Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mufuruki: Vijana wengi hawana sifa soko la ajira

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by lifeofmshaba, Jun 17, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Fredy Azzah
  MWENYEKITI wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni zilizopo nchini, Ali Mufuruki amesema vijana wengi wanaomaliza vyuo vikuu mbalimbali nchini, wanashindwa kupata ajira kwa kuwa hawana sifa zinazotakiwa katika soko la ajira.Mufuruki alisema vyuo vingi nchini vinazalisha watu wasio na sifa na kushindwa kupata ajira katika soko la ushindani.
  Mwenyekiti huyo aliyasema hayo juzi jioni, wakati wakurugenzi hao walipokutana kwa ajili ya kula chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.Umoja wa maofisa hao wamekuwa wakikutana mara moja na pia kupata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali zinazohusiana na uchumi na biashara.“Vyuo vinazalisha watu ambao kampuni na mashirika mbalimbali hawahitaji wahitimu ambao wamesoma nadharia.

  “Kwa mfano, kama mtu umesoma Uhandisi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hapa nchini, ukaajiriwa kwenye kampuni fulani inayohusika na shughuli hizo, itabidi kampuni iliyokuajiri iingie tena gharama ya kukusomesha ili uweze kufanya kazi kwa vitendo zaidi,” ,” alisema Mufuruki.Kwa mujibu wa Mufuruki, hali hiyo ndiyo chanzo cha kampuni nyingi kuajiri watu kutoka nje ya nchi, licha ya kuingia gharama kubwa.Alisema pamoja na mambo mengine, hali hiyo inachangiwa na mitaala ya vyuo mbalimbali, kufundisha vitu ambavyo kwa sasa havihitajiki kwenye soko la ajira.
  “Ndiyo maana leo tumeamua kumwalika Mkuu wa Shule ya Bishara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS, Dk Marcellina Chijoriga ili tubadilishane mawazo, tuangalie ni kwa namna gani kwa pamoja tutaweza kukatatua tatizo hili,” alisema Mufuruki.
  Kwa upande wake Dk Chijoriga alisema shule hiyo imebaini kasoro hiyo na kwamba katika kuipatia ufumbuzi, wameamua kuanzisha mfumo mpya na kwamba wanafunzi sasa watapaswa kufanya mafunzo kwa vitendo kwa kipindi cha miezi mitatu mpaka sita.Alisema mfumo huo utaanza mwaka huu na kwamba wanafunzi watafanya mafunzo hayo mwaka wa mwisho tofauti na mwanzoni walikuwa wakiyafanya kwa miezi miwili tu.
  “Hivi karibuni nilitembelea baadhi ya vyuo huko Denmark, kule mwafunzi akimaliza mwaka wa kwanza anaenda kufanya mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu, pia mwaka wa pili na wa tatu anafanya hivyo hivyo, hii inamjengea uzoefu mzuri sana,” alisema Dk Chijoriga.
  Alisema wanafunzi wanapaswa kufanya mafunzo hayo bila kujali kama watalipwa na kampuni husika. “Huko kwa wenzetu, mwanafunzi akienda kufanya haya mafunzo, anailipa kampuni, sasa hapa kwetu hiyo hali haipo, ni vyema sasa wanafunzi wetu wakabadilisha mitizamo yao, wajue wanachoenda kufanya katika kampuni hizo ni kujifunza na siyo vinginevyo,” alisema Dk Chijoriga.
   
 2. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Walim pia tatizo, yani walim wanajifanya wako busy sana na mambo yao binafsi zaidi ya yale yahusuyo taaluma na ajira zao.
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi wanadhani tatizo ni mafunzo kwa vitendo? Hakuna creativity! Walimu wamechoka na vitabu vyao vya 1990's. Yaani mtu anasoma vislides. Labda tungerudisha ari ya kujisopmea vitabu huenda ingesaidia. Hii ya kusoma page 2 umemaliza semister ni matatizo tu!
   
Loading...