Ozzanne Issakwisa
JF-Expert Member
- Mar 7, 2016
- 288
- 240
Huyu jamaa nilidhani hawapendi wazungu tu, sasa naona 'kawachenjia' hadi marafiki zake wachina.
Uchina ndiyo mwekezaji mkuu katika sekta ya uchimbaji almasi Zimbabwe.
Kampuni ya Wachina ya Anjin Investments ni miongoni mwa kampuni zilizoathiriwa na agizo la Mugabe na imewasilisha kesi kortini kupinga agizo la Rais Mugabe.
Kiongozi huyo alisema alilalamika moja kwa moja kwa Rais Xi Jinping majuzi kuhusu Zimbabwe kutopata haki kutoka kampuni za uchimbaji madini za Uchina.

Mugabe: Kampuni za kigeni zinaiba almasi
- 4 Machi 2016
Image captionMugabe amesema Zimbabwe haifaidi kutokana na almasi
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amedai kampuni za uchimbaji madini za kigeni zinaibia taifa hilo na kutangaza kwamba nchi hiyo itatwaa umiliki wa machimbo yote ya almasi.
Bw Mugabe amedai kampuni hizo zinafanya ‘utapeli’ na biashara ya ‘magendo’ ya kusafirisha almasi nje ya nchi hiyo.
"Hatujapokea pesa zozote za maana kutoka kwa sekta ya almasi,” alisema Mugabe na kulalamika kwamba Zimbabwe imepata $2bn (£1.4bn) pekee kutoka kwa mapato ya takriban $15bn (£11bn).
Akizungumza wakati wa mahojiano katika runinga ya taifa ya ZBC TV, kiongozi huyo wa umri wa miaka 92 amekanusha kwamba hatua yake ya kutwaa umiliki wa machimbo ya madini itaathiri uhusiano kati ya nchi hiyo na Uchina.
Uchina ndiyo mwekezaji mkuu katika sekta ya uchimbaji almasi Zimbabwe.
Kampuni ya Wachina ya Anjin Investments ni miongoni mwa kampuni zilizoathiriwa na agizo la Mugabe na imewasilisha kesi kortini kupinga agizo la Rais Mugabe.
Kiongozi huyo alisema alilalamika moja kwa moja kwa Rais Xi Jinping majuzi kuhusu Zimbabwe kutopata haki kutoka kampuni za uchimbaji madini za Uchina.
Marais Mugabe na Xi Jinping awali
Zimbabwe ilikuwa ya ya nane katika uuzaji nje wa almasi mwaka 2014.
Bw Mugabe pia alishutumu baadhi ya raia wa Zimbabwe akiseza wamehusika katika wizi wa almasi.
“Wale tuliotarajia wawe macho na masikio yetu hawajaweza kutazama wala kusikia yanayofanyika,” alisema.
Chanzo: BBC Swahili