PostGE2025 Muhtasari Taarifa ya Awali ya Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025 kutoka SADC (SOEM): Uchaguzi haukutimiza Viwango vya Uchaguzi wa Kidemokrasia vya SADC

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Black Opal

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2023
Posts
304
Reaction score
543
Hapa chini ni muhtasari wa taarifa ya awali (final) ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 kutoka SADC (SEOM), uliowasilishwa na Richard Msowoya, Spika wa zamani wa Bunge la Malawi na Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa SADC.

Upo kwa kifupi na kwa Kiswahili, ukitaka maelezo zaidi pitia PDF.

===
1762437457341.png

MUHTASARI WA TAARIFA YA AWALI YA WAANGALIZI WA SADC (SEOM) – UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2025

Utangulizi

Ujumbe wa Waangalizi wa SADC (SEOM) ulialikwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushuhudia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, uliofanyika tarehe 28 na 29 Oktoba 2025. Ujumbe ulikuwa na watu 80 kutoka nchi 10 wanachama wa SADC, waliotumwa katika mikoa 27 ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Taarifa hii inahusu kipindi cha kabla ya uchaguzi, siku ya kupiga kura, na mchakato wa kuhesabu kura. Ripoti ya mwisho itajumuisha pia tathmini ya kipindi cha baada ya uchaguzi.

Mambo Makuu Yaliyobainishwa

1. Changamoto kwa waangalizi

  • Waangalizi walikumbana na ugumu wa kupata ushirikiano kutoka baadhi ya wadau, hasa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), kutokana na kuchelewa kupatiwa barua za utambulisho rasmi.
  • Baadhi ya wadau hawakuwa tayari kushirikiana kikamilifu na waangalizi, na waliwarejelea kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa maelezo zaidi.
  • Baadhi ya maafisa wa usalama waliwahoji waangalizi kwa ukali, wakachukua nyaraka zao (japokuwa zilirejeshwa baadaye) na hata kuwalazimisha kufuta picha za kazi zao.
***SEOM ikakumbusha kuwa nchi wanachama wa SADC zinatakiwa kuruhusu waangalizi kushuhudia mchakato mzima wa uchaguzi bila vikwazo.

2. Hali ya kisiasa na kiusalama
  • Kwa ujumla, hali ilikuwa tulivu na ya amani, isipokuwa matukio machache ya vurugu mwishoni mwa upigaji kura.
  • Baadhi ya wadau walieleza kuwa utulivu huo ulitokana na ratiba ya kampeni iliyopangwa na INEC ili kuepusha migongano kati ya vyama.
  • Hata hivyo, wadau wengine walisema kulikuwa na vitisho na hofu ya kisiasa, ikiwemo madai ya utekaji wa wanaharakati na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani kama vile Tundu Lissu (CHADEMA) na kukataliwa kwa wagombea kama Luhaga Mpina (ACT-Wazalendo).
  • Tukio hili lilionekana kupunguza ushindani wa kisiasa na kuathiri ushiriki wa wananchi.
***Katika muktadha huu, ujumbe wa SADC umeelekeza umakini kwenye Kifungu cha 4.1.7 cha Kanuni na Miongozo hiyo, kinachozitaka nchi wanachama kuhakikisha mazingira ya ushindani wazi bila vizuizi visivyo vya lazima, na kutoa haki kwa raia wote waliostahili kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi.

3. Usimamizi wa mchakato wa uchaguzi
  • INEC na ZEC zilionekana kujiandaa vizuri kwa uchaguzi.
  • Usajili wa wapiga kura ulifanyika kwa awamu tatu kati ya Julai 2024 na Julai 2025, na jumla ya wapiga kura 37.6 milioni walisajiliwa, ongezeko la 26.5% ukilinganisha na 2020.
  • Wanawake walikuwa asilimia 50.3 ya wapiga kura.
  • Wadau walitofautiana kuhusu mageuzi ya sheria za uchaguzi – baadhi waliona hayajafanyika vya kutosha.
  • Kwa taarifa hii ya awali, SEOM imejikita kwenye hoja chache muhimu zinazohusu umuhimu wa kufanyika kwa mageuzi ya mfumo wa uchaguzi:
    • Kutokuwepo kwa haki ya kupinga matokeo ya urais mahakamani.
    • Ukosefu wa uhuru kwa tume za uchaguzi, kwani wajumbe wake wanateuliwa na Rais ambaye pia ni mgombea.
    • Kutokuruhusiwa kwa wagombea binafsi (wanaogombea bila chama).
    • Kupiga kura mapema kwa askari Zanzibar pekee, jambo lililoibua mjadala kuhusu uadilifu wa zoezi hilo.
4. Uwakilishi wa kijinsia na vijana
  • Kati ya wagombea urais 17, watatu tu walikuwa wanawake.
  • Vikwazo vikuu vilivyotajwa: ukosefu wa fedha, malezi ya uongozi, mfumo wa uteuzi ndani ya vyama, na mitazamo ya kijamii inayopendelea wanaume au watu waliooa/olewa.
5. Ushiriki wa watu wenye ulemavu
  • Wapiga kura 49,174 walikuwa ni watu wenye ulemavu.
6. Elimu ya mpiga kura
  • Asasi za kiraia, hasa zile zinazoongozwa na vijana na wanawake, zilihusika kikamilifu kutoa elimu ya uraia.
  • Njia zilizotumika ni pamoja na redio, televisheni, magari yenye vipaza sauti, vipindi vya muziki na michoro za katuni.
  • Hata hivyo, kulikuwa na upungufu wa fedha na kuchelewa kwa idhini za uelimishaji, jambo lililosababisha baadhi ya mashirika kukosa muda wa kutekeleza programu zao.
  • Baadhi ya mashirika makubwa ya kiraia yaliona kuwa yalikataliwa makusudi kupewa idhini na INEC, jambo ambalo linaweza kuwa limeathiri ubora wa elimu ya wapiga kura.
7. Uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari
  • Kulikuwa na malalamiko kuhusu ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza, hasa mtandaoni, kwani baadhi ya mitandao ya kijamii haikupatikana.
  • Vyombo vya habari vya serikali vilionekana kuzingatia zaidi chama tawala, huku vyombo binafsi vikijizuia kwa hofu ya kufutiwa leseni.
  • Ukosefu wa fedha na hofu ya wafadhili pia uliathiri uwezo wa vyama vya upinzani kujitangaza.
Uangalizi Siku ya Uchaguzi
  • Upigaji kura ulianza kwa utaratibu na amani katika maeneo mengi, lakini kulikuwa na matukio ya risasi na vurugu katika baadhi ya mikoa kama Mbeya, Dodoma, Arusha na Dar es Salaam ambapo polisi walirusha risasi.
  • CCM ilikuwa na mawakala wengi zaidi ukilinganisha na vyama vingine, huku katika baadhi ya vituo mawakala walizuiliwa kuingia kwenye vituo vya kupiga kura kuangalia taratibu za ufunguzi.
  • 70% ya vituo havikuwa na mabango ya kampeni, na 93% vilifunguliwa kwa wakati.
  • 85% ya vituo vilivyoangaliwa, Afisa wa Kituo alionyesha sanduku tupu la kura kwa wote waliokuwepo kabla ya kulifunga.
  • Vifaa vya uchaguzi vilikuwapo kwa kiwango cha kuridhisha, lakini kulikuwa na mwonekano wa askari wengi katika baadhi ya vituo, hasa Dar es Salaam.
  • Idadi ndogo ya wapiga kura iliripotiwa, na katika baadhi ya vituo hakukuwa na wapiga kura kabisa.
  • Waangalizi wa ndani hawakuwepo katika sehemu nyingi za kupigia kura
  • Kulikuwa na tuhuma za udanganyifu wa kura kutokana na kura za mafungu zilizokuwa zimepangiliwa vizuri kwenye masanduku ya kura zikiashiria watu walipiga kura nyingi kwa wakati mmoja, pamoja na ukosefu wa waangalizi wa ndani katika vituo vingi.
  • Kufungwa kwa mtandao wa intaneti kulizuia SEOM kupata takwimu kamili za upigaji kura na kuhesabu
  • Waangalizi wengi hawakuweza kushuhudia kufungwa na kuhesabiwa kwa kura kutokana na matukio na vitisho vya vurugu katika baadhi ya maeneo.
Mapendekezo ya Awali
  1. Serikali ianzishe mchakato wa katiba mpya au marekebisho yatakayoruhusu wagombea binafsi na kesi za uchaguzi wa urais kupelekwa mahakamani.
  2. Waangalizi wa kimataifa wapewe nyaraka na kibali kwa wakati, na waheshimiwe wanapotekeleza majukumu yao.
  3. Vyama vya siasa vizingatie sheria mpya za usawa wa kijinsia ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa.
  4. Kuwe na mazingira wezeshi kwa kila mtu yanayoondoa vikwazo vya kuizia uteuzi kwaajili ya uchaguzi
Hitimisho

SEOM imebaini kuwa:
  • Mchakato wa kabla na mwanzo wa uchaguzi ulifuata utaratibu.
  • Hata hivyo, kutokana na mazingira ya hofu, vikwazo vya mawasiliano, na changamoto za uwazi, wapiga kura wengi hawakuweza kuonesha kwa uhuru matakwa yao ya kidemokrasia.
  • Kwa msingi huo, uchaguzi wa mwaka 2025 haukutimiza kikamilifu viwango vya Uchaguzi wa Kidemokrasia vya SADC.
SEOM imetoa wito kwa Watanzania kutumia njia za kisheria kushughulikia malalamiko yao na kuepuka vurugu. Ripoti ya mwisho itatolewa ndani ya siku 30 baada ya taarifa hii ya awali.

