Mufti wa Tanzania aongoza dua ya kumuombea heri Rais Magufuli

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Dkt. Magufuli amemjulia hali Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubery Ally aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo amempa pole na kumuombea apone haraka.

Pamoja na kupokea pole ya Rais, Mufti wa Tanzania ameongoza dua ya kumuombea heri Rais Magufuli ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake katika kuwahudumia watanzania.

Dua kama hiyo pia imefanywa na wananchi wengine waliokuwa wakimsubiri nje ya majengo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo katika dua hiyo wamemuomba Mwenyezi Mungu kumlinda na kumuongoza katika majukumu yake ya kuiongoza nchi.

"Mwenyezi Mungu mbariki Rais wetu, mpe hekima, busara na upendo katika kazi zake za kuiongoza nchi hii ili watanzania wote wanufaike" ilisema sehemu ya dua hiyo iliyoongozwa na mmoja wa akina Mama.

Chanzo: EATV
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom