Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa yeye sio Mmarekani wala Muingereza wakati akiwahutubia karibu watu 50,000, wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika kwenye mji mkuu Harare kwa heshima yake.
"Mataifa ya magharibi na chama cha MDC-T wanataka niachie madaraka lakini najiuliza kama wana nia nzuri ya kusema hivo.
Wanataka nikapumzike au wanatishwa na utawala wangu? kawaambieni siendi popote.
Ikiwa watu wangu watanitaka kuachia madaraka, nitaachia. Lakini kwa kuwa nina nguvu za kutosha kuwahudumia, nitaendelea kuwahudumia." Alisema Mugabe
Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amekana uwezekano wowote wa kuondoka madaraklani na kuwashambulia viongozi hasimu ndani ya chama tawala cha ZANU-PAFU kwa kupanga kumrithi.
Amesema kuwa yeye anawahudumia watu wa Zimbabwe na kuwa ataondoka tu ikiwa watu wangetaka afanye hivyo. Hata hivyo amesema kuwa haondoki na haendi popote.
========
Nimegundua kuwa bado huyu mzee anawaumiza sana kichwa mataifa ya magharibi. Nahisi ni miongoni mwa viongozi watakaokumbukwa sana Afrika.
Go Mugabe..