Mugabe awalipua Walokole

Jamani bila michango unadhani hayo matangazo ya kwenye tv utayaona?

Sent from my GT-N7100 using Tapatalk 2

Mbona Mohammedi Iddi anarusha kipindi cha Al-Sallah pale chanel ten na hatuyaoni hayo matangazo ya biashara? We jiulize kitu kimoja tu! Kwa nini matangazo ya Makanisa mengi yanakaa sehemu moja na matangazo mengine ya biashara lakini hapo huwezi kita matangazo ya Misikiti? Hao ni Matapeli tu kama vibaka wengine!
 
hahahah..gazeti gani hilo la CDM mkuu,kama ni kipeperushi cha TANZANIA DAIMA hakina tofauti na yale yaliyojimbambanua kuwa ni magazeti ya udaku,sema tu lenyewe halijajipambanua
Mkuu mimi nilisoma lile gazeti la CDM sasa nalo kumbe ni la Udaku, BTW Hawa jamaa too much sasa yaani wanatumia dini kuwaibia wajinga
 
Mugabe kafunguka ukweli
 
Mzee wa upako ye anajisifia ana magari 5 ya kutembelea tena yote ya mzungu km vogue, benz, bmw etc anadai ukingoza kanisa lililonona na mchungaji lzm anone. Nilicheka saaana

Nafikiria na mimi kuanzisha kanisa langu
 
kwani mugabe ni mkuu wa wilaya?

Chama
gongo la mboto dsm

ukiwa uganda ukisema rais kasema ukimaanisha rais kikwete hawatakuelewa, ukisema jambo ukasema rais kasema ukawa nch husika manake unamaanisha rais wa ile nchi.
 
Sio tu Zimbabwe hata hapa Tanzania walokole wamezidi kila siku wanakuja manabii tena mtu anajiita Mtume,na Nabii yani vyeo vyote vyake ukiuliza Unabii na Utume kampa nani hatujui.........wanazidi kuwanyonya wananchi bila huruma nyama hao
wako wanaofanya kazi ya mungu kweli lakini baadhi ya wachungaji wa kilokole huwapumbaza waumini kwa mistari ya biblia na kuendelea kuwanyonya kama watakavyo. wawapo kwenye mimbari wana-shine kwa suti na mavazi ya thamani kubwa wengine wanatambia utajiri wao. mmoja nilimsikia akitambia magari kibao yote toka ulaya tena ya mamilioni huku anaowatambia wanateseka kutafuta kodi ya nyumba. wengine wanasema umaskini ni laana uvivu n.k. ingawa umasikini ni mbaya hebu waseme kama sehemu ya mali zao si nguvu za waumini wao.
Imgefaa watueleze ni kwa nini Yesu hakuwa tajiri ambapo baada ya kufa kilichogawanywa ni gwanda lake pekee? Ni kwa nini alisisitiza kuwa maskini wataurithi ufalme wambigu na kufananisha matajiri na nganmia kupenya tundu la sindano?
sawa,utajiri ni mzuri, lakini basi waeleze chanzo cha utajiri wao. wanaona fahari gani wengi wa waumini wao kuwa masikini huku wakimeremeta kwa vito vya thamani?
tena huwajaza waumini hofu ya mapepo na kuwaangusha kla siku kama wako kwa waganga. sehemu kubwa ya mahubiri ni kumtolea Mungu ni sawa. lakini je , haya matoleo wao wananufaika kiasi gani?
 
Mi mwenyewe najipanga nfungue langu hapa dsm
 
Mbona Rais mwenyewe anayeongelewa aka aliye walipua Walokole ni Rais wa Zimbabwe Mr. Robert Mugabe ???

Acha chuki zako za ajabu, inaonyesha uliifungua hi thread ukiwa tayari ushaandaa majibu ya kejeli kwa rais flani ambaye una hamu tu ya kumkejeli na kuchochea udini sehem fulani.Baada ya kukuta siye unaanza kushtuka.
 
Mzee wa upako ye anajisifia ana magari 5 ya kutembelea tena yote ya mzungu km vogue, benz, bmw etc anadai ukingoza kanisa lililonona na mchungaji lzm anone. Nilicheka saaana

Huyo jamaa ana mbwembwe balaaaa....hahaha.....
 
Mwenye Chuki na Udini ni wewe, Ifike wakati tuwe tunafikiri kabla ya kuandika au kuongea. Heading na Ujumbe ni vitu viwili tofauti.
Ficha Upumbavu na Ujinga wako.

Acha chuki zako za ajabu, inaonyesha uliifungua hi thread ukiwa tayari ushaandaa majibu ya kejeli kwa rais flani ambaye una hamu tu ya kumkejeli na kuchochea udini sehem fulani.Baada ya kukuta siye unaanza kushtuka.
 
"....haya tumpige shetani kwa mwekundu wa msimbazi...mara watu wanarusha noti za elfu kumi!....anaendelea kusema wale wenye milioni tano wakae huku, wenye milioni moja na zaidi ndio wataombewa na mimi. na wale ambao wana chini ya milioni mtaombewa na msaidizi wangu...." waumini wanatoa pesa tu, wanatoa pesa tu.... ona sasa mwenzenu kajenga mishule kibao ya saint Ms! Zindukeni wa TZ... humu pia viongozi walione hili maaana wananchi wa kawaida ndio wanazidi kuwa maskini huku wakiwatajirisha akina Nabii, Mchungaji n.k
 
ukiwa uganda ukisema rais kasema ukimaanisha rais kikwete hawatakuelewa, ukisema jambo ukasema rais kasema ukawa nch husika manake unamaanisha rais wa ile nchi.

Huu ni mtandao soma habari kamili kabla ya kurukia!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mwenye Chuki na Udini ni wewe, Ifike wakati tuwe tunafikiri kabla ya kuandika au kuongea. Heading na Ujumbe ni vitu viwili tofauti.
Ficha Upumbavu na Ujinga wako.

Kumbe we ukisikia Rais tu, akili ishakimbia na kuwaza ni nani? Unasahau kuna marais mpaka wa mashirikisho na taasisi? Jipange
 
Mzee wa upako ye anajisifia ana magari 5 ya kutembelea tena yote ya mzungu km vogue, benz, bmw etc anadai ukingoza kanisa lililonona na mchungaji lzm anone. Nilicheka saaana

Hakika ni jambo la kushangaza Mzee wa Upako anapojisifia kwa mambo ya kidunia. Lakini cha kushangaza zaidi ni sisi tuliompa uwezo wa kuyanunua hayo magari ya kifahali. Ama kweli wajinga ndo waliwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…