Muhimbili yafungwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
08 FEBRUARY 2012



*Huduma zote zasitishwa hadi kitakapoeleweka
*Tamko la serikali lasubiriwa kuokoa jahazi
*Wizara yahaa kutafuta madaktari wa ziada

Na Waandishi Wetu Majira


Vitanda vya wagonjwa vikiwa tupu kufuatia mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendela katika Hospitari ya Taifa ya Muhimbili (MNH), madaktari bingwa na wauguzi wa hospitari hiyo wameungana katika mgomo huo kuanzia juzi, Dar es Salaam jana. (Picha na Michael Machellah)


HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MHN) imetangaza rasmi kusitisha utoaji wa tiba baada ya kuathiriwa na mgomo hadi hapo Serikali itakapotoa tamko rasmi kuhusu muafaka wake na madaktari.

Uamuzi wa hospitali hiyo kubwa kuliko zote nchini kusitisha kutoa huduma ulitangazwa Dar es Salaam jana na Ofisa Habari wa MNH Bw. Aminieli Aligaesha, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema huduma hizo zimesitishwa kuanzia juzi kutokana na kamati ya madaktari bingwa kuandikia uongozi kwa MNH,Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi ya Tiba (MUHAS) kusitisha utoaji wa huduma zote zinazotolewa na hospitali hiyo.

Kwa msingi huo alisema huduma zitaendelea baada ya muafaka kupatikana.

Alisema kuwa wagonjwa walioko wodini wataendelea kuonwa na madaktari wachache waliojitolea, na wakuu wa idara waliopo hospitali hapo, ambapo madaktari wa JWTZ wataendelea kuona wagonjwa wa dharura.

Alisema kwa takwimu walizonazo kuanzi usiku wa juzi na jana asubuhi wapo wagonjwa 811 waliolazwa wodini na wanaendelea kupatiwa matibabu.

Hata hivyo alisema hali hospitalini hairidhisi kutokana na huduma kuendelea kudorora kila wodi, huku vitengo vingine vikiwa hakuna huduma hata moja inayoendelea.

Waandishi wa habari walipotembelea jengo la watoto walibaini hakuna huduma zozote zinazoendelea katika wodi hizo.

Akizungumza katika wodi hiyo Bi. Adela Shomari alisema kuwa tangu afike hospitali hapo mtoto wake hajapatiwa matibabu kwani licha ya kuwa anahitaji kufanyiwa upasuaji.

"Tangu nifike hospitali hapo kutoka Shinyanga mtoto wangu hajapatiwa matibabu zaidi ya kupewa vidonge vya kuongeza damu na panado," alisema.

Naye Saida Kassimu ambaye anamuuguza mtoto anayeumwa ugonjwa wa ngozi alianza kutokwa machozi baada ya waandishi wa habari kufika kwenye kitanda chake na kuanza kusimulia hali iliyopo hospitalini hapo.

"Roho inaniuma, nalia kwa uchungu nikiona mwanangu akiteseka, sina amani kwani leo ni siku ya tano tangu nilipofika hospitali hapo sijawahi kuonwa na daktari," alisema.

Habari ambazo gazeti hili lilipata ni kuwa Waziri wa Afya na ustawi wa jamii,Dkt. Haji Mponda,Naibu waziri Dkt. Lucy Nkya, Katibu Mkuu Bi Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Bw. Deogratasia Mtasiwa, jana usiku walitembelea hospitali hiyo saa sita usiku wa kuamkia jama ili kujionea hali ilivyo.

Wakati huo huo viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutwa nzima ya jana walishinda wakihaha kwa lengo la kutafuta madaktari wa kupeleka Muhimbili ili kuokoa jahazi.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana Ofisa Habari, Bw. Nsachris Mwamwaja alisema jana walikuwa wakitafuta madaktari wa kwenda kutoa huduma kwa baadhi ya wodi.

"Juzi kilikaa kikao na kuchukulia suala hilo kama dharura, hivyo iliamuliwa wachukuliwe madaktari wa wizara na kupelekwa Muhimbili," alisema na kuongeza;

"Jana tumehangaika huku na kule kutafuta madaktari hao, lakini hadi muda huu sina uhakika wamepatikana wangapi."

Alisema madaktari hao si mbadala wa tatizo, lakini watakuwa wanatoa msaada kwa zile kazi zilizopo hospitali hapo ambazo zimeachwa kabisa wakati ufumbuzi wa mgogoro huo ukiendelea.

"Sasa hivi tupo tunahangaika ili kuona ni jinsi gani tunaweza kupunguza idadi ya vifo," alisema. Wakati hayo yakiendelea suala hilo liliibuka bungeni jana mjini Dodoma baada ya Mbunge Godfrey Dhambi, kuomba mwongozo kwa Spika Bi Anna Makinda, akitaka kusitishwa kwa kikao cha bunge ili kujadili mstakabari wa madaktari.

Lakini mwongozo huo ulipingwa na Spika Makinda kwa maelezo kuwa suala hilo lipo katika kamati maalumu, hivyo ni vema kusubiri majibu kutoka kwa kamati hiyo.

Kutokana na kusitishwa lwa huduma katika hospitali hiyo, baadhi ya wadau wamesema ni lazima serikali itambue kuwa wananchi wanapoteza maisha, hivyo suala hilo linahitaji ufumbuzi wa haraka.

Mtanzania aliyeishi Ufaransa, Bw. Mohamed alisema Serikali imeshindwa kuonesha utu kwa kushindwa kumaliza suala hilo.

"Hili ni tatizo kubwa na hasa inapofikia hata kiongozi mkuu akashindwa kusema jambo lolote," alisema Bw. Mohamed .

Alisema viongozi wengi ni wabinafsi ndiyo maana wameshindwa kuchukua uamuzi mapema.

Naye Bw. Bw.Edgar Mwankuga alisema serikali imeshindwa kuweka maslahi ya wananchi mbele hasa katika huduma za muhimu kama sekta ya afya.

"Rais kuendelea kukaa kimya kuhusu mgogoro huo ni ishara tosha kuwa hana uchungu na sisi wananchi ambao kipato chetu hakituruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi",alisema Bw.Mwankuga

Naye Bi.Julieth Swai mkazi wa Dar es Salaam alisema watendaji wa JK wameshindwa kusuruhisha mgogoro huo kwa sababu kila kukicha hali inakuwa mbaya hasa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


 
Hivi kule wodi ya wazazi mtaa wa Kalenga na Uluguru vipi? Wale premature babies nani anawaangalia?
 
Serikali imeshindwa ni bora i privatize shughuli muhimu zinazohudumia wananchi kama Hospitali, Umeme, Maji ili ziwe zinatolewa kiufanini

Waziri Wa Fedha ni Mpya hakuwahi kufanya kazi kwenye mtandao wa kazi wa kitanzania nadhani alikuwa nje ya nchi muda wote akaitwa nyumbani akapewa ubunge na Uwaziri kwahiyo sidhani ataujua Muongozo wa Kitanzania
 
Serikali imeshindwa ni bora i privatize shughuli muhimu zinazohudumia wananchi kama Hospitali, Umeme, Maji ili ziwe zinatolewa kiufanini

Waziri Wa Fedha ni Mpya hakuwahi kufanya kazi kwenye mtandao wa kazi wa kitanzania nadhani alikuwa nje ya nchi muda wote akaitwa nyumbani akapewa ubunge na Uwaziri kwahiyo sidhani ataujua Muongozo wa Kitanzania

Waziri wa Fedha gani? Mustafa Mkulo aliyekuwa NSSF au mwingine?
 
Sasa mpaka madaktari bingwa wanagoma tuwalaumu chadema tena? Mie nawaunga mkono madaktari! Na ni kwanini rais asitoe tamko? Ukweli ni kwamba kila mtanzania anajua nchi yetu ni tajiri ila inaliwa mimtu michache yenye roho mbaya na isio na huruma!
 
Back
Top Bottom