RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Rais wa Zimbagwe, Robert Mugabe amemwambia katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki Moon awaambie(wazungu) kwa mara ya mwisho, kwa kuwapa ujumbe kama kiongozi wao kwamba kunatakiwa kuwe na usawa kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Mugabe amesema makao makuu ya umoja wa mataifa yamekaa si mahala pake 'misplaced' kwa kuhoji wapi watu wengi wapo ikiwemo India, China na Afrika kulinganisha na sura nyeupe zenye pua za pink, idadi yao wangapi hata kwa ulinganifu wa mtu kwa mtu na kuwaruhusu kuwasumbua hata kwenye nchi zao huru kwamba mfanye mabadiliko ya utawala 'Mugabe hatakiwi kuwa pale, tunahitaji mtu mwingine.'
"Kikwete alikuwa ananiambia kwamba ameambiwa kwamba hapana, chama chako, Chama cha Mapinduzi kimekuwa madarakani kwa muda mrefu, unatakiwa kuruhusu chama kingine kuchukua madaraka, hio ni demokrasia? Na hio ilikuwa inatoka Ulaya. (Moon) waambie wafunge midomo yao"