Mufti: Viongozi wa Kiislamu muombeeni Rais Magufuli

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MUFTI wa Tanzania, Shehe Abubakar Zuberi, amewataka viongozi wa dini ya Kiislamu kumuombea Rais John Magufuli aweze kuongoza nchi kwa misingi ya haki na kutunza rasilimali ziwanufaishe Watanzania wote. Aidha, amewataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawajibike kwa tija na kuleta matokeo chanya.

Mufti alitoa kauli hiyo Dar es Salaam wakati akifungua semina elekezi ya viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), iliyohusisha mashehe wa mikoa, wenyeviti wa halmashauri na makatibu wa mikoa mbalimbali nchini.

Alisema kuna umuhimu wa viongozi hao kuielimisha jamii umuhimu wa kufanya kazi na kujishughulisha katika kutafuta riziki halali na kuachana na tabia ya kutafuta kwa njia ya dhuluma kwa kuwa hata Mungu hapendi.

“Kauli ya Rais inasema ‘Hapa Kazi Tu’ tunatakiwa kuisimamia kwa kuwajibika na kuitekeleza. Tujitume katika ajira zetu na biashara ili tupate riziki ya halali katika njia zinazompendeza Mwenyezi Mungu,” alisema Sheikh Zuberi.

Katika hatua nyingine, Mufti aliwataka viongozi hao kujenga umoja, mshikamano na kusahau hitilafu walizonazo. Pia waangalie namna ya kutatua changamoto mbalimbali zilizopo. “Nyumba ni moja tunayojenga hivyo haina haja ya sisi viongozi na waumini wetu kugombea fito, tutambue kuwa sisi kama viongozi tuna jukumu la kuwajenga waumini ili wawe na tabia njema za uadilifu maana uadilifu umepotea miongoni mwetu,” alisema.

Aidha, Mufti alizungumzia suala la dawa za kulevya na alisema elimu zaidi inatakiwa kwa jamii na hasa vijana kwa kuwa ndio waathirika wakubwa. Mufti Zuberi pia aliwataka waumini wote wa dini hiyo kuwa wazalendo na kuipenda nchi, huku akihimiza viongozi kutumia majukwaa vizuri kwa kuhamasisha upendo na mshikamano ili kuendeleza amani iliyopo.

Semina hiyo ya kwanza kufanyika, iliambatana na mada mbalimbali zikiwamo utiifu kwa viongozi, utawala bora, uchumi na maendeleo, kubadilika kutoka kwenye ufanyaji kazi kwa mazoea pamoja na mambo mengine.
 
Mimi ni wa kwanza kumuunga mkono Rais JPM.Kwa Mwenyezi Mungu ni MWENYE HAKI na anawapenda watendao na kusimamia HAKI,hatuna budi waislamu wote kumuunga mkono kila mwenye kusimamia haki bila ya kujali imani yake.
 
Mufti wa Bakwata hawezi kuongea chochote kisichoifurahisha serikali.
 
masheikh wenzako wanahangaika jela kwa ajili ya serikali ya ccm lkn umeshindwa kutoa neno...napata mashaka na umufti wako.....nb tunamuombea mh raisi aendelee kufanya kazi kwa weledi....lkn mufti acha uoga watetee masheikh au hukumu itolewe ushahidi gani miaka haukamiliki...hiyo ni dhima unaibeba amiri unashindwa kutetea haki.....maybe unatetea tumbo
 
Wamuombee kwani anaumwa nini?? Ametaja watumie sura ipi katika "kusoma"

Maana kama ni maradhi sisi tunayo kumbukumbu kuwa mzee ambilikile alimpa dawa kwenye kikombe.

Mweye picha aiweke ili na mufti aione.
 
Amuambie kwanza huyo Rais aanze kuonyesha haki kwa wapinzani wake na awaachie masheikh amabao wanashikiliw kwa dhulma hapo ndio ageukie kwetu waumini ndio tutamsikiliza
 
Back
Top Bottom