Muhimbili yakauka vifaa vya tiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili yakauka vifaa vya tiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dr Klinton, Feb 27, 2012.

 1. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hali MUH2 ni mbaya kwani kwa muda wa wiki 2 sasa theater gowns zimeadimika kwani machine ya kufulia nguo imekosa lubricant muhimu hadi leo Hii
  oxygen nayo imeadimika haileweki ni lini itapatikana hivyo ndugu zanguni mnaoweza kwenda aga khan regency na kwingineko msijaribu kuja muh2 kwa muda huu...
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rais kawapuuza, miye nasubiria mgomo huu unaokuja maana hapo ndio watetezi wa serikali watakapogundua kuwa madaktari walikuwa na hoja na bado wanahoja na ndio maana signature yangu haibadiliki bado! Kikwete amewapuuzia kabisa madaktari na sasa wakiitisha mgomo mkubwa zaidi ndio Watanzania wajua kuwa sera za CCM kwenye sekta ya afya zimeshindwa.
   
 3. m

  mashambani kwao JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  samahani mwanakijiji ile kamati imepotelea wapi?
   
 4. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Mungu atunusuru! Hakuna kitu kibaya kama mtu mzima mnamueleza matatizo halafu badala ya kuyasolve anayapuuza!!Hivi huu moto wa madaktari ukiwaka tena utazimwa na nani?
  Tutawaleta kina K . Anan kuja kusuluhisha?
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  MM, hamna hata sera moja ya CCM iliyofanikiwa.
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Gharama alizotumia JK alipokuwa Uingereza kwa Cameron na Botwana zingetosha kabisa kununua lubricants na Oxygen ya kutumia mwaka mzima. Tatizo ni kuwa nchi haina vipaumbele na mambo yanaenda ovyo hovyo. After all wao hawatibiwi humu nchini kwa hiyo haiwahusu sana
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  walipumzika mpaka trh 3/3. Baada ya hapo ndo wataanza kazi yao. Waliiacha kamati aliyounda pinda ili isijitetee kwamba wamewaingilia kwenye utendaji wao.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyingi zimejaribiwa na zinaendelea kujaribiwa lakini bado sijafanikiwa kuona iliyojaribiwa ikafanikiwa - quote me.
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  tarehe tatu sio mbali!
   
 10. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  Nasikia pia kuna mgomo mkubwa zaidi unakuja! Serikali wataleta tena propaganda ila this tyme hawatafanikiwa! Jambo litazua jambo!
   
 11. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kamati ilisema itaanza mikutano ya tathimini kuanzia tarehe tatu mwezi wa tatu.subiri mkuu
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimeangalia kwa siku hizi zote kuona kama wale waliokuwa wanaitetea serikali watakuwa wa kwanza kuipigia kelele ili itimize madai ya madaktari kuepusha mgongano mwingine ujao.. but kimya..
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wabunge wanaotishia kujiuzulu wafanye hivyo haraka [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 27 February 2012 19:46 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]SIKU nzima ya jana ilitawaliwa na gumzo katika redio na vyombo vingine vya habari vya hapa nchini, kutokana na kauli iliyotolewa juzi na Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba kutopandishwa kwa viwango vipya vya posho za vikao kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh230,000 kwa kila kikao kumesababisha nusu ya wabunge kutishia kujiuzulu kwa madai ya hali ngumu ya maisha inayowakabili.

  Akiwahutubia wananchi mwishoni mwa wiki katika Jimbo la Njombe Kusini ambalo analiwakilisha bungeni, kiongozi huyo alisema wabunge hao wamemwendea wakitaka kuacha ubunge lakini aliwakatalia kwa kuhofia gharama kubwa za kufanya chaguzi ndogo katika majimbo watakayotoka. Spika huyo alisema wabunge hao wamechoka kabisa na kwamba hawakujua kwamba kuacha taaluma zao na kuwa wabunge kungewatia umaskini.

  Kauli yake hiyo ambayo ilikuwa inarudiwa mara kwa mara jana katika vipindi vya redio za hapa nchini wakati wananchi walipokuwa wakijadili tishio hilo la wabunge, iliibua hisia kali kutoka kwa wananchi ambao walisema wabunge wa namna hiyo hawafai na kumtaka Spika awaache waondoke kwa kusema ni wabunge maslahi.

  Katika hotuba hiyo, Spika Makinda alisema miaka 10 kuanzia sasa, mtu mwenye taaluma yake hatagombea ubunge kwa sababu ni eneo la umaskini wa kutupwa. Alisema wabunge wa Kenya wanawacheka wenzao wa Tanzania kwa kushindwa kujipitishia fedha zinazoendana na kazi wanayoifanya, huku akisahau kwamba amani, umoja na mshikamano wetu umetokana na sera zinazojenga usawa.

  Tumeshangazwa sana na kauli hiyo ambayo hakika imelipa Bunge taswira mbaya ya umamluki wa posho. Tangu posho hizo zisitishwe wiki kadhaa zilizopita baada ya wananchi wengi kuzipinga, wabunge wengi wamejitokeza hadharani na kuzitetea kwa kusema maisha yao yamekuwa magumu, hasa wawapo bungeni mjini Dodoma ambapo wanadai gharama za maisha ni kubwa mno kuliko sehemu nyingine nchini.