***SEAC itarudi wakati unaofaa kufanya ukaguzi baada ya uchaguzi ili kubaini kiwango ambacho mapendekezo ya SEOM yametekelezwa na aina ya msaada, ikiwa upo, ambao Nchi Mwanachama inayoshiriki uchaguzi inaweza kuhitaji kutoka eneo la SADC.

Asante sana.
 
Attachments

Hata taarifa ya AU imesema uchaguzi ulikuwa ni wa hovyo.

Wamemgeuka mwenyekiti wao aliyempongeza Samia 😂
Atabaki kutoa macho tu, kila mtu atamgeuka, hata kivuli chake kitamkimbia
 
Hapa chini ni muhtasari wa taarifa ya awali (final) ya waangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 kutoka SADC (SEOM), uliowasilishwa na Richard Msowoya, Spika wa zamani wa Bunge la Malawi na Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa SADC.

Upo kwa kifupi na kwa Kiswahili, ukitaka maelezo zaidi pitia PDF.

===
View attachment 3498185

  • Kuwe na mazingira wezeshi kwa kila mtu yanayoondoa vikwazo vya kuizia uteuzi kwaajili ya uchaguzi
Mapendekezo ya Awali
  1. Serikali ianzishe mchakato wa katiba mpya au marekebisho yatakayoruhusu wagombea binafsi na kesi za uchaguzi wa urais kupelekwa mahakamani.
  2. Waangalizi wa kimataifa wapewe nyaraka na kibali kwa wakati, na waheshimiwe wanapotekeleza majukumu yao.
  3. Vyama vya siasa vizingatie sheria mpya za usawa wa kijinsia ili kuongeza ushiriki wa wanawake katika siasa.
  4. Kuwe na mazingira wezeshi kwa kila mtu yanayoondoa vikwazo vya kuizia uteuzi kwaajili ya uchaguzi
Hitimisho

SEOM imebaini kuwa:
  • Mchakato wa kabla na mwanzo wa uchaguzi ulifuata utaratibu.
  • Hata hivyo, kutokana na mazingira ya hofu, vikwazo vya mawasiliano, na changamoto za uwazi, wapiga kura wengi hawakuweza kuonesha kwa uhuru matakwa yao ya kidemokrasia.
  • Kwa msingi huo, uchaguzi wa mwaka 2025 haukutimiza kikamilifu viwango vya Uchaguzi wa Kidemokrasia vya SADC.
SEOM imetoa wito kwa Watanzania kutumia njia za kisheria kushughulikia malalamiko yao na kuepuka vurugu. Ripoti ya mwisho itatolewa ndani ya siku 30 baada ya taarifa hii ya awali.

***SEAC itarudi wakati unaofaa kufanya ukaguzi baada ya uchaguzi ili kubaini kiwango ambacho mapendekezo ya SEOM yametekelezwa na aina ya msaada, ikiwa upo, ambao Nchi Mwanachama inayoshiriki uchaguzi inaweza kuhitaji kutoka eneo la SADC.

Asante sana.
Watu wengine wana roho ngumu sana. Dunia nzima inasema uchaguzi haukukidhi viwango vya uchaguzi wa kidemokrasia, lakini yule layama wa Kizimkazi anakuambia ni uchaguzi “usiotiliwa shaka”. WTF!

Wakati mwingine mimi nafikiri hata Ibilisi is no match for this blood-thirsty monster!
 
SADC na Au wamesema kulikuwa na UCHAFUZI na sio UCHAGUZI!haya sasa kazi kwako SAMUYA!
 
Watu wengine wana roho ngumu sana. Dunia nzima inasema uchaguzi haukukidhi viwango vya uchaguzi wa kidemokrasia, lakini yule layama wa Kizimkazi anakuambia ni uchaguzi “usiotiliwa shaka”. WTF!

Wakati mwingine mimi nafikiri hata Ibilisi is no match for this blood-thirsty monster!
Madaraka matamu Mkuu hadi mtu anakuwa Shetani
 
Back
Top Bottom