Muhimbili njiani kupata Serikali

Muhimbili njiani kupata Serikali

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Ikiwa ni takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa bila ya serikali ya wanafunzi,wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi za Tiba Muhimbili wanakaribia kupata serikali yao. Serikali ya wanafunzi chuoni hapo almaarufu kama MUHASSO ilivunjwa na kufutwa chuoni hapo tar. 20/10/2011. Tayari Katiba imekamilika ikisubiri kuidhinishwa na Baraza la Chuo hicho. Uchaguzi unatarajia kufanyika Januari au Februari mwakani.
 
Mkichagua masalia mmekwisha!! Dat is mapandikizi? Kuweni makini!!!
 
Mimi ndiye niliyewasimamia wanafunzi (Kamati ya Mapitio ya Katiba) kurekebisha Katiba hiyo 'mpya' ya MUHASSO
 
Mimi ndiye niliyewasimamia wanafunzi (Kamati ya Mapitio ya Katiba) kurekebisha Katiba hiyo 'mpya' ya MUHASSO

kumbe na we ni mmoja wa wasaliti? Unajua kwamba kuna watu walisimamishwa mwaka,miaka miwili na wengine kufukuzwa?
 
kumbe na we ni mmoja wa wasaliti? Unajua kwamba kuna watu walisimamishwa mwaka,miaka miwili na wengine kufukuzwa?
Najua Mkuu. Mimi si mwanafunzi pale. Ni Kamanda wa kwenda kumaliza mtafaruku. Kila kitu kitakuwa sawa. Kwanza wanafunzi wapate viongozi. Waliofukuzwa wameanza kurejeshwa. Mimi nilikwenda kama Mwanasheria huru
 
Lakini mkuu umefuatilia kwa nini chuo kilikuwa kinalazimisha katiba ibadilishwe huku vyuo vingine vikiwa havijabadilisha? nilikuwepo kipindi mambo yakitokota tangu kina charles, yahaya na baadaye wengine wakafukuzwa. Suruhisho siyo kupata tu serikali ambayo msemaji mkuu atakuwa dean of students. Unawafahamu madean wa siku hizi? Wengi wao wamegeuka na kuwa deans of administrations na kukandamiza wanachuo badala ya kuwa washauri wao.
 
Kutokana na taarifa nilizo nazo kuhusu haya mambo, mtazo wangu ni juwa haina maana kurudisha MUHASSO kwa sasa kwa sababu bado kuna wanafunzi wengi wako nyumbani(waliokuaa wakidai hiyo hiyo MUHASSO) irudishwe.Wengi wamekatishwa masomo.

Iwapo MUHASSO ikirudishwa, ni vizuri/vyema na busara wanafunzi hao pia warudishwe.

Why let them suffer home and accomplish what they wanted/fight for at first place?
Mkuu Kichwani-Kichwa, you real have to consider that..if nmyou already have, what can you say about it?
 
Last edited by a moderator:

Kiongozi usijali. Jambo la kwanza kuzingatia ni hilo. Kila mwanafunzi atarudishwa. Wameshaanza kurudishwa. Kila kitu kitakuwa sawa. Lakini,wapate Serikali kwanza
 
Last edited by a moderator:
Kiongozi usijali. Jambo la kwanza kuzingatia ni hilo. Kila mwanafunzi atarudishwa. Wameshaanza kurudishwa. Kila kitu kitakuwa sawa. Lakini,wapate Serikali kwanza

na waliofukuzwa je? Naomba nikuulize, ulikuwepo wakati wanahojiwa na mashitaka yao ukayaona? Umejiuliza kwa nini walishitakiwa kwa mashitaka yale yale ila adhabu zikawa tofauti ie kusimamishwa mwaka 1,miwili na wengine kufukuzwa? Kwenye hiyo commitee ya katiba kulikuwa na uwakilishi wa madarasa yote? For sure mmefanya kazi na first year mpaka third year wasiojua nini muhasso na mgogoro ulianzia wapi. Hao mmewapeleka peleka tu, siku hizi si mtu akiuliza anaambiwa we cdm na kufukuzwa chuo!
 
Loh! Mambo ya muhas bwana! Lakini si yule jamaa wa tiss ameshastaafu-? Jamaa alikuwa mbabe kama nini! Sijui kama aliyemrithi atakuwa kama yeye ila all in all wanachuo wa siku hizi hawana kash kash zozote.
 
Back
Top Bottom