Muhingo Rweyemamu Niliyemfahamu...

maggid

Verified Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Points
1,500

maggid

Verified Member
Joined Dec 3, 2006
1,084 1,500
Ndugu zangu,

Ametutoka, Muhingo Rweyemamu. Kila nilipokutana nae nilizoea kumwita Kaka.

Nilifahamiana na Muhingo kupitia ndugu yangu Absalom Kibanda. Nakumbuka jioni moja mwaka 2000 giza likianza kuingia nyumbani kwetu Kinondoni Biafra , alikuja Absalom Kibanda.

Nikakaa nae sebuleni. Kibanda akaliweka gazeti la Mwananchi mezani. Kisha akatamka;

" Braza niko na Muhingo tunaomba uanze kutuandikia makala kwenye gazeti hilo tunaloliongoza."

Nilimkubalia Kibanda na hazikupita siku mbili akanikutanisha na Muhingo Rweyemamu pale kwenye ofisi zao, Jengo la CCM Kariakoo.

Muhingo alinichangamkia sana na akaniahidi ushirikiano. Tangu hapo tukaanza kufahamiana zaidi.

Nakumbuka mwaka 2003 nilipata bahati ya kupanda basi moja na Muhingo kuanzia Ubungo kwenda Iringa. Ni basi la Scandinavia. Naweza kabisa kusema, kwenye safari ile ndipo niliweza kumfahamu zaidi Muhingo.

Safari ile ya saa tisa barabarani ilikuwa darasa kubwa na muhimu kwangu. Wakati huo nilikuja likizo nikitokea Sweden. Muhingo aliweza kunieleza mengi anayoyaona na anavyoyatafsiri kupitia uandishi. Muhingo alionyesha kuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya nchi hii hata yale yasioandikwa magazetini.

Mahali fulani kwenye mazungumzo yetu tukaingia kwenye mgogoro wa DR Congo. Muhingo tena akaonyesha alivyo na uelewa mpana wa Nchi za Maziwa Makuu na migogoro yake.

Mathalan, alinisimulia safari yake ya kiuandishi kupitia Rwanda hadi Goma akiwa nyuma ya vikosi vya Laurent Kabila. Alinieleza jinsi askari wale walivyowafuata milimani wanajeshi wa Maimai. Milio ya bunduki na mabomu ilikuwa ni kitu cha kawaida na akazoea. Akanithibitishia pia kuwa askari wa Kagame nao waliokuwepo kwenye operesheni ile ndani ya DRC.

Tukafika Iringa kwa basi kwenye safari niliyoiona fupi sana kutokana na mazungumzo yangu na Muhingo.

Jioni ile nikiwa Iringa, Muhingo aliyekuwa, wakati huo, Mwanafunzi wa Tumaini University, alihakikisha nafika anakoishi pale maeneo ya Semtema.

Nilipofika Semtema, kwenye nyumba ndogo aliyokuwa akiishi Muhingo, aliishi pia ndugu yangu Assah Mwambene. Naye alikuwa mwanafunzi wa Tumaini University.

Mazungumzo yaliendelea tukiwa watatu kwenye familia ya habari.
Chakula kikapikwa, tukala. Tukaendelea na mazungumzo kuhusu masuala mbali mbali ikiwamo media na demokrasia. Tuliongea hadi usiku mwingi.

Kesho yake Muhingo alinialika kutembelea Tumaini University. Nilipofika Chuoni ndipo nilipoona namna Muhingo alivyoheshimika kuanzia kwa wanafunzi wenzake hadi wahadhiri wa chuo.

Muhingo alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji kwenye Serikali ya Wanafunzi. Kwa nafasi yake hiyo alinitembeza kila idara kunionyesha.

Muhingo akaendelea kuwa kaka yangu tuliyeheshimiana na kushirikiana. Kila nilipofika Habari Corporation akiwa Mhariri Mtendaji, Muhingo akioniona naongea na wanafamilia wengine chumba cha habari alikuwa akiniambia;

" Maggid, ukimaliza usiondoke bila kupanda juu ofisini kwangu tuongee."

Akiwa DC Handeni, nilikutana nae pale Chalinze kwenye mgahawa wa Kituo Cha Mafuta cha Kobil. Aliponiona alifurahi sana. Alinitambulisha kwa Mkurugenzi wake wa Halmshauri na kunikaribisha nifike Handeni nikaoene shughuli zinazofanyika huko na kushauri inapowezekana. Alinisisitiza. Bahati mbaya sikuweza kufika Handeni.

Akiwa DC Makete, Muhingo nilikutana nae kwenye Jengo la Akiba ( NSSF) Iringa.

Aliponiona alifurahi sana. Akanitamkia kama alichonitamkia Chalinze. Bahati mbaya tena sikuweza kufika Makete.

Kaka yangu Muhingo umeondoka nikiwa na mengi niliyojifunza kutoka kwako kupitia media.

Nasikitika pia , sikuweza kukuona na kujifunza kutoka kwako kupitia Utumishi wa Umma kama kiongozi wa Serikali.

Kaka yangu Muhingo Rweyemamu, umeondoka nikiwa na hamu ya siku moja kukaa na wewe tukarejea mazungumzo yetu ya kwenye basi lile la Scandinavia kutoka Dar kwenda Iringa. Kufanya tathmini ya nini kimetokea na nini tafsiri yake.

Nitakukumbuka.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
 
Attachments:

  • File size
    21.7 KB
    Views
    51

gogo la shamba

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2013
Messages
6,677
Points
2,000

gogo la shamba

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2013
6,677 2,000
mimi nilisoma shule moja na Xyes Muhingo alikuwa kichwa sana je?wana undugu na huyu jamaa?tulisoma Vituka sec.kuanzia mwaka 1975 na wengine walikuwa Kassimu Masuod,Zuberi Masoud,Juma Chopeka,Shila.Amra Buringa nk
 
Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2006
Messages
2,124
Points
1,500

Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2006
2,124 1,500
Ndugu zangu,

Ametutoka, Muhingo Rweyemamu. Kila nilipokutana nae nilizoea kumwita Kaka.

Nilifahamiana na Muhingo kupitia ndugu yangu Absalom Kibanda. Nakumbuka jioni moja mwaka 2000 giza likianza kuingia nyumbani kwetu Kinondoni Biafra , alikuja Absalom Kibanda.

Nikakaa nae sebuleni. Kibanda akaliweka gazeti la Mwananchi mezani. Kisha akatamka;

" Braza niko na Muhingo tunaomba uanze kutuandikia makala kwenye gazeti hilo tunaloliongoza."

Nilimkubalia Kibanda na hazikupita siku mbili akanikutanisha na Muhingo Rweyemamu pale kwenye ofisi zao, Jengo la CCM Kariakoo.

Muhingo alinichangamkia sana na akaniahidi ushirikiano. Tangu hapo tukaanza kufahamiana zaidi.

Nakumbuka mwaka 2003 nilipata bahati ya kupanda basi moja na Muhingo kuanzia Ubungo kwenda Iringa. Ni basi la Scandinavia. Naweza kabisa kusema, kwenye safari ile ndipo niliweza kumfahamu zaidi Muhingo.

Safari ile ya saa tisa barabarani ilikuwa darasa kubwa na muhimu kwangu. Wakati huo nilikuja likizo nikitokea Sweden. Muhingo aliweza kunieleza mengi anayoyaona na anavyoyatafsiri kupitia uandishi. Muhingo alionyesha kuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya nchi hii hata yale yasioandikwa magazetini.

Mahali fulani kwenye mazungumzo yetu tukaingia kwenye mgogoro wa DR Congo. Muhingo tena akaonyesha alivyo na uelewa mpana wa Nchi za Maziwa Makuu na migogoro yake.

Mathalan, alinisimulia safari yake ya kiuandishi kupitia Rwanda hadi Goma akiwa nyuma ya vikosi vya Laurent Kabila. Alinieleza jinsi askari wale walivyowafuata milimani wanajeshi wa Maimai. Milio ya bunduki na mabomu ilikuwa ni kitu cha kawaida na akazoea. Akanithibitishia pia kuwa askari wa Kagame nao waliokuwepo kwenye operesheni ile ndani ya DRC.

Tukafika Iringa kwa basi kwenye safari niliyoiona fupi sana kutokana na mazungumzo yangu na Muhingo.

Jioni ile nikiwa Iringa, Muhingo aliyekuwa, wakati huo, Mwanafunzi wa Tumaini University, alihakikisha nafika anakoishi pale maeneo ya Semtema.

Nilipofika Semtema, kwenye nyumba ndogo aliyokuwa akiishi Muhingo, aliishi pia ndugu yangu Assah Mwambene. Naye alikuwa mwanafunzi wa Tumaini University.

Mazungumzo yaliendelea tukiwa watatu kwenye familia ya habari.
Chakula kikapikwa, tukala. Tukaendelea na mazungumzo kuhusu masuala mbali mbali ikiwamo media na demokrasia. Tuliongea hadi usiku mwingi.

Kesho yake Muhingo alinialika kutembelea Tumaini University. Nilipofika Chuoni ndipo nilipoona namna Muhingo alivyoheshimika kuanzia kwa wanafunzi wenzake hadi wahadhiri wa chuo.

