa kifungo kwa msamaha wa Rais John Magufuli, alioutoa kwa wafungwa katika Sikukuu ya Muungano Aprili 26, mwaka huu.

Rais hutoa msamaha kwa wafungwa wenye vigezo ambapo kama ameshatumikia robo ya hukumu yake anaweza kuachiwa huru lakini kama hakufikisha robo, atapunguziwa 1/6 ya hukumu yake.

Msamaha wa rais kwa msanii huyo ambaye alitakiwa kutoka gerezani Machi mwaka 2019, ulipelekea muda wake kupungua na siku yake ya kutoka kuwa Novemba 12 2018.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatatu Mei 14, Naibu Kamishna wa Magereza, Augustino Mboje amesema baadaye Magereza ilipokea amri kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kwamba mfungwa huyo amebadilishiwa adhabu hivyo wamwachie huru.

“Ieleweke bado ni mfungwa wetu na angeendelea kukaa gerezani hadi Novemba 12, mwaka huu ila hiki kifungo kimepunguzwa kwa msamaha wa rais bila msamaha wa rais ambaye amempunguzia moja ya sita ya adhabu ya kifungo chake, ilikuwa atoke machi 12, mwaka 2019.

“Kwa hiyo bado ni mfungwa kwa mujibu wa Sheria Community Service Namba sita ya 2002 ambayo inaruhusu mtu kutoka akawa na kifungo cha nje yaani kifungo cha huduma za jamii, hii ina maana atapangiwa kazi wilayani, sijui wilaya gani, na atapangiwa kazi kwa masaa fulani kwa siku tano. Hatakuwa chini yetu yetu kwa masharti ya sheria hiyo,” amesema.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili Novemba mwaka jana, kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpenzi wake, Steven Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, Aprili 7, mwaka 2012.
 
Akina Aveva, Malinzi, Nyange Kaburu watatoka lini jamani? Nawaonea huruma sana hawa wanamichezo wenzetu. Nadhani basi wangepewa hata dhamana da!! Uwa nikimuona Aveva, Kaburu, Malinzi nasikitika sana. Natambua kuwa wanaweza wakawa wanamakosa, ila wapewe dhamana. Badala yake wanatolewa watu ambao ni hasara kwa Taifa kama Lulu.
Sidhani kama watatoka leo au kesho maana na makofia nae anatafutwa aunganishwe
 
Hizo ni story za vijiwe vya kahawa, lulu kila siku anaonekana pale ukonga akipiga kazi za usafi,

Lulu nilisha mwona kama mara mbili akiwa na wafungwa wenzake wamama wanakusanya na kuhamisha kuni na miti, gerezani alitoka lini isijulikane?

Haha wabongo bhana kweli raha
Lol, Ukonga hakuna wafungwa wanawake... labda useme ulimuona Segerea na ndiko alikokua.
 
Mara msamaha wa Rais, mara amri ya Mahakama Kuu. Tushike lipi? Mahakama Kuu ilifikaje kutoa amri pasipo na rufaa? Au ilifanya marejeo yenyewe? Shibisha Mkuu katika habari hii
nina wasiwasi huyu ni mtumishi undercover... ndio maana hata maajabu ni mengi kwake... fatiria kuanzia mwanzo mpaka huu mwisho...
 
ndio tofauti yetu wananchi na wenye nchi. Haya niambieni hali ya mama kanumba huko aliko hahahaha
 
Back
Top Bottom