ZANU-PF ni muungano wa vyama viwili vya ZANU ambacho ndio chama cha Mugabe na ndio chenye majority Shona, na PF Kilichokuwa cha Joshua Nkomo , ambacho kilikuwa na majority Ndebele, Nyerere ndio alishiriki na kuwashawishi sana waunganishe hivi vyama na kuwa chama kimoja
kugawanyika kikabila inaonekana kama sio rahisi sana kwani Ndebele wamekuwa kama wamemezwa na Washona, Wandebele wamejikita sana maeneo ya Bulawayo lakini na idadi kubwa ya Washona pia imeamia Bulawayo, kwa upande mwingine Harare na miji mingine imejaa Washona bila kuwa na idadi ya Wandebele,
hivyo ZANU PF inaweza kugawanyika lakini sio kwa misingi ya ukabila kama ulivyoeleza hapo juu