Muhimu: Kingunge, Nape na Kikwete

Muhimu: Kingunge, Nape na Kikwete

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2009
Posts
1,093
Reaction score
1,737
KINGUNGE NA KIKWETE: Tujikumbushe

Nilikuwa Dodoma mwaka 2005 wakati wa vikao vya kuteuamgombea urais kwa CCM.
Mzee Mkapa aliingia Dodoma saa saba mchana. Alipokelewa uwanjani katikati ya mvutano mkubwa wa wagombea. Dodoma ilikuwa inazizima nyuma ya Jakaya Kikwete.

Na Mzee Mkapa aliingia Dodoma akiwa amepania kulikata jina la Kikwete kwa kile alichodai, "Kijana huyu ana kiburi, anawezaje kudai akikatwa CCM itapasuka?". Mkapa alipania kulikata jina lake na kama CCM inapasuka ipasuke.

Alipoingia White House Dodoma aliendewa na wazee wakiongozwa na Mzee Kingunge. Bila kupepesa macho, Mzee Kingunge alimwambia Mzee Mkapa maneno mazito. Alisema, mgombea ni Jakaya. Aliongeza kuwa, Zamu kati ya Wazanzibari na Wabara haina shida tena, Wazanzibari wanamkubali Jakaya. Zamu za Wakristo na Waislamu; sasa ni zamu ya Waislamu na wamesema wanamtaka Jakaya.

Mzee Mkapa hakujibu. Aliondoka kwenda kupata taarifa za usalama na kamati ya maadili. Yaliyotokea baadaye wote mnakumbuka. Hotuba ya Mkapa ilibadilika. Aliokuwa ameishawaambia kuwa atakata jina la Jakaya walibaki midomo wazi. Wengine wakadai amerogwa. Wengine wakasema ametishwa, na mengine mengi.

Sasa nimwulize Nape Nnauye: Huyu Mzee Kingunge mwaka 2005 alipomuunga mkono mgombea mmoja, Jakaya, hakukigawa chama? Kumuunga mkono Lowassa ndipo amekigawa chama?

Uungwana ni kukubali ukweli kuwa kuondoka kwa mzee Kingunge ni pigo, kisha tuendelee na safari.
 
Hivi kuna MtanZania ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake wa kuchagua chama fulani kwa sababu Kingunge ameamua kukiunga au kutokukiunga mkono chama fulani?

Hivi Wananchi wa Mikoa ya Mz, Shy, Kagera, Kigoma, Mb, Ir hata wanajua Kingunge ni nani?
 
Wananchi kwenye hiyo mikoa waliona kwenye tv jana na wamesoma kwenye magazeti leo kuwa kingunge kasema ccm imebinafsishwa
 
Na hapo ndipo ukawa mnapochemka kama alivyo Kiongozi wenu fisadi Lowasa mmepoteza uhalisia na hamjui nini kinaendelea!
Hivi ni asilimia ngapi ya Watz wanaweza kuangalia TV na kujua nini kinaendelea? kwa kukusaidia tu, wenye Umeme TZ nzima ni asilimia 14% tu na hiyo ni pamoja na wakazi wa Dar!
 
Nape anajidanganya sana. Yeye bado mchanga lakini yuko busy kujikusanyia maadui. Nafasi aliyonayo ingeweza kumsaidia zaidi kujenga mahusiano, kama akiba muhimu ya baadae. Siku akikwama abaki na angalau wa kumfuta machozi.
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Hivi kuna MtanZania ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake wa kuchagua chama fulani kwa sababu Kingunge ameamua kukiunga au kutokukiunga mkono chama fulani?

Hivi Wananchi wa Mikoa ya Mz, Shy, Kagera, Kigoma, Mb, Ir hata wanajua Kingunge ni nani?
Kwetu simiyu hata hatumjua sijui huyu kinguke ni mti gani.
 
Na hapo ndipo ukawa mnapochemka kama alivyo Kiongozi wenu fisadi Lowasa mmepoteza uhalisia na hamjui nini kinaendelea!
Hivi ni asilimia ngapi ya Watz wanaweza kuangalia TV na kujua nini kinaendelea? kwa kukusaidia tu, wenye Umeme TZ nzima ni asilimia 14% tu na hiyo ni pamoja na wakazi wa Dar!

Hapo sasa ndio umekubali ccm haijafanya kitu na inatakiwa kupumzishwa. Kwanini wenye umeme wawe 14% tu????why wasiwe kwenye 70%
 
Nape anajidanganya sana. Yeye bado mchanga lakini yuko busy kujikusanyia maadui. Nafasi aliyonayo ingeweza kumsaidia zaidi kujenga mahusiano, kama akiba muhimu ya baadae. Siku akikwama abaki na angalau wa kumfuta machozi.
Unawezaje kujenga mahusiano na fisadi na kingunge na Lowasa majitu majizi hata paka afadhari.
 
Hapo sasa ndio umekubali ccm haijafanya kitu na inatakiwa kupumzishwa. Kwanini wenye umeme wawe 14% tu????why wasiwe kwenye 70%

Uko nje ya Mada, unaweza kuanzisha hiyo mada kama ukipenda na tukakutana huko!
 
Hivi kuna MtanZania ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake wa kuchagua chama fulani kwa sababu Kingunge ameamua kukiunga au kutokukiunga mkono chama fulani?

Hivi Wananchi wa Mikoa ya Mz, Shy, Kagera, Kigoma, Mb, Ir hata wanajua Kingunge ni nani?

Wananchi wa mikoa uliotaja wanaweza kuwa hawamjui Mzee Kingunge, lakini wana CCM wa kweli ambao ni sehemu ya wananchi wanafahamu Kingunge ni nani.
 
Unawezaje kujenga mahusiano na fisadi na kingunge na Lowasa majitu majizi hata paka afadhari.

Itamsaidia sana kama ataacha kulipuka na kuropokea hata waliomlea baba yake. Kama unampenda usimdanganye
 
Na hapo ndipo ukawa mnapochemka kama alivyo Kiongozi wenu fisadi Lowasa mmepoteza uhalisia na hamjui nini kinaendelea!
Hivi ni asilimia ngapi ya Watz wanaweza kuangalia TV na kujua nini kinaendelea? kwa kukusaidia tu, wenye Umeme TZ nzima ni asilimia 14% tu na hiyo ni pamoja na wakazi wa Dar!

Hapa CCM ndiyo mnakuwa kama nyumbu kumbe unajua watanzania wanakosa umeme na walio nao ni 14% nani kasababisha umaskini kama siyo serikali isiyowajibika na zembe kama yetu. Nyie muda mwingine muone haya Nchi mumeifirisi mpaka ni maututi sasa unasema 14% ndiyo wanapata umeme mpake leo tuko gizani miaka 50 ya kujitawala mnatupa hasara alafu eti CCM, kafie mbele nyie nuksi na balaa katika Nchi hii tumewachoka hata sasa mgengali ondoka tu!
 
Huyu Nape ni mropokaji tu. Nakumbuka baada ya kuchaguliwa mwaka 2005, kuna kikao alizungumzia jinsi alivyolelewa ndani ya chama na kumtaja Mzee Kingunge km mmoja wa watu waliomlea JMK, Na ikumbukwe kuwa kwenye baraza lake la kwanza la mawaziri alimteua Kingunge kuwa waziri km shukrani. Ss iweje Nape amkebehi kiasi hicho?
 
Wakati wa kingunge , Nyerere na kawawa, haya mambo ya ujana uliopitiliza hayakuwepo
12122487_727046454092009_3942719311512115876_n.jpg
 
Na hapo ndipo ukawa mnapochemka kama alivyo Kiongozi wenu fisadi Lowasa mmepoteza uhalisia na hamjui nini kinaendelea!
Hivi ni asilimia ngapi ya Watz wanaweza kuangalia TV na kujua nini kinaendelea? kwa kukusaidia tu, wenye Umeme TZ nzima ni asilimia 14% tu na hiyo ni pamoja na wakazi wa Dar!

CCM wote wasafi bila shaka,
Mabadiliko lazima
 
Hivi kuna MtanZania ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake wa kuchagua chama fulani kwa sababu Kingunge ameamua kukiunga au kutokukiunga mkono chama fulani?

Hivi Wananchi wa Mikoa ya Mz, Shy, Kagera, Kigoma, Mb, Ir hata wanajua Kingunge ni nani?
Yaani kuna watu akili zao sijui zikoje! hivi bado wanadhani kuna mtu anaweza kuchagua Ukawa eti kwa sababu kahamia Kingunge!!!!
Kura yangu ni kwa Makufuli tu, hata iwaje!!!
 
Hivi kuna MtanZania ambaye anaweza kubadilisha uamuzi wake wa kuchagua chama fulani kwa sababu Kingunge ameamua kukiunga au kutokukiunga mkono chama fulani?

Hivi Wananchi wa Mikoa ya Mz, Shy, Kagera, Kigoma, Mb, Ir hata wanajua Kingunge ni nani?
jibu ni ndio
 
Back
Top Bottom