Muhimbili: No Comments

Madaktari wakidai kuboreshwa kwa huduma bora za afya wao wanawatoa kucha na meno wawe vibogoyo
 
Mbuze Mzee niseme asante kwa kazi nzuri.
Kitu kama hiki nilitegemea madokta wangeiweka wazi siku nyingi kama sehemu ya kuwaonyesha watanzania nini hasa wanakilalamikia.

Mimi kwa maoni yangu MODS kwenye ile Forum ya masuala ya afya kama sehemu ya kuleta maboresho kuwe na sub forum mahususi kwa ajili ya kuweka Picha kama hizi.Tukifanya mambo kwa uweledi wa kuonyesha mapugufu kwa uhalisia wake itatusaidia au kusaidia wahusika na watazamaji au wasomaji kupima uzito wa matatizo tuliyonayo kama jamii.
 
Jamani "Nyota ya Kijani" ule mpango wa uzazi afadhali urudishwe.
Kwani namna hii wamama wajawazito kurudindika mawodini sio vyema.
Halafu akina baba/mama hebu basi tutafute mchezo mwingine wa usiku! Maanake Duuh
Hata kama imeandikwa "nendeni mkaijaze dunia" these are too many prenatal/postnatal women in one room!
 
Mh kwakweli hali ni mbaya sana na inasikitisha sana..
Eh mungu tunusuru
 
Hii picha nahisi ni msibani, akina mama huwa wana tabia hiyo ya kukusanyika msibani wakati wakifariji mfiwa.
 
Madaktari wakigoma watanzania wanawachukia masikini hawajui kama nikwamasilaho yao.

Hakuna kitu kibaya kama kuzoea shida maana wengi wa kinamama mnaowanona hapa hawaoni kama hilo ni tatizo. Yaani hawajawahi kukutana na huduma bora nchini. Huenda kwa upeo wa watanzania wengi masiknini hiyo ni standard ya juu ya huduma za afya
 


Hii inasemekana ni Nachingwea
Mbuzi hapa sio kwa mgaga wa kienyeji kweli? Mimi naona kama hiyo picha wako kwenye banda la nyasi na sina hakika kama tuna zahanati zenye kuezekwa kwa nyasi za umma. Niliwahi kufanya kazi Msumbiji (Gaza Province) maeneo hayo ndo niliona vitu kama hivyo. Hizo picha zinaonesha zahanati lakini kwa hadhi ya Tanzania ukiliganisga na msumbiji its too much
 

Attachments

  • HealthPost.jpg
    161 KB · Views: 113
Babu wa Samunge uko wapi utuokoe. Au na wewe ulikuwa na malengo yako baada ya kuyatimiza umetushit.
 
Niliwahi kufanya kazi Msumbiji (Gaza Province) maeneo hayo ndo niliona vitu kama hivyo. Hizo picha zinaonesha zahanati lakini kwa hadhi ya Tanzania ukiliganisga na msumbiji its too much
Tanzania is more than ten times resourceful than Mozambique
 

Thanks Mkuu for the comments
 
mkuu hii picha ni hospital ya temeke wodi ya wakina mama wajawazito ya zamani, kwa sasa inakarabatiwa na wakina mama wamehamishiwa kwenye jengo jipya kule chini kama unaeleka mochwali.

Wewe usiwe kama wale vijana waliobishana kuwa jalala liko tandale au mbagala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…