Muhimu: Usafiri wa Wagombea wetu ni Salama?

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,488
86,004
Greetings,

Nimetafakari kwa kirefu suala hili na nikaguswa zaidi na kutoweka ghafla kwa rafiki yangu. Nimeona ni vyema sana tukumbushane haya kwa Wagombea wa vyama vyote.

Moja, hakikisha Usafiri unaotumia uko kwenye hali stahili na kama ni ndege basi imepitishwa kwenye viwango vyote stahili. Ni hatari kutumia chombo ambacho chaweza kuleta hasara ya Mali na maisha kwa ujumla.
Pili, wapi umefanyia service na check up ya Usafiri wako? katika kipindi hiki ni vyema kuwa na sehemu ambayo unaiamini wewe binafsi na kama utaweza hakikisha unakagua vitu minor mara baada ya Usafiri wako kutoka garage kwenye service. Epuka kuamini mtu yeyote kwenye matengenezo ya gari yako.

Unalaza wapi Usafiri wako? Usalama ukoje? je FUNGUO za.gari hubaki nazo nani? Je asubuhi unapochukua gari unaikagua? Break ziko okay? Nati za tairi hazijalegezwa?

Mipira ya gari imezeeka kiasi gani? Hapa sizungumzii uwepo wa kashata nzuri bali muda wa matumizi ambao mara nyingi huandikwa hivi 4310 (huu ni mfano tu) ukimaanisha kuwa tairi hii imetengenezwa week ya 43 ya mwaka 2010. Kwa maana hio mipira kama hii haifai kwa safari lazima ubadilishe.

Nne, dereva wako ni nani? Mna uhusiano gani? Umekaa nae kwa muda gani? Ana uelewa kiasi gani na barabara za jimboni kwako? Usichukue mtu kwakua ni rafiki yako, ni ndugu yako, n.k. Hakikisha unajiridhisha na majibu ya Maswali yote hapo juu. Huku ukizingatia itikadi yake thabiti ya chama.

Tano, ukienda kwenye kampeni na ukarudi salama, hakikisha unaikagua gari yako kwa msaada wa fundi na dereva. Usimuachie peke yake.

Sita, hakikisha hakutokei influence yeyote ya kubadilisha gari tofauti na lile ulilolichagua hadi pale inapobidi tu na.hili linaenda sambamba na kubadilisha dereva ghafla. Hata akiwa dereva unaemfahamu kiasi kikubwa naomba sana usimkabidhi gari yako akuendeshe. Ni heri ukaendesha mwenyewe au ukodi Taxi.

Saba, hakikisha unabeba watu ambao ni walengwa tu kwenye msafara wako, kwa mfano, hakikisha unakua uko wewe, dereva na watu ambao unawafahamu kwa "uziada " unaostahili. Namaanisha kuwa ikibidi Uwe na taarifa za ziada za abiria wako.

Nane, hakikisha unawasiliana na watu wako wa karibu sana kila wakati hasa wana familia yako, kwa mfano, waweza kuwajulisha hata kwa text sms tu kuwa tumefika kwenye mkutano, tumemaliza mkutano, tunaondoka eneo la mkutano, nipo na fulani na fulani, tunaelekea sehemu fulani, tunatarajia kufika sehemu fulani baada ya muda fulani. Ni info rahisi sana lakini zenye maana sana kama mambo yataharibika.

Mwisho, kila mara hakikisha kusoma mood ya watu wako wanaokuzunguka, walioko jirani yako, na jifunze kunasa na kuzisoma sura ngeni zinazojaribu kujisogeza karibu na wewe ili waombe lift au wajenge tu ukaribu ambao unautilia shaka. Epuka kukutana na watu usiwajua vizuri mahali pa faragha kwa namna yeyote iwayo.

Mungu awabariki tumalize kampeni zetu salama na Tanzania iwe moja tena.
 
Laiti kama Mchungaji Mtikila, Deo Filikunjombe, na wale Wagombea wengine wangepata muda wakapitia uzi huu, pengine nasema pengine leo tusiongekua na haja ya kuwabatiza majina mengine!
 
Mgosi hapo huyu jamaa anataka kumaanisha nini? Huu uzee nao unakuja kasi ndugu zangu bado kidogo tuu nami nitasema Rais Obama ni wa China. Au alikuwa anamzungumzia mzee wa HighCourt?
Mpwa nafufua makaburi kidogo leo
 
Back
Top Bottom