  Wabunge hao, akiwamo Spika wamekuwa wakitoa sababu zisizo na mashiko ilihali wahalalishe posho hizo. Spika alikaririwa na vyombo vya habari akisema hivi karibuni kuwa, wabunge wanakatwa fedha nyingi kutokana na mikopo ya benki na kwamba fedha zinazobaki haziwezi kuwakimu muda wote wawapo Dodoma kwenye vikao vya Bunge. Spika anasahau ukweli kwamba mikopo hiyo siyo ya lazima ambayo mara nyingi imechukuliwa na wabunge kufanya matanuzi tu.

  Tunachoweza kusema hapa ni kwamba kauli ya Spika kuhusu tishio la kujiuzulu kwa nusu ya wabunge kwa madai ya ukata imetufungua macho kwa kuelewa aina ya wabunge tuliowapeleka bungeni. Sasa tumeelewa kwamba baadhi ya wabunge waliomba kura siyo kwa lengo la kutaka kutatua matatizo ya wananchi, bali kwa maslahi binafsi. Vinginevyo, haiingii akilini kusikia mbunge akisema bila kumung'unya maneno kwamba laiti angejua ubunge hauna fedha nyingi asingeacha taaluma yake kuganga njaa bungeni.

  Tunapata shida kuwaelewa wabunge wanaodhani bungeni ni mahali pa kuchumia matumbo au kupata ukwasi. Tulidhani kelele za wananchi dhidi ya ongezeko la posho za vikao zilitosha kuwaamsha wabunge watambue kwamba posho hizo za vikao siyo tu zilikuwa nyingi, bali pia zilikuwa ni wizi wa mchana kweupe kutokana na malipo hayo kufanyika kwa kazi ambayo tayari wamelipwa kuifanya kupitia mishahara yao.

  Ni kichekesho cha mwaka Spika anaposema wabunge wa Kenya wanawacheka kwa kutojiidhinishia fedha nyingi wakati ndio wanaopitisha bajeti ya serikali, wakati akijua fedha wanazojilipa wenzao wa Kenya zilipingwa sana na wananchi lakini hawakusikilizwa. Hapa nyumbani serikali yetu ni sikivu na ndiyo maana Rais Jakaya Kikwete alisitisha posho hizo baada ya wananchi kusema hapana.

  Sisi tunasema wabunge wanaotishia kujiuzulu eti kwa kutiwa umaskini na ubunge waachwe waachie ngazi haraka na wasibembelezwe kwa kauli kwamba wakijiuzulu nchi yetu itapata gharama za kufanya chaguzi ndogo. Tunasema litakuwa jambo la kheri iwapo wabunge maslahi wataondoka ili tuwapate wengine wenye dhamira na moyo wa kuwatumikia wananchi. Tunawataka wabunge wenye ujasiri wa kujiuzulu wafanye hivyo sasa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 14. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #14
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Waliosababisha mgomo wa madaktari sasa kuburutwa kortini [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 27 February 2012 19:45 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Geofrey Nyangóro
  WANAHARAKATI nchini wamejipanga tayari kwa kufungua kesi dhidi ya watu wote waliosababisha mgomo wa madakatari uliosababisha watu baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha na wengine kuathirika.
  Habari hizo zinakuja wakati zikiwa zimebakia siku tano kwa madakatari kukutana na kufanya tathimini kuhusu utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati yao na Serikali katika hatua za kumaliza mgomo huo wa hivi karibuni.

  Akiuzngumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Hellen Kijo –Simba, alisema hatua hiyo itakuja baada ya kukalimika kwa mchakato wa uchambuzi wa madhara yaliyotokana na mgomo huo uliodumu wa zaidi ya wiki mbili.
  "Sisi wanaharakati wa haki za binadamu kwa kuzingatia matukio, maamuzi na matokeo yaliyojiri kwa kipindi cha wiki mbili tangu kusitishwa kwa mgomo wa madaktari nchini, tumebaini kuwa madaktari wamerudi kutoa huduma kama kawaida."alisema Bisimba.

  Alisema hata hivyo wamegundua kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya hawajawajibika na kujutia vifo na madhara waliyoyasababisha kwa wananchi kutokana na uzembe na kushindwa kwao kutekeleza wajibu.

  "Tunamtaka Rais Kikwete awafukuze kazi mara moja"alisema Bisimba ambaye pia aliishutumu Serikali kuwa imeshindwa kutekeleza mambo manne yaliyotolewa na wanaharakati katika tamko lao.

  Alisema pamoja na mambo mengine, wanaharakati walimtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kutoa taarifa kwa umma kuhusu athari zilizotokana na mgomo huo."Tuliitaka Serikali itoe taarifa kwa umma kuhusu athari zilizotokana na mgomo, lakini hadi sasa haijatekeleza," alisema.

  Alitaja jambo lingine kuwa ni pamoja na kkuwataka Spika wa Bunge Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai, waombe radhi kufuatia kitendo chao cha kuzima hoja zilizowasilisha bungeni za kutaka mgomo wa madaktari ujadiliwe.

  "Tunataka mamlaka zote nchini zitambue ziheshimu na kuwajibika kwa wananchi. Lakini pia tunataka umma wa Watanzania kuamuka na kuunga mkono harakati za kuikumbusha Serikali kuwajibika," alisisitiza mkurugenzi huyo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #15
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Source Mwananchi 27/02/2012

   
Loading...