Muhimu: Busara Yahitajika Suala la Maxence Melo

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,251
2,000
Wasalaam,

Nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa uzima afya ya mwili na akili pia licha ya changamoto za hapa na pale .....

Pili nimuombe aendelee kuwapa moyo wa subira familia ya ndg Maxence Melo ....

Wengi wetu kama si wote twatambua kuwa Mkurugenzi wa kampuni ya JAMII MEDIA inayoendesha tovuti maarufu ya JAMII FORUMS ndg Maxence Melo anashikiliwa na vyombo vya dola na tayari kesi iko mahakamani ....

Miongoni mwa makosa ikiwa ni kushindwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi lilipokuwa linafanya uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyochapishwa kielektroniki kwenye tovuti hiyo .... kulingana na Sheria ya Makosa ya Mtandao ( (Ciber Crime Act)


Muhimu:- Suala hili tayari liko mahakamani hivyo BUSARA na HEKIMA zahitajika sana tunapolijadiri humu jukwaani ama tunapotoa CRITICISM zetu juu ya serikali na viongozi wake hasa wa ngazi za juu .....

Tuutumie uhuru wetu wa kutoa maoni and any critical ideas we have lakini tukiwa twajiepusha na lugha tata (offensive language) maana tuitumiapo lugha hiyo iliyo kali kwanza twazidi kumweka Mkurugenzi wetu katika mazingira tata zaidi maana jf ni tovuti iliyo katika umiliki na usimamizi wake .... pili yaweza pelekea maamuzi ya karipio ama kufungwa kwa tovuti ....

Swali: Je kama tovuti ikifungwa tutaweza vp kufikisha critical ideas zetu?

Najua watapatikana ambao watabeza maoni yangu na hata kutukana but huo ni mtazamo niloona tushirikishane ....

Good morning
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom