Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' abadilishiwa adhabu, sasa kutumikia kifungo cha nje

Sababu ya kubadilishiwa adhabu ni ipi kwa mujibu wa magereza?? anayejua aniambie nijifunze

Hapa ndo zile conspiracy theories za kwamba Kanumba ilikuwa lazima afe na atakayemuua ataachiwa au kutakuwa na hukumu ya kiupendeleo zina apply.

Tutaletewa swaga za hazijaiva, au msamaha wa Rais toa ¼ na ⅓
 
ile kesi ngumu sana maana ukweli anao lulu na marehemu... plus na jina kubwa la lulu ni kesi ngumu sana kumfunga kifungo cha kibabe
 
Kuna mtu aliniambia kitambo tu lulu hayupo gerezani.

Iko hivi lulu alipohukumiwa wakafanya mpango lulu akaandiksha watu wa3 tu ndio anahitaji waende kumuina gerezani, majizzo, mama yake na dr cheni. Mtu akienda hapat nafas ya kuonana nae, halafu mule ndani ya gereza zikawekwa taarifa kuwa lulu amehamishwa gereza ili wafungwa wenzie wasishitukie lolote kwa lulu kukosekana gerezani.. Hapo ndio lulu kachukuliwa kafichwa mtaani anakula maisha ndani tu, watu wamepiga pesa.
Hizo ni story za vijiwe vya kahawa, lulu kila siku anaonekana pale ukonga akipiga kazi za usafi,

Lulu nilisha mwona kama mara mbili akiwa na wafungwa wenzake wamama wanakusanya na kuhamisha kuni na miti, gerezani alitoka lini isijulikane?

Haha wabongo bhana kweli raha
 
Nakubalina na wewe haiwezekani ulikuwa ukienda kumwona jela huwezi kumwona ata anakataa... hakuna msanii hata mmoja amewahi kwenda kumwona jela... hakuna ha ha ha ha aha
Hapa ndio bongo dar es salaam. Watu wanajua yupo gerezani kumbe anakula bata ufichoni uraiani. Hahaa.
 
Dady is coming,,, ndio amefika leooo hiii tz hiiiiiii dadekiiii zakeeee
 
he he heee "" hii nchi raha sana "" MAMA KANUMBA KAMA NAMUONA HUKO ALIKO"" ....waliosema kuwa dunia haina usawa hawakuwa wamekosea..walishawahi kukutana na matukio yanye mfananao watukio kama hili "pia "
Misemo mingi inazuka baada ya kukuta, yakishakukuta ndio unapata la kulonga..

Ni kweli dunia haina usawa.
 
Baby baby ashafanya yake... hapo maadui zake watatembelea mikono kwa jinsi ambavyo Lulu huwa anabwabwaja!
 
Hizo ni story za vijiwe vya kahawa, lulu kila siku anaonekana pale ukonga akipiga kazi za usafi,

Lulu nilisha mwona kama mara mbili akiwa na wafungwa wenzake wamama wanakusanya na kuhamisha kuni na miti, gerezani alitoka lini isijulikane?

Haha wabongo bhana kweli raha
Mkuu ukitaka kubisha bisha, jf kichaka tusijekuropoka mengine tukaanza kusakana na wasiojulikana, ila yangu ndio hayo. Habari hii ni ya uhakika asilimia 99.9999999%, mengin tuachie hapo.

Hushikiwi fimbo wala bunduki ili uamini.
 
hydrochloric acid meet again vigogo from Tanzania hicho kifungo cha nnje kwa TZ ni sawa na kumuambia mtu kila day apeleke buku 10 ukonga then arudi home kula bata naamin kifungo hakitafuatwa kama kilivyoandikwa bali ni kama kitakavyo dadavuliwa
 
Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael, maarufu Lulu, amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia 'kifungo cha nje' kwa amri ya Mahakama Kuu Tanzania.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Akizungumza na MCL Digital Jumatatu Mei 14,2018, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tananzia, Dar es salaam.

"Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje, kitaalamu tunaita ' Community service'' amesema Mboje

Chanzo: Mwananchi

View attachment 776666
Dady is coming
 
Alipofungwa waliongea mbovu ...ametoka watachonga mbovu...!!
Hajatoka, amebadilishiwa adhabu. Bado yupo kifungoni. Tunasubiri vijana wa kiisilamu waliopo team Lumumba waweke hisia zao hapa kuhusu masheikh wa Uamsho
 
Back
Top Bottom