Muhingo alikuwa Waziri wa Habari na Utangazaji kwenye Serikali ya Wanafunzi. Kwa nafasi yake hiyo alinitembeza kila idara kunionyesha.

Muhingo akaendelea kuwa kaka yangu tuliyeheshimiana na kushirikiana. Kila nilipofika Habari Corporation akiwa Mhariri Mtendaji, Muhingo akioniona naongea na wanafamilia wengine chumba cha habari alikuwa akiniambia;

" Maggid, ukimaliza usiondoke bila kupanda juu ofisini kwangu tuongee."

Akiwa DC Handeni, nilikutana nae pale Chalinze kwenye mgahawa wa Kituo Cha Mafuta cha Kobil. Aliponiona alifurahi sana. Alinitambulisha kwa Mkurugenzi wake wa Halmshauri na kunikaribisha nifike Handeni nikaoene shughuli zinazofanyika huko na kushauri inapowezekana. Alinisisitiza. Bahati mbaya sikuweza kufika Handeni.

Akiwa DC Makete, Muhingo nilikutana nae kwenye Jengo la Akiba ( NSSF) Iringa.

Aliponiona alifurahi sana. Akanitamkia kama alichonitamkia Chalinze. Bahati mbaya tena sikuweza kufika Makete.

Kaka yangu Muhingo umeondoka nikiwa na mengi niliyojifunza kutoka kwako kupitia media.

Nasikitika pia , sikuweza kukuona na kujifunza kutoka kwako kupitia Utumishi wa Umma kama kiongozi wa Serikali.

Kaka yangu Muhingo Rweyemamu, umeondoka nikiwa na hamu ya siku moja kukaa na wewe tukarejea mazungumzo yetu ya kwenye basi lile la Scandinavia kutoka Dar kwenda Iringa. Kufanya tathmini ya nini kimetokea na nini tafsiri yake.

Nitakukumbuka.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
Desturi zetu zinakataza kumsema vibaya marehemu lakini sifa hizi anazomwagiwa Muhingo baada ya kufariki haziondoi ukweli kuhusu uhuni aliofanya yeye na akina Salva Rweyemamu, Gideon Shoo na wengineo kumhujumu kila waliyemwona tishio kwa mgombea Jakaya Kikwete kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Muhingo anaingia kaburini na dhambi ya kumchulia Dokta Salim uongo mbaya kabisa ikiwa ni pamoja na kuchakachua picha iliyodai Salim ni mwana-Hizbu.Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimarondo

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Messages
259
Points
250

Kimarondo

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2017
259 250
Naikumbuka nakala yake kwenye gazeti la rai"raisi wangu kikwete wananchi wanasema hivi" alitiririka kwa data na hoja pevu sana.huyu alikuwa mwalimu wangu kwenye maswala mengi sana .
R.I.P kaka muhingo
 
Ibambasi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2007
Messages
8,190
Points
2,000

Ibambasi

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2007
8,190 2,000

Hata kama Ni kuandika obituary ndugu hapa umechemka Na ukochukulia experience yako katika uandishi
 
Ibambasi

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2007
Messages
8,190
Points
2,000

Ibambasi

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2007
8,190 2,000
Desturi zetu zinakataza kumsema vibaya marehemu lakini sifa hizi anazomwagiwa Muhingo baada ya kufariki haziondoi ukweli kuhusu uhuni aliofanya yeye na akina Salva Rweyemamu, Gideon Shoo na wengineo kumhujumu kila waliyemwona tishio kwa mgombea Jakaya Kikwete kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Muhingo anaingia kaburini na dhambi ya kumchulia Dokta Salim uongo mbaya kabisa ikiwa ni pamoja na kuchakachua picha iliyodai Salim ni mwana-Hizbu.Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa alikuwa katika ike team iliyomfanya vibaya sana Dr. Salim. Basi tu
 
Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
4,756
Points
2,000

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
4,756 2,000
Huyu bwana kipindi anaandikia gazeti la Rai kwenye utawala wa Mkapa alikuwa very objective na aliikosoa sana serikali, lkn kwa kushawishiwa, nafikiri na Salva Rweyemamu, ndio waliyompigia Kikwete debe kwa gharama ya kuwaponda wengine kama akina Salim.

Nafikiri malipo aliyopata kama fadhila kwa hilo ndo akatunukiwa u-DC kule Handeni na Kikwete.

Mengine yote sasa tunamuachia Mungu ndiye hakimu wa kweli ila waliyomfanyia Salim kwa tamaa za kidunia, haikuwa haki kabisa kwani vyote vya hapa duniani vinapita tu.
 
Forum statistics

Threads 1,381,515
Members 526,130
Posts 33,803,047
Top