MUHONGO: Marufuku kununua nguzo za umeme nje ya nchi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na wakandarasi wake kununua nguzo za umeme kutoka nchi za nje wakati nguzo hizo zinazalishwa kwa wingi na wawekezaji wa ndani.

Profesa Muhongo alitangaza marufuku hiyo alipofanya ziara mkoani Njombe hivi karibuni na kutembelea kiwanda cha kuzalisha umeme unaotokana na mazao ya miti.

“Tuna miradi mingi, wakandarasi wameenda kununua nguzo Uganda, wamenunua nguzo Kenya, wamenunua nguzo Zimbabwe na sasa hivi wananunua nguzo nyingi kutoka Afrika Kusini. Sasa tumemsikia ndugu yetu pale ana nguzo… kwa hiyo lazima hicho kikao chenu na nyie Mkoa mwende pale,” alisema Profesa Muhongo.

“Mkinunua hizo nguzo kwanza nyie mtapanua mashamba, wakulima watapata kazi. Na kuna wengine wakulima wa miti waliopanda miti wanavuna wanaweza wakakiuzia hicho kiwanda (cha kufua umeme),” alisema.

Waziri huyo wa nishati pia alikitaka kiwanda hicho pia kupunguza bei ya umeme kinacholiuzia shirika hilo.
 
Huu ndio uzalendo tunaotaka wa kuthamini vitu vya ndani kuliko vya njee. Kama bidhaa inaweza kupatikana au kutengenezwa hapa nchini kwanini tuanze kuhangaika huko nje. Hii ni namna ya kuwainua watanzania. Ila wamechelewa sana. Ni hatua nzuri.
 
Muhongo ni mzalendo kweli, baadhi ya media zilijaribu kumchafua lakini huyu mzee wa kijita anaipenda nchi yake. Kwanini tuhangaike kununua nguzo nje ya nchi wakati nchi imejaa misitu yenye miti mizuri!. Watu wametengeneza "cha juu", fedha nyingi imetumika katika manunuzi, tufike maliza tuseme sasa basi. Well Done Geologist Muhongo.
 
Akili za kushikiwa hizo, Tanesco ina zaidi ya miaka 10 inanunua nguzo nje, inamaana alipokuwepo wakati Wa mkwere hakuliona hilo.SIFA zimwendee JPM

Waziri hufanya kazi kulingana na matakwa ya rais, wewe mwenye akili za kwako mwenyewe huoni kuwa Ombeni Sefue wa JK ndio huyu huyu wa JPM?, mbona alikuwa anakula bata tu enzi za mkwere?. Afrika haina misingi ya uongozi inayokuwepo bila ya kuangalia madarakani kipo chama gani, kila anayeingia kwenye uongozi anakuja na kauli mbiu yake huku akifanya kazi na watu wake anaowaamini. Na sio hili tu ambalo linathibitisha uwezo wa Muhongo kikazi labda ndugu yangu wewe ni mmoja wa wale waliofuata mkumbo wa kumkashifu Muhongo?. Huwezi kumsifu JPM pasipo kumsifu Muhongo.
 
Akili za kushikiwa hizo, Tanesco ina zaidi ya miaka 10 inanunua nguzo nje, inamaana alipokuwepo wakati Wa mkwere hakuliona hilo.SIFA zimwendee JPM

Kwani alipokuwepo wakati wa JK ulikuwa humsikii akiwakataza TANESCO kununu nguzo kutoka nje? hukumbuki kuwa ni yeye aliyeibua ulaghai wa Tanesco kununua nguzo hapa nchini kisha wanasema zimenunuliwa South Africa? Au ulikuwa unanyonya na kuvalishwa nepi kipindi hicho?
 
...funny thing is ni miti hiyo hiyo inauzwa nje wanaifanyia treatment kule then inakuja tena kuuzwa huku!.
 
hats off kwa sos muhongo. lazima kwanza tuangalie ndani. huu ndo uzalendo niliokuwa nikiusubiri. bila shaka na wengine watafuata nyayo za sos muhongo. namna hii hata ajira zitaongezeka. pia wizara husika ifanye buzuki(promo) kubwa kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa nchini. wananchi waelimiswe faida za kununua bidhaa zinazozalishwa nchini. mbona japs wanafanya hivyo tena kwa nguvu na wamefanikiwa sana.
 
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amepiga marufuku Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na wakandarasi wake kununua nguzo za umeme kutoka nchi za nje wakati nguzo hizo zinazalishwa kwa wingi na wawekezaji wa ndani.

Profesa Muhongo alitangaza marufuku hiyo alipofanya ziara mkoani Njombe hivi karibuni na kutembelea kiwanda cha kuzalisha umeme unaotokana na mazao ya miti.

“Tuna miradi mingi, wakandarasi wameenda kununua nguzo Uganda, wamenunua nguzo Kenya, wamenunua nguzo Zimbabwe na sasa hivi wananunua nguzo nyingi kutoka Afrika Kusini. Sasa tumemsikia ndugu yetu pale ana nguzo… kwa hiyo lazima hicho kikao chenu na nyie Mkoa mwende pale,” alisema Profesa Muhongo.

“Mkinunua hizo nguzo kwanza nyie mtapanua mashamba, wakulima watapata kazi. Na kuna wengine wakulima wa miti waliopanda miti wanavuna wanaweza wakakiuzia hicho kiwanda (cha kufua umeme),” alisema.

Waziri huyo wa nishati pia alikitaka kiwanda hicho pia kupunguza bei ya umeme kinacholiuzia shirika hilo.

Ajabu sana nguzo zinazalishwa Njombe, zinasafirishwa kwenda Kenya, then tunazinunua toka Kenya kwenda kusambazia umeme Igwachanya, Kidugala, Ilembula, na maeneo mbalimbali ya Njombe yenyewe ikiwa na Kibena kilipo hicho kiwanda cha kuzalisha hizo nguzo
 
Safi sana Prof.
Sasa nadhani ni wakati wa kuifumua na kuigawanya Tanesco Uzalishaji na Usambazaji.

Waonyeshe ubora wako wale wote waliokupaka matope kwa kufanya zaid ya hayo, mpaka waje wakuombe radhi
 
Huu ndio uzalendo tunaotaka wa kuthamini vitu vya ndani kuliko vya njee. Kama bidhaa inaweza kupatikana au kutengenezwa hapa nchini kwanini tuanze kuhangaika huko nje. Hii ni namna ya kuwainua watanzania. Ila wamechelewa sana. Ni hatua nzuri.
Of course imports za nguzo huchangia kushusha thamani ya shilingi
 
Back
Top Bottom