Muhimbili: Utaratibu huu mpya ni hatari kwa maisha ya wagonjwa

sikia2017

New Member
Oct 26, 2017
1
1
Kwanza napenda kutoa pongezi za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa mabadiliko makubwa uliyoweza kuyafanya katika kipindi kifupi cha uongozi wako.

Malalamiko yangu ni kutokana na Kitendo cha kuindoa wodi ya ICU ya magonjwa ya upasuaji chini ya idara ya idara ya usingizi na kuikabidhi kwa madaktari wasiokuwa na taaluma yoyote ya upasuaji wala usingizi. Wale madaktari hawawezi hata kuweka mpira wa kumsaidia mgonjwa kupumua ukiacha uwezo wa kuwaandikia wagonjwa dawa za kulala.

Kwa sababu wale Wacuba wapo ingekuwa njia nzuri ya kuiimarisha idara ya usingizi na wagonjwa na mahututi lakini maamuzi haya yatakuwa na athari mbaya sana kwa wagonjwa pengine tutegemee vifo zaidi vya wagonjwa.Haya ni maamuzi ambayo hayana faida kwa wagonjwa. Ni vizuri utaratibu huu ukafikiriwa tena upya.

Jana (tarehe 25 october) yametokea matatizo makubwa katika wodi ile ambayo inawezekana yaligharimu maisha ya mgonjwa (utapita kwenye ile wodi kuuliza kilitokea nini kwa yule mama aliyefariki jana, nani aliyemuwekea mpira wa kupumulia, na kama alifanikiwa kuweka)

Kilichotekea Muhimbili ni maamuzi ambayo tunaweza kuyaita kama kituko. Katibu mkuu wa wizara ya afya natambua wewe una uelewa na masuala ya afya nakuomba uliangalie hili kwa jicho la pili.